Tafuta

Papa Leo XIV:Ni huruma tu inayookoa ubinadamu,unaohitaji msamaha na upatanisho

Papa Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa Takatifu huko Tenerife,Juni 12 ikiwa ni hitimisho la Ziara yake ya kitume nchini Hispania.Katika mahubiri kwa mtazamo wa sherehe ya Moyo Mtakatifu alisema,tuhoji mioyo yetu,tukisukumwa kila mara kutoka ndani.Kuna uzima tunapotoa maisha yetu na tusipunguze kila kitu kwa biashara na faida.Katika visiwa vilivyo katikati ya njia panda za uhamiaji,vinakabiliwa na wanaohisi kukata tamaa.Wakristo lazima wawasaidie.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV alihitimisha Ziara yake ya nne ya Kitume kwa kuongoza Ibada ya Misa Takatifu iliyoadhimishwa Ijumaa tarehe 12 Juni 2026, sambamba maadhimisho ya Sherehe ya Moyo Mtakatifu. Baba Mtakatifu akiwa katika Uwanja wa Bandari ya (Santa Cruz de Tenerife), yaani Msalaba Mtakatifu wa Tenerife, alielezea hisia za shukrani kwa waamini takribani 40,000 waliokuwapo na kuwasihi waendelee kuishi kwa umoja na ushirika. “Ninarudi Roma nikisukumwa na upendo mkubwa ulionizunguka na kufarijiwa na ushuhuda wa imani na upendo kwa Kanisa, vielelezo vya moyo mkuu wa Kikatoliki wa Hispania,” Papa Leo alisema.

Papa katika njia za Tenerife
Papa katika njia za Tenerife   (@Vatican Media)

Kauli mbiu: !Alza la mirada"

Baba Mtakatifu kabla ya misa alifika kwenye kigari cha kipapa, alizunguka kuwasalimia na kuwabariki maelfu ya wamini waliokusanyika hata barabarani kumwona akipita, huku wakimpiga picha, na kumkaribisha ambapo,  Papa  alionekana kuwa na furaha kubwa ya umati huo. Kwa hakika ilipendeza kusikia hata wimbo "Alza la mirada,"inua macho yako, kama kauli mbiu ya ziara ya Papa, ambao umeimbwa mara nyingi katika siku hizi za uwepo nchini Hispania. Watu  walioneakana wameshika bendera, mabango katikati ya kofia zenye rangi nyingi kwa ajili kujikinga jua kali. Watu mbalimbali wa Mungu, vijana, barubarua, watoto pamoja na wazazi wao walimsifu kwa furaha na kumshangilia mrithi wa 266 wa mtume Petro, lzaidi ya hayo walikusanyika pamoja, wakiongozwa na kwaya na wanamuziki, mara tu Papa alipofika kwenye sakristia kuvaa mavazi yake ya kiliturujia.

Waamini zaidi ya 40,000 waliudhuria misa
Waamini zaidi ya 40,000 waliudhuria misa   (@Vatican Media)

Wahamiaji wanaoanza safari ya Atlantiki kutafuta mustakabali bora

Katika mahubiri ya  Papa alitoa maneno ya shukrani, ikiwa ni  sherehe ya mwisho katika ardhi ya Hispania. "Neema katika Sherehe ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, siku ambayo moyo wa Kristo unaturuhusu kuutafakari kama kitovu cha historia lakini pia sababu ya furaha kwa ushuhuda mwingi wa "imani" na "upendo" uliopokelewa katika siku za hivi karibuni. Tafakari yake, ambayo ilianza na Visiwa vya Kanari, mahali ambapo maelfu ya wahamiaji wanaoanza safari ya Atlantiki kutafuta mustakabali bora, na ambapo mabaharia, wakujitolea, Kanisa, Caritas, mashirika, vyama, na watu wa kawaida wanafanya juhudi zozote kuwakaribisha, hugusa moyo wa kila mtu. Mahali pa kijiografia pa Jimbo hili na changamoto za kichungaji zinazokabiliana nazo zinashuhudia kwamba tulizaliwa kwa ajili ya kukutana na kwamba hakuna kikwazo," Papa alisema.

