2026.06.10 Kisiwa kikubwa cha Kanari. 2026.06.10 Kisiwa kikubwa cha Kanari. 

Papa anaelekea Las Palmas de Gran Canaria

Baada ya kuadhimisha misa tarehe 10 Juni 2026 katika Basilika ya Familia Takatifu,Papa Leo XIV alihitimisha hatua ya pili ya ziara yake ya Kitume huko Barcellona na sasa anaelekea katika Kisiwa kikubwa cha Bahari ya Atlantiki.Mkutano wa kwanza ni ule wa hali halisi ya makaribisho ya wahamiaji.

Vatican News

Baba Mtakatifu  Leo XIV aliondoka kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Josep Tarradellas Barcelona-El Prat kuelekea Las Palmas de Gran Canaria saa 2.45, Alhamisi asubuhi  tarehe 11 Juni 2026. Hii inakuwa kituo cha tatu cha Ziara yake ya kitume, mara baada ya kuadhimisha misa katika Basilika ya Familia Takatifu huko Barcelona usiku wa tarehe 10 Juni 2026 na kuzindua mnara wa Kanisa Kuu hilo.


Kwa ziara hii ya visiwa vikubwa katika Bahari ya Atlantiki, ambavyo pia zitajumuisha kituo kingine cha Santa Cruz de Tenerife, Papa Leo XIV atahitimisha Ziara yake ya nne ya kitume nchini Hispania iliyoanza tangu tarehe 6 Juni.

Kwaheri kutoka Barcelona

Alhamisi  takriban saa 7:30 asubuhi, Papa Leo XIV aliondoka nyumbani kwa Askofu Mkuu kuelekea uwanja wa ndege, ambapo alipokelewa na mamlaka mahalia. Kisha Papa Leo XIV alipanda ndege ya Iberia A320, ambayo, ndani ya saa tatu na nusu, itampeleka kwenye kituo cha anga cha Gran Canaria-Gando. Kwa mujibu wa utamaduni, mamlaka mahalia zitakuwepo kumkaribisha, ikifuatiwa na mkutano katika ukumbi wa watu mashuhuri.

Mabango ya kumkaribisha Papa Leo XIV katika Kisiwa kikubwa cha Kanari
Mabango ya kumkaribisha Papa Leo XIV katika Kisiwa kikubwa cha Kanari

Mkutano na Vituo vya mapokezi vya wahamiaji

Kituo cha kwanza katika ziara ya Papa katika Visiwa vya Kanari kitakuwa mkutano na vituo vya mapokezi vya wahamiaji katika bandari ya Arguineguín, kwenye pwani ya kusini ya kisiwa cha Kanari. Bandari hii bado inajulikana kama "Bandari ya Aibu" kwa sababu mnamo 2020, muda mfupi baada ya kuzuka kwa dharura ya Uviko19, takriban wahamiaji 3,000 walifika huko ndani ya Juma moja. Hata hivyo, kutokana na janga hilo, hakuna mtu aliyeruhusiwa kuingia bandarini: ni Caritas pekee iliyopanga shughuli zake kusaidia ajali ya meli iliyoharibika, ikileta chakula na vifaa vya matibabu. Mtu wa kujitolea kutoka shirika hilo atakuwa miongoni mwa wale watakaoshiriki ushuhuda wao na Papa.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here

11 Juni 2026, 08:55