Tafuta

Papa Pio XI kunako tarehe 11 Juni 1932 katika Katiba yake ya Kitume “Christo Pastorum Principi” Yani “Kristo Mkuu wa Wachungaji” miaka 95 iliyopita alipoanzisha rasmi utawala wa Kanisa la Siro Malankarese, Papa Pio XI kunako tarehe 11 Juni 1932 katika Katiba yake ya Kitume “Christo Pastorum Principi” Yani “Kristo Mkuu wa Wachungaji” miaka 95 iliyopita alipoanzisha rasmi utawala wa Kanisa la Siro Malankarese,   (ANSA)

Papa Leo XIV: Kanisa la Siro Malankarese: Umoja wa Kanisa

Papa Leo XIV amekumbushia kwamba, ilikuwa ni Papa Pio XI kunako tarehe 11 Juni 1932 katika Katiba yake ya Kitume “Christo Pastorum Principi” Yani “Kristo Mkuu wa Wachungaji” miaka 95 iliyopita alipoanzisha rasmi utawala wa Kanisa la Siro Malankarese, tangu wakati huo, kumekuwepo na viongozi mbalimbali waliowaongoza, wafundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu katika hija ya maisha yao hapa duniani, wote hawa Mama Kanisa anawashukuru na kuwapongeza!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kwa mara ya kwanza waamini wa Kanisa la Siro Malankarese wanaoishi Barani Ulaya, wanafanya kongamano lao la kwanza chini ya uongozi wa kardinali Baselios Mar Cleem ambaye, leo tarehe 15 Juni 2026 anaadhimisha kumbukizi ya Miaka 67 tangu alipozaliwa na Mwezi Agosti 2026  anaadhimisha Jubilei ya Miaka 25 tangu alipowekwa wakfu kuongoza, kufundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu, maadhimisho ambayo tayari yameanza kutimua vumbi mjini Roma, kwa uwepo na ushiriki wa Askofu Kuriakose Mar Osthathios aliyeteuliwa hivi karibuni na Baba Mtakatifu Leo XIV kuwa Mwangalizi wa Kitume wa Kanisa la Siro Malankarese wanaoishi Barani Ulaya.

Miaka 95 ya Kanisa la Siro Malankarese
Miaka 95 ya Kanisa la Siro Malankarese   (@VATICAN MEDIA)

Wajumbe wa Kanisa hili Jumatatu tarehe 15 Juni 2026 wamekutana na kuzungumza na Baba Mtakatifu Leo XIV. Katika hotuba yake amekumbushia kwamba, ilikuwa ni Papa Pio XI kunako tarehe 11 Juni 1932 katika Katiba yake ya Kitume “Christo Pastorum Principi” Yaani “Kristo Mkuu wa Wachungaji” miaka 95 iliyopita alipoanzisha rasmi utawala wa Kanisa la Siro Malankarese, tangu wakati huo, kumekuwepo na viongozi mbalimbali waliowaongoza, wakawafundisha na kuwatakatifuza watu wa Mungu katika hija ya maisha yao hapa duniani, wote hawa Mama Kanisa anawashukuru. Wote hawa wamejenga na kudumisha umoja na ushirika na Khalifa wa Mtakatifu Petro, kama kielelezo cha kuishi, kutangaza na kushuhudia Imani yao kwa Kristo Yesu na Kanisa lake, Viongozi wakuu wametamani kuona umoja na ushirika wa Kanisa unajengwa na kuimarishwa, kama chachu ya upatanisho wa Ulimwengu.

Umoja wa Kanisa ni muhimu sana kama ushuhuda wa Injili
Umoja wa Kanisa ni muhimu sana kama ushuhuda wa Injili   (@VATICAN MEDIA)

Imani ya Kanisa hili ni matunda na kazi ya Mtakatifu Thoma, Mtume, aliyekazia kwamba, uinjilishaji wa kina, hauna budi kumwilishwa katika matendo ya huruma: kiroho na kimwili, yaani katika Injili ya huduma ya upendo, kwa kujikita katika haki msingi za jamii, elimu, ustawi, maendeleo na mafao ya wengi na kwamba, ushuhuda wa Injili ni sumaku yenye mvuto kwa watu wengi kutaka kukutana na Kristo Mfufuka. Hiki ni kielelezo cha mvuto kutoka kwa Kristo Yesu mwenyewe, kwa njia ya nguvu ya upendo wake, aliweza kuwavuta watu wengi kwake na hatima ya upendo huu ni mateso, kifo na ufufuko wake kwa wafu!

Uinjilishaji wa kina: Mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili
Uinjilishaji wa kina: Mahitaji ya mtu mzima: kiroho na kimwili   (@VATICAN MEDIA)

Kazi ya Uinjilishaji wa kina unaogusa mahitaji msingi ya binadamu: kiroho na kimwili, ilianza kunako mwaka 1934, huko Tamil Nadu nchini India, leo hii Kanisa hili limeenea sehemu mbalimbali za dunia na kwamba, watawa wa Shirika la Maria, wameenea sehemu mbalimbali za dunia. Hii ni changamoto anasema Baba Mtakatifu Leo XIV amechukua fursa hii kuwahimiza wajumbe wa Sinodi pamoja na Taasisi mbalimbali za maisha ya wakfu zimendelee kushikamana na kukua. Baba Mtakatifu Leeo XIV hivi karibuni ameunda Jimbo jipya la Kanisa nchini India, lakini bado Kanisa hili ni dogo kwani idadi ya wahamiaji na wakimbizi inazidi kuongezeka maradufu na kwamba, yalikuwa ni matumaini ya Baba Mtakatifu Leo XIV kukutana na kuzungumza na washiriki wa Jubilei, lakini bado alikuwa ni mgeni ofisini, lakini alishuhudia umati wa watu wa Mungu kutoka sehemu mbalimbali za dunia wakishiriki. Askofu Kuriakose Mar Osthathios ndiye mhusika mkuu wa waamini wa Kanisa la Siro Malankarese wanaoishi Barani Ulaya.

Umoja na Mshikamano wa Kanisa katika maisha na utume wake
Umoja na Mshikamano wa Kanisa katika maisha na utume wake   (@VATICAN MEDIA)

Tayari Baba Mtakatifu Leo XIV amekwisha liomba Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki kumsaidia kupata mwongozo, ili kumwezesha Askofu wa Makanisa ya Mashiriki kutekeleza wajibu wake wa kufundisha, kuongoza na kuwatakatifuza watu wa Mungu sanjari na kuanza kuweka misingi ya mafundisho tanzu ya Kanisa itakayolifaidisha Kanisa Katoliki katika ujumla wake. Watambue, wathamini na kukuza utambulisho wao kwa kushiriki kikamilifu katika maisha na utume wa Kanisa; kwa kujikita katika tajiriba, amana na utajiri wa Sinodi ya Maaskofu na kwamba, Kanisa hili limekuwa ni chimbuko la miito mbalimbali ya Kipadre na Kitawa ndani ya Kanisa. Baba Mtakatifu Leo XIV anaendelea kusali hili kwamba, ushuhuda huu wa imani thabiti kwa Kristo Yesu na Kanisa lake, uendelea kushamiri ndani ya familia, nyoyoni mwa waamini na hasa miongoni mwa vijana wa kizazi kipya. Hatimaye, Baba Mtakatifu Leo XIV amewapatia baraka zake za kitume.

Umoja wa Kanisa
15 Juni 2026, 15:11