Papa wakati anaelekea Altareni
Papa wakati anaelekea Altareni   (@Vatican Media)

Siri ya moyo wa mwanadamu

Akitazama ndani ya mwanadamu, Askofu wa Roma anaelezea kwamba "siri ya moyo" ni "wito wa ndani wa kutoka na kukutana, kwa hivyo, hakuna mtu ambaye ametulia, awe anabaki mahali pamoja kwa ajili ya maisha yote, au kuchagua au kulazimishwa kuondoka." Na Yesu, kwa mfano wake, anatufundisha jinsi ya kutojipoteza katika nguvu tasa. Kuna uzima tunapotoa maisha yetu. Vinginevyo, tunatangatanga bure. Hakika, "kama Mtaguso  unavyokumbusha, mwanadamu anaitwa kwenye ushirika na Mungu na 'hawezi kujipata kikamilifu isipokuwa kupitia zawadi ya dhati ya nafsi': wito wake mkubwa zaidi ni kuingia katika harakati ya Utatu ya upendo unaopokelewa na kushirikishwa."

Mbele ya Sanamu ya Bikira Maria
Mbele ya Sanamu ya Bikira Maria   (@Vatican Media)

Tenerife kama kivutio cha watalii

Papa Francisko alisisitiza hili katika Barua yake ya Laudato Si': "Watu wengi hupata ukosefu wa usawa mkubwa unaowasukuma kuharakisha mambo ili kujishughulisha, katika msongamano wa mara kwa mara ambao nao unawaongoza kuzidi kila kitu kinachowazunguka,"  akitualika kuzingatia maneno ya mtangulizi wake, ikiwa ni pamoja na yale kuhusu "wito wa Tenerife kama kivutio cha watalii." Hivyo, "kwa mioyo ya wale wanaochagua kutumia likizo hapa" na "wale wanaoishi na kufanya kazi kisiwani humo wakiwasiliana na wageni kutoka nchi nyingi duniani," Papa aliuliza swali. Moyo wa mwanadamu unatamani nini? Tunawezaje kujibu kiu yake kwa njia isiyo ya udanganyifu? Ni muhimu sana, hasa kwa wale wanaoongozwa na Injili, kutopunguza kila kitu katika biashara na faida."

Altare ya Misa katika Bandari
Altare ya Misa katika Bandari   (@Vatican Media)

Watu wa Tenerife wanajifafanua kwa ukarimu

Katika Laudato si' inabainisha zaidi kwamba "wale wanaofurahia zaidi na kuishi vizuri zaidi kila wakati ni wale wanaoacha kuchokonoa hapa na pale, kila mara wakitafuta wasichonacho", wanaothamini "kila mtu na kila kitu" na kufurahia "uhalisi rahisi zaidi". "Tafasiri hizi aliongeza kuwageukia waamini kuwa ni, wito wao wa kuwakaribisha. Papa kwa Watu wa Tenerife  alionesha njia ya Injili ambapo "utajiri wa maskini unajitokeza: kitendawili ambacho kinahusu moja kwa moja maisha ya Yesu, ukweli wake, ni njia ambayo bado anatuomba tumfuate". Wale wadogo, “wale ambao hakuna mtu anayewaona kuwa na uwezo wa kufikiri na kuzungumza”, ambao “Mungu amejifunua kwao”, wametajirishwa na Mungu “kwa yale ambayo yamesalia yaliyofichwa kutoka kwa wale ambao wamezungukwa na sifa na mafanikio,” Papa alisema.

