Miaka 44 ya Upadre wa Papa Leo XIV mnamo Juni 19,1982
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV anafanya kumbukizi ya miaka 44 tangu alipopewa daraja Takatifu ya Upadre kunako tarehe 19 Juni 1982 katika Kikanisa cha Mtakatifu Monica, ambacho kinapakana na Ofisi Takatifu za Vatican mahali alipoishi akiwa mkuu wa Baraza la Curia Romana na ambacho kunako mwaka 2023, Baba Mtakatifu Francisko alimkabidhi kuwa shamasi wakati wa kuundwa kwake kuwa Kardinali katika Baraza la Makardinali.
Daraja la upadre lilitolewa na Askofu Mkuu Jeaan Jadot wa Ubelgiti, ambaye wakati ule alikuwa ni Rais wa Sekretarieti ya Kipapa kwa ajili ya Wasio Wakristo. Wakati wa Upadrisho wake, Padre Robert Francis Prevost alikuwa na umri wa miaka 27 na tayari alikuwa amesomea Sheria ya Kanisa katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Mtakatifu Thomas Aquinas. Alikuwa amejiunga na Shirika la Mtakatifu Agostino baada ya miaka mitano na kufunga nadhiri za daima mwaka 1981. Mwaka 1985, alitumwa kama mmisionari nchini Peru, akihudumu katika utume huko Chulucanas, Piura.
Padre Robert Francis Prevost alichaguliwa kuwa Mkuu wa Shirika la kiagostinian kunako mwaka 2001, ambapo aliongoza shirika hilo kwa mihula miwili hadi mwaka 2013, wakati wa kuchaguliwa kwa Baba Mtakatifu Francisko. Kuna trehe 3 Novemba 2014 aliteuliwa na Baba Mtakatifu kuwa msimamizi wa Jimbo katoliki la Chiclayo na kuwa n kiti cha Sufar, na kupewa wakfu wa kiaskofu kunako tarehe 12 Desemba 2014 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Maria kwa kuwekewa mikono yake na Askofu Mkuu James Green nchini Peru, na baadaye 2015, akateuliwa rasmi kuwa Askofu wa Jimbo hilo hilo tarehe 26 Septemba 2015.
Mnamo tarehe 13 Julai 2019 Askofu Prevost aliteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Kipapa la Mapadre. Mnamo tarehe 15 Aprili 2020 akateuliwa kuwa msimamizi wa kitume wa Callayo. Mnamo tarehe 21 Novemba 2020 akawa sehemu ya Baraza la Maaskofu. Mnamo tarehe 30 Januari 2023, Papa Francisko alimteua Askofu Prevost kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu, akimpa cheo cha Askofu Mkuu Mstaafu wa Chiclayo. Askofu Prevost alikuwa ameonesha upendeleo wa kubaki Peru lakini alikubali utume huo. Aliendelea kuwa hai katika Baraza la Maaskofu la Amerika Kusini na Visiwa vya Carribiean, akihudhuria mikutano ya Baraza hilo huko Aguadilla, Puerto Rico, mnamo Mei 2023.
Mnamo tarehe 30 Septemba 2023, Papa Francisko alimnyanyua Askofu Mkuu Prevost hadi wadhifa wa Kardinali, akimpatia ushemasi wa Kikanisa cha Mtakatifu Monica. Kama mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la maaskofu , alichukua jukumu muhimu katika kutathmini na kupendekeza wagombea wa maaskofu duniani kote, na kuongeza mwonekano wake ndani ya Kanisa, ambapo katika mkutano mkuu wa mnamo Oktoba 2023, Papa Francisko alimteua kuwa mjumbe katika mabaraza mengine saba na pia akamjumuisha katika Tume ya Kipapa ya mji wa Vatican.
Mnamo tarehe 5 Februari 2025, Papa Francisko alimpandisha cheo Prevost hadi kuwa Kardinali-Askofu, akimpatia Jimbo la Albano. Mnamo tarehe 11 Februari, iliyofuata, Mkuu wa Shirika la Kijeshi Kardinali John Timothy Dunlap alimteua katika hadhi na cheo cha Msalaba Mkuu wa Heshima na Ibada ya Shirika la Malta.
Na mnamo tarehe 21 Aprili 2025, ilikuwa ni karibu kuacha wadhifa huo wa Mkuu wa Baraza la Kipapa