Papa akutana na Waziri Mkuu wa Hispania,Sánchez
Vatican News
Kabla ya kufika katika Bunge la Manaibu kwa ajili ya mkutano na wabunge wa Bunge la Hispania asubuhi ya Jumatatu tarehe 8 Juni 2026 ikiwa ni siku yake ya tatu katika Ziara yake ya Kitume nchini Hispania, akiwa Madrid, Papa Leo XIV alikutana kwa muda mfupi na Waziri Mkuu, Pedro Sánchez Pérez-Castejón.
Ofisi ya Habari ya Kiti Kitakatifu iliripoti hili kwenye chaneli yake ya Telegram, ikibainisha kwamba Papa baadaye aliwasalimia baadhi ya washirika wake. Mkutano huo wa faragha ulidumu kwa takriban dakika 20.
Mara ya Mwisho alikuwa amekutana naye hivi karibuni mnamo tarehe 27 Mei 2025 mjini Vatican.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