Familia walipeleka vipaji
Familia walipeleka vipaji   (@Vatican Media)

Upendeleo wa Mungu kwa walio wadogo

Papa Leo XIV alibanisha alivyotaka kuvuta "umakini  wa "mahali hapa pazuri pa maskini katika Ufunuo wa Kimungu na katika utume wa Kanisa" pamoja na Waraka wake wa Kitume Dilexi te. Hata katika Visiwa vya Kanari, "katikati ya njia za uhamiaji zinazozifanya kuwa mahali pa makaribisho ya awali kwa kaka na dada ambao safari yao kwa ujumla inakabiliwa na hatari na vurugu zisizoelezeka," upendeleo wa Mungu kwa wale walio na bahati mbaya hujitokeza. Mbele ya wale wanaofikiria kuhusu kukata tamaa, kama Wakristo hatuwezi kutoa tu taswira ya Bwana anayesema, "Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha" (Mt 11:28).  Badala yake neema kubwa zaidi ni kwamba tujiruhusu kuhubiriwa Injili  na wale tunaowasaidia, kwamba tunatambua hekima ya siri ya Mungu iliyoandikwa katika miili yao."

Papa wakati wa kuhubiri
Papa wakati wa kuhubiri   (@Vatican Media)

Mungu anajua kukemea,anataka maisha ya Kanisa yawe rahisi na furaha

Maskini wamejifunza mengi kwa kukua "katika hali ngumu sana, wakijifunza kuishi katika hali mbaya zaidi, wakimtumaini Mungu kwa uhakika kwamba hakuna mtu mwingine anayewachukulia kwa uzito, wakisaidiana katika nyakati za giza zaidi," Papa aliongeza, akinukuu tena Dilexi te. Huu ni "uzoefu wa maskini," na tukiunganisha malalamiko yetu na mateso na umaskini wao, tunaweza kupokea karipio linalotualika kurahisisha maisha yetu." Kwa sababu Mungu, "anayewakemea na kuwarekebisha wale anaowapenda, anatamani" kwamba "maisha ya Kanisa" yawe "rahisi na ya furaha."

Waamini katika misa
Waamini katika misa   (@Vatican Media)

Kufikiria tena kina cha moyo usiotulia

Kwa ufupi, akiwa na maskini, wahitaji, wahamiaji, na walio katika mazingira magumu zaidi akilini, Papa Leo XIV aliwashukuru Watu wa Kanari. "kwa kile mlicho, asanteni kwa kile mnachofanya, mkifanya kisiwa hiki kuwa mahali ambapo tunakutana na moyo wa Kristo katika nyuso za kirafiki na za kukaribisha za watu binafsi na jamii za kidugu." Na aliomba kufikiria sana  wema kwa majirani zetu."  Zaidi Papa aliwaomba wazingatie hasa vijana na barubaru, matajiri na maskini, wakazi na wageni: wanahitaji kujulikana kwa mtazamo unaoona zaidi ya mwonekano na kutambua kina cha mioyo yao isiyotulia, ambayo mara nyingi tayari imeelekezwa, labda bila kujua, kwa Ufalme wa Mungu na haki Yake." Matumaini ya Papa Leo XIV  ni kwamba tunaweza kupumua moyo wa Injili, moyo wa Kristo, kwamba Mungu ni upendo; yeyote akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake." Fungulieni bahari hii ya upendo kwa kila mtu! Hili ndilo ombi langu na maombi yangu kwa ajili yenu na kwa wale wote mnaokutana nao katika safari yenu.”

Baba Mtakatifu katikati ya Maaskofu
Baba Mtakatifu katikati ya Maaskofu   (@Vatican Media)

Ni Wakati wa Neema kwa Kanisa la Njia Panda

Mara baada ya Misa, miongoni mwa nyimbo za mwisho kulikuwa na onyesho la Tardi ti amai - Nilipenda nimechelewa, lililochukuliwa kutoka katika Ungamo la Mtakatifu Agostino na salamu kutoka kwa Askofu wa Mtakatifu Cristóbal,  Askofu Santiago Eloy Alberto Santiago, ambaye aliita ziara ya Papa Leo XIV, ya kwanza na Papa kwa Jimbo la Tenerife, kama: "wakati wa neema kwa Kanisa hili maalum lililoko katika Njia panda ya Ulaya, Amerika, na Afrika." Askofu alitoa shukrani zake kwa niaba ya Kanisa dogo,  la unyenyekevu" la mahalia, ambalo, linatamani kuwa Kanisa la Heri, Kanisa linalowapatia nafasi watoto wadogo na kutembea katika umaskini na maskini."

