Papa Leo XIV atembelea Wafungwa wa Brians:Turuhusu upendo wake utuongoze!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Ushuhuda wa Montse na Josefina umengana na ule wa Padre Jesús Bel Gaudó, wa Shirika la Mercedarian, Padre anayehudumia gereza lililoko katika manispaa ya Mtakatifu Esteve Sesrovires, Barcelona, iliyotembelewa asubuhi tarehe 10 Juni 2026 na Papa Leo XIV, katika siku ya tano ya Ziara yake ya kitume nchini Hispania. Mkurugenzi wa kituo cha gereza ambacho kwa sasa kinawashikilia wanaume elfu moja na wanawake 150 wakisubiri kesi, alimkaribisha Papa Leo XIV. Hata hivyo, baadhi ya wafungwa kutoka vituo vya Brians 2 na Wad Ras, uwakilishi mdogo wa jumuiya ya Wakristo ya wafungwa kutoka Katalonya, pia walikuwepo kwa kuwasili kwa Askofu wa Roma.
Mara baada ya shuhuda hizo Baba Mtakatifu alitoa tafakari yake. Asanteni nyote kwa makaribisho yenu ya joto na ya kirafiki! Nimeguswa sana na ushuhuda ulioshirikishwa na Montse na Josefina. Asante sana. Pia nathamini maneno ya Padre Jesús, ambayo yanaakisi kujitolea kwa mapadre na watu wa kujitolea wa huduma ya gereza la Jimbo huko Mtakatifu Feliu de Llobregat. Baba Mtakatifu alisisitiza kwamba, “Kila mwanadamu anastahili tu kiukweli, kwa kuwa amekusudiwa, ameumbwa na kupendwa na Mungu"(Magnifica Humanitas, 52). Kwa hivyo, hakuna hali inayomfanya Bwana asitututazame kwa macho. Ni ukweli unaotufariji unaotusindikiza wakati wote na kutukumbusha jinsi upendo wake wa huruma unavyozidi wema au uovu wowote ambao tunaweza kuwa tumefanya.”
Makosa hayabainishi maisha ya mtu,inawezekana kubadilika
Baba Mtakatifu alisema kuwa, "hii ni kweli hasa kwenu mnaobeba mzigo wa kuwa mbali na wapendwa wenu na mnaoteseka kwa sababu ya hali zenu za sasa. Mnapojaribiwa kujisikia duni na kudhani haifai kuendelea, "inua macho yenu" kwa Yule ambaye, kupitia uwepo wa watu wengi, haachi kamwe kuwaonesha upendo na ukaribu wake. Hata kama wasiwasi na huzuni vinaashiria nyakati fulani za safari yako, kumbuka kwamba makosa ya maisha hayabainishi utambulisho wa mtu. Mtakatifu Agostino katika maungamo yake, anazungumzia hili anaposhirikisha safari yake ya maisha nasi.
Tumtengezee Bwana nafasi
Papa kisha alisisitiza kuwa "Tukiamini neema ya Mungu na kujiruhusu kuongozwa na kubadilishwa nayo, tunagundua katika maisha yetu jinsi yaliyopita hayahukumu wakati ujao, bali yanatupa uwezekano wa kubadilisha maamuzi na chaguo zetu. Tumtengenezee Bwana nafasi mioyoni mwetu na kuutafuta uso wake. Turuhusu upendo wake utuongoze. Tumshikilie, ambaye hutualika kila mara kutumaini na kutuonesha upeo mzuri ambao hakuna kizuizi cha kimwili kinachoweza kutuzuia kuufikia. Leo hii, anaendelea kuzungumza nasi katika kina cha dhamiri zetu, akitusaidia kugundua kwamba anakaa kati yetu. Anatusubiri tu tumpe nafasi," Papa alisema.
Ninawaalika kuendelea kuota ndoto ya Mungu
Papa alitoa mwaliko kwako kuwa "Wapendwa, ninawaalika mwendelee kuota ndoto ya Mungu. Kwa kila mmoja wenu nawaambia: Mungu anawapenda kama mlivyo, lakini anaota mkiwa bora zaidi! Bwana anaturuhusu sote kuanza upya, kwani kuwa mwanadamu na kuwa Mkristo haimaanishi kutofanya makosa kamwe, bali kukua katika uwezo wa kubadilisha, kutubu, kurekebisha na, zaidi ya yote, kupatanisha na kusamehe. Ninakukabidhi kwa njia ya pekee kwa maombezi ya mama ya Mama Yetu wa Huruma, na ninamwomba Bwana kwa hiari awabariki. Asante sana,” Papa alihitimisha.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
