Papa Leo XIV,Watu wa kujitolea:Wakristo wameitwa kuleta chachu ya ukarimu kwa ulimwengu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Hitaji la kufikiria na kuishi kulingana na mantiki ya maendeleo fungamani ya binadamu limesikika katika hotuba ya Baba Mtakatifu XIV akihitimisha hija yake mjini Madrid kwa kukutana na watu wa kujitolea 17,000 katika Ukumbi wa 3 wa IFEMA, jijini Madrid, Jumanne tarehe 9 Juni 2026 kabla ya kupanda Ndege kuelekea mji wa Barcelona ikiwa ni sehemu yake ya Pili ya Ziara ya 4 ya Kitume nchini Hispania iliyoanza tangu Juni 6 na itahitimishwa 12 kwa kutembelea pia Visiwa vya Kanari na Tenerife. Banda hilo la 3 ni moja ya taasisi tano muhimu zaidi za maonyesho ya biashara barani Ulaya, moja kuu nchini Hispania ambapo alifika kwa gari katikati ya watu wa kujitolea, waliotambulika kwa rangi ya machungwa.
Shukrani kwa wote kwa kutoa uwepo wao
Katika hotuba yake Askofu wa Roma alianza na shukrani kwa Kardinali, José Cobo Cano, Askofu Mkuu wa jiji kuu la Madrid, kwa kaka na dada wapendwa, na kuwapa habari za asubuhi! “Mkutano huu ni wa mwisho wa ziara yangu ya Kitume ya Madrid, lakini ninafurahi sana kuwa hapa nanyi, wajitolea”Papa alisema. Hapa wote walisikika wakitoa ukelele wa kusikitika, na Papa akaendelea. “Kila mmoja wenu, na wengine wengi ambao hawakuweza kuwa hapa asubuhi ya leo, wanastahili "shukrani" maalum sana, kwa sababu mmetoa uwepo wenu na huduma yenu, na mmefanya hivyo kwa upendo kwa Bwana, Kanisa, na Papa.”
“Asante kutoka ndani ya moyo wangu! Ninawashukuru "wazungumzaji" wawili walioshiriki ushuhuda wao nasi na wale waliotengeneza video na onyesho la muziki.” Papa aliendelea kusema kuwa “Nimejifunza kwamba, tangu mwanzo, majibu yenu kwa wito yamekuwa ya shauku: katika siku chache mmezidi takwimu zilizoombwa na hivyo mahitaji yamefunikwa kwa kiasi kikubwa. Mmechukua siku mbali na kazi, wengine wako wamejitolea muda wote kwa miezi, lakini kila mmoja ametoa kile alichoweza, kutoa moyo, mikono, maoni, talanta, tabasamu. Mungu awalipe kama yeye pekee ajuaye kufanya!”
Yesu alitumia mfano wa chachi kuhusu Ufalme wa Mbingu
Baada ya kusema hayo, lakini Papa alipenda kushirikishana nao tafakari rahisi, ambayo alisema kuifupisha kama ifuatavyo: “Wakristo wameitwa kuleta chachu ya ukarimu kwa ulimwengu. Yesu alitumia taswira ya chachu katika mfano kuhusu Ufalme wa Mbinguni, ulioandikwa na mwinjili Mathayo: “Ufalme wa Mbinguni ni kama chachu ambayo mwanamke aliichanganya na takriban pauni sitini za unga hadi ukachachuka wote” (Mt 13:33). “Uzoefu wenu siku hizi, kama ule wa kaka na dada wengi, wanaojitolea katika hali kama hizo”, Papa aliongeza ninafikiria Jubilei ya mwaka jana(2025) ni ishara ya Ufalme ujao, na ni hivyo kwa sababu ya kipengele kimoja muhimu cha “ukarimu.” Utoshelevu ni chachu inayokuza ukuaji wa kibinadamu, kimaadili, na kiroho wa jamii, kwa sababu tunaweza kusema ni sifa ya kawaida ya "Mji wa Mungu."
Ulimwengu unathiriwa na mantiki ya ubinafsi na faida
“Katika ulimwengu unaoathiriwa kila mara na mantiki ya ubinafsi na faida, ambapo neno "ukuaji" hupunguzwa hadi kiwango cha kiuchumi na kifedha, ni muhimu kufikiria na kuishi kulingana na mantiki ya kweli zaidi, ile ya ukuaji fungamani wa mwanadamu. Ni mantiki ya Injili, ambayo inasema: "Mkiwatendea mema wale tu wanaowatendea mema, mna sifa gani? Hata wenye dhambi hufanya hivyo. Na mkiwakopesha wale mnaotarajia malipo kutoka kwao, mna sifa gani?" (Lk 6:33-34),” Papa alibainisha.”
Kristo alikuja kuleta chachu duniani ya ufalme wa Mbinguni wa haki na amani
“Kaka na dada wapendwa, Yesu Kristo alikuja kuleta duniani chachu ya Ufalme wa Mbinguni; aliichanganya na unga wa ubinadamu wetu mgonjwa ili kuuponya kutoka ndani, kwa maji na damu ya sadaka yake na kwa moto wa Roho Mtakatifu. Na baada ya kifo na ufufuko wake, aliwatuma wanafunzi wake, kwa nguvu ya Roho yule yule, kuwa ishara na vyombo vya Ufalme wake duniani, Ufalme wa upendo, haki, na amani.”
Sifa muhimu ya mtindo huu wa maisha ni kutokuwa na ubinafsi
Papa alisema “Hili linatimizwa kupitia kuhubiri, lakini pia, na ningesema zaidi, kupitia mtindo wa maisha, njia ya kufikiri na kutenda ambayo ni ile ya Injili. Naam, sifa muhimu ya mtindo huu wa maisha ni kutokuwa na ubinafsi ambao mmeonesha siku chache zilizopita hapa Madrid. Asante! Asante!” Papa Leo aliwapongeza.
Upendo wa Mungu,unaosonga jua na nyota,na unaosonga mioyo ya wale waliokutana na Bwana
Hata hivyo Papa kuhusiana na hili aliongeza “Labda takwimu hazitaonesha hilo, lakini tunajua kwamba, katika siku hizi, shukrani pia kwenu, jiji hili limekua na liko karibu zaidi na Ufalme wa Mungu. Je, ni sifa yetu wenyewe? Hapana! Ni neema yake yote! Hii ndiyo siri: upendo wa Mungu, unaosonga jua na nyota, na unaosonga mioyo ya wale waliokutana na Bwana Yesu, ambaye alisema, “Ni heri kutoa kuliko kupokea” (Mdo 20:35).”
Bikira awajali kuwa chachu ya Ufalme siku zote na kila mahali
Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alitoa ushauri kwao: "Kaka, na dada hebu tuendelee katika njia hii! Kwa unyenyekevu na upole, bila kiburi chochote, bali kuweni imara katika imani na ukarimu katika huduma. Bikira Maria awajalie kuwa chachu ya Ufalme siku zote na kila mahali." Aliwapa mwaliko kuwa "Asante! Nasi tutawaona Roma!” Ndiyo ilikuwa hitimisho la Hotuba katika mji wa Madrid aliongia tangu tarehe 6 Juni, wakati wa kueleka Barcelona na vizisiwa vya Kanari na Tanarife.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
