Tafuta

Wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika 28 Juni 2026 Papa Leo XIV aliwakumbuka na kuwaombea watu wa Mungu nchini Venezuela ambao hivi karibuni walikumbwa na tetemeko la ardhi Wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika 28 Juni 2026 Papa Leo XIV aliwakumbuka na kuwaombea watu wa Mungu nchini Venezuela ambao hivi karibuni walikumbwa na tetemeko la ardhi   (AFP or licensors)

Mshikamano wa Papa Leo XIV Kwa Watu wa Mungu Nchini Venezuela

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 28 Juni 2026, aliwakumbuka na kuwaombea watu wa Mungu nchini Venezuela ambao hivi karibuni walikumbwa na tetemeko la ardhi ambalo limepelekea watu milioni 7 kuathirika; kati yao watu 1, 450 wamefariki dunia, watu 3, 238 wamejeruhiwa vibaya na kwamba, watu 50, 000 hawajulikani mahali walipo! Maafa makubwa!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana, kwenye Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 28 Juni 2026, aliwakumbuka na kuwaombea watu wa Mungu nchini Venezuela ambao hivi karibuni walikumbwa na tetemeko la ardhi ambalo limepelekea watu milioni 7 kuathirika; kati yao watu 1, 450 wamefariki dunia, watu 3, 238 wamejeruhiwa vibaya na kwamba, watu 50, 000 hawajulikani mahali walipo! Hizi ni takwimu zilizotolewa Jumatatu tarehe 29 Juni 2026.

Tetemeko limesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao
Tetemeko limesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao   (AFP or licensors)

Baba Mtakatifu Leo XIV anawaombea wale wote waliofariki dunia, raha ya milele na mwanga wa milele uweze kuwaangazia na wapumzike kwa amani. Baba Mtakatifu anapenda kuonesha uwepo wake wa karibu kwa familia, majeruhi na wale wote walioguswa na kutikiswa na janga hili ambalo limeacha madhara makubwa kwa maisha ya watu wa Venezuela. Baba Mtakatifu Leo XIV anapenda kuwapongeza na kuwatia moyo vikosi vya ulinzi, usalama na uokoaji vinapoendelea kutekeleza dhamana na wajibu wake nyeti katika kipindi hiki cha mateso makali.

Papa Venezuela
29 Juni 2026, 15:28