Maaskofu wakati wa misa katika Bandari ya Tenerife
Maaskofu wakati wa misa katika Bandari ya Tenerife   (@Vatican Media)

"Papa pia ni Mkanari atakuwa na nyumba yake katika visiwa hivi kila wakati"

Askofu alimwakilishia kuwa: "Tutegemee, Baba Mtakatifu, kwa ajili ya kazi ya  uumbaji wa Kanisa ambalo ni chachu ya ulimwengu uliopatanishwa, lenye uwezo wa kuhifadhi na kulea ubinadamu wa ajabu, lililotolewa kama zawadi, likiheshimu utu wa binadamu, likilinda haki za msingi za binadamu, na kukuza maendeleo kamilifu ya binadamu,” na lenye uwezo wa kuongoza “ukuaji wa udugu wa binadamu na urafiki wa kijamii.” Kwa hiyo, Askofu wa Mtakatifu Cristóbal alisisitiza kwamba wametiwa "moyo kuinua macho yetu, kama kauli mbiu ya ziara  ya kitume inavyosema, kuelekea Kristo, tukihisi kutiwa moyo katika uinjilishaji; katika kuwatunza maskini na wahamiaji; na katika kujenga jamii yenye haki zaidi na udugu, ambamo amani ya unyenyekevu na endelevu huishi. Bila kusahau, utunzaji wa nyumba yetu ya pamoja, inayoonekana katika uzuri na bioanuwai iliyopo katika Visiwa vya Kanari. Papa ni mmoja wetu. Papa Leo XIV pia ni Mkanari na atakuwa na nyumba yake katika visiwa hivi kila wakati.”

Wakati wa kupokea zawadi ya kikombe
Wakati wa kupokea zawadi ya kikombe   (@Vatican Media)

Shukrani kwa wote walioandaa ziara yake kuanzia Madridi hadi Kanari

Makofi makubwa yalipigwa, na Papa Leo XIV, mara baada ya kumpatia Askofu wa Mtakatifu Cristóbal kikombe, na alijibu kwa shukrani za dhati kwa kila mtu aliyemkaribisha na "kwa njia elfu, kwa  walioshirikiana katika maandalizi na utekelezaji wa matukio mbalimbali huko Madrid, Barcelona, ​​​​Montserrat, na hapa katika Visiwa vya Kanari." Kutoka Bandari hii, ambayo ina jina la Msalaba Mtakatifu, mawazo yangu yanaenea kwa ulimwengu mzima na majeraha yake, ambayo husababisha mateso kwa watu wote.

Mtazamo wetu kwa Kristo Msulibiwa

Papa alielendelea: "Kwa kila mtu, ningependa kushughulikia kauli mbiu ya Safari hii: "Inua macho yako juu! "mtazamo wetu kwa Kristo Msulibiwa," ambaye moyo wake "ndiyo chanzo cha huruma, ambacho pekee kinaweza kuokoa wanadamu wanaohitaji msamaha na upatanisho ili kufikia amani ya kweli na ya kudumu": hii ndiyo pendekezo la mwisho la Papa. Lakini kabla ya kuondoka, pia alialika tutembee "kwa matumaini,"kwa kuongozwa na Maria, hadi altareni tukiwa na uso wa Bikira wa Candelaria, mlinzi wa Visiwa vya Kanari, na kubaki "tumeungana katika sala na katika ushirika katika Kristo na Kanisa Takatifu."

Furaha ya waamini katika misa
Furaha ya waamini katika misa   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

MAHUBIRI PAPA HITIMISHO
Papa aliongoza Misa katika Kisiwa cha Tenerife Juni 12.
12 Juni 2026, 16:30