Papa Leo XIV akutana na kikundi cha waathirika wa nyanyaso huko Madrid
Na Salvatore Cernuzio – Madrid.
Jumatatu tarehe 8 Juni 2026 alasiri umefanyika mkutano kati ya Papa Leo XIV na kundi la waathiriwa wa nyanyaso na mapadre na Kanisa nchini Hispania iliodumu kwa karibu saa moja, na ambao ulijaa historia za maumivu na ambayo Papa mwenyewe ameyahisi. Mkutano huo, ulitangazwa na Ofisi ya Habari ya Vatican kwamba Mkutano huo “ulifanyika katika Ubalozi wa Vatican huko Madrid ambapo Papa anakaa wakati wa ziara yake.”
Ofisi ya Habari, kupitia Telegram, pia ilitangaza kwamba mazungumzo "yaliyodumu kwa takriban saa moja, “ulianza kwa kusikiliza matukio ya kibinafsi yenye uchungu ya kila mmoja wa wale waliokuwepo," ambao kila mmoja alimpatia Papa "mapendekezo ya kufanya kama majibu ya Kanisa kwa muktadha wa kesi kama hizo za kusikitisha kuwa na ufanisi zaidi." Taarifa ya Vatican inaendelea kuwa, "Papa aliwasikiliza kwa upendo na umakini, akawahakikishia ukaribu wake, na ule wa jumuiya nzima ya Kanisa, na kujitolea kwake kuhakikisha kwamba mapendekezo yaliyopokelewa yanatumika kama msingi wa juhudi zaidi na kwamba Kanisa linaweza kuwa mahali salama na penye afya njema ya kiroho, ambapo majeraha hupata faraja na uponyaji."
Msaada wa kusaidia
Waathiriwa walihisi kwamba Papa alikuwa amevumilia maumivu yao. Waliofika kwenye Ubalozi wa Vatican karibu saa 10:00 jioni masaa ya huko walikuwa ni Kundi hili la Proyecto Repara, yaani mpango wa ukarabati ambao ni wa Jimbo Kuu la Madrid ulioundwa ili kutoa msaada kamili kwa waathiriwa wa nyanyaso na kuzuia tabia kama hiyo ndani ya Kanisa na jamii. Kifupi chake kinawakilisha nguzo nne muhimu: Utambuzi, Kinga, Usaidizi, na Fidia. Watu waliopokelewa na Papa walipokelewa pamoja na wahudumu wa Kanisa waliojitolea kuwasaidia waathiriwa.
Mikutano iliyopita na Waathiriwa
Hii ni kwa mara ya kwanza Papa Leo XIV kukutana na waathiriwa wa unyanyasaji wakati wa ziara yake nje ya nchi, lakini si mkutano wake wa kwanza na wanaume na wanawake ambao wameathiriwa na unyanyasaji wa kijinsia ndani ya Kanisa Katoliki. Itakumbukwa mbamo Oktoba 2025, aliwapokea wajumbe sita wa bodi ya wakurugenzi ya ECA Global (Kumaliza Unyanyasaji wa Wakleri) mjini Vatican, ambalo ni Shirika la Kimataifa la haki za binadamu linalotetea usaidizi mkubwa na fidia kwa waathiriwa wa unyanyasaji. Mnamo Novemba 2025, alitumia takriban saa tatu na manusura 15 wa unyanyasaji wa kijinsia wa mapadre nchini Ubelgiji, wakisindikizwa na Tume ya Kipapa ya Ulinzi wa Watoto Wadogo.
Hatimaye, mnamo Februari 2026, Papa Leo XIV alikutana na David Ryan , mwathiriwa wa nyanyaso akiwa mtoto katika Chuo cha Blackrock huko Dublin pamoja na kaka yake Mark, ambaye alifariki mwaka 2023. "Papa Leo XIV alihisi uchungu wangu," Ryan alisema baada ya mkutano huo.
Tatizo la nyanyaso Nchini Hispania
Mazungumzo haya muhimu ya faragha, katika sehemu ya ziara yake ya kitume nchini Hispania, yamekuwa kivutio cha umakini kwa miaka mingi, kufuatia utafiti uliowasilishwa na Mtetezi wa Pueblo kwa Bunge la Manaibu, ambao ulikusanya ushuhuda 487 kutoka kwa waathiriwa wa nyanyaso katika Kanisa Katoliki nchini Hispania. Hii ilifuatiwa na uchunguzi wa waandishi wa habari na mipango iliyoiona Kanisa la Hispania likiwa mstari wa mbele. Na hivi karibuni, mwezi Machi 2026 lilikuwa makubaliano yaliyosainiwa na Baraza la Maaskofu, Baraza la Watawa, Mtetezi wa Pueblo wenyewe, na Wizara ya Urais ili kufafanua mpangilio na utendaji kazi wa mfumo wa utambuzi na fidia kwa waathiriwa.
Maneno ya Papa
Tayari akiwa safarini kutoka Roma hadi Madrid, Papa Leo, aliyechochewa na mwandishi wa habari, alielezea suala la nyanyasìo kama "jeraha ambalo bado liko wazi," akisisitiza kwamba katika sehemu nyingi ambazo amekuwa na kufanya kazi, amekuwa akipambana na unyanyasaji kila wakati. Ahadi hii itaendelea.
Na asubuhi ya Jumatatu tarehe 8 Juni 2026 akiwa katika makao ya Baraza la wakati wa hotuba yake Papa Leo XIV alisema kwamba: "safari yetu imeundwa na kukutana," na katika haya "hakutakuwa na upungufu wa wale wanaopitia nyakati za giza na kutuomba tuwe Wasamaria kwa ajili yao. Mojawapo ya kukutana kugumu zaidi," Papa Leo XIV alisema, "ni pamoja na wale ambao wamejeruhiwa na watu wale wale ambao walipaswa kuwatunza, wakiwemo mapadre. Kwa kukabiliwa na jeraha hili, Papa alihimiza, jumuiya ya Kanisa inaitwa kujibu kwa kusikiliza, ukweli, haki, fidia, na kujitolea zaidi kwa kuzuia na utamaduni wa utunzaji. Kila mtu aliyejeruhiwa lazima aweze kupata usikilizaji wa dhati, kukubalika, ulinzi, na njia halisi za uponyaji."
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.
