Tafuta

2026.06.21 Angelus

Papa Leo XIV:Tuendelee kupitisha ujumbe wa matumaini,upendo na amani.Ulimwengu unahitaji sana!

Leo kama ilivyokuwa hapo awali,jitihada kubwa inabaki aminifu kwa mafundisho ya Yesu na kutangaza Neno lake:kujibu chuki kwa upendo,nguvu kwa upole,kukata tamaa kwa uvumilivu.Ni lazima kukabidhi mizizi ya imani yetu na utume wetu katika mahusiano ya kina na Bwana. Kwa sababu anatunapatia nguvu ya kutoacha na kuendelea kupitisha kwa wote,na kwa kila hali,ujumbe wake wa matumaini,upendo na amani.Ulimwengu unahitaji sana!Papa Leo XIV alisema hayo Dominika Juni 21.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza tafakari yake Dominika tarehe 21 Juni 2026 akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume mjini Vatican, kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika uwanja wa Mtakatifu Petro. Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana, Papa alisema: “Katika Injili ya Luturujia ya leo(Mt 10,26-33), Yesu anawatuma mitume katika utume, lakini mbali na hayo anawapa ushauri kuwa: “Niwambialo ninyi katika giza, lisemeni katika nuru; na msikialo kwa siri, lihubirini juu ya nyumba(Mt 10, 27). Kuna jambo la kutilia maanani ambalo tunasikiliza “katika masikio”, yaani katika siri ya moyo na kile ambacho tumeitwa kutangaza kwa wote, kwa kutukumbusha kuwa tangazo la Injili, awali ya yote ni kushirikishana kwa mkutano binafsi na Yeye, kipekee na  kwa kila mtu.

Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Nguvu ya utume, kiukweli mbali na ufundi na zana, inajikita katika kazi ya Roho Mtakatifu ndani mwetu na juu ya udhati wa jibu letu. Mtakatifu Thomas wa Aquino alikuwa akizungumza juu kuhubiri kama kuonesha wengine kile ambacho tunatafakari (Summa Theologiae,III,1,2). Na hakuna haja ya kufikiria kuwa “kutafakari “kunakuwa uzoefu pekee, uliohifadhiwa na baadhi ya watakatifu au wamonaki na watafakuri. Wote wanaweza kufanya, kujitahidi kuhifadhi, kama ya jitihada za siku zetu, wakati wa wasiwasi ambao unatuweka katika ukimya mbele ya Mungu, ili kusikiliza sauti yake, kukamkabidhi furaha zetu na wasiwasi wetu, kutazama upya na Yeye maisha yetu.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea “hii inatufanya daima kuwa watu wa imani thabiti na utambuzi, na matokeo yake, kuwa mitume waaminifu na huru, wanaume na wanawake wenye uwezo wa kutafakari katika nuru ya Injili kila maezingira na kila hali ya maisha, na kumshuhudia mahali ambapo thamani yake haijatambuliwa au kukubaliwa. Mtakatifu Matayo, mwandishi ya kifungu cha Injili ambacho tunafafanua, alikuwa akiwaandikia Jumuiya ambayo maisha hayakuwa rahisi. Walikuwa wakabiliana na vizingiti na mateso, kama jinsi inavyotokea hata leo hii kwa Wakristo wengi katika maeneo mengi ya dunia, na kishawishi cha kukata tamaa na kushindwa uchovu au hofu iliyokuwa kubwa zaidi.”

Papa Leo XIV alibanisha kuwa leo hii  kama ilivyokuwa hapo awali, jitihada kubwa inabaki aminifu kwa mafundisho ya Yesu na kutangaza Neno lake: kujibu chuki kwa upendo, nguvu kwa upole, kukata tamaa kwa uvumilivu. Kwa njia hiyo ni lazima kukabidi mizizi ya imani yetu  na utume wetu katika mahusiano ya kina na yeye(Evangelii gaudium, 8). Baba Mtakatifu aliongeza, kwa “hiyo inatunapatia nguvu ya kutoacha na kuendelea kupitisha kwa wote, na kwa kila hali ujumbe wake wa matumaini, wa upendo na wa amani. Ulimwengu unahitaji sana! Bikira Maria atusaidie kuwa mitume wamisionari wa Bwana Yesu, kila mmoja kwa mujibu wa wito wake.”

Sala ya Malaika wa Bwana,Dominka 21 Juni
Papa Kabla ya sala ya Malaika wa Bwana,Juni 21

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

21 Juni 2026, 12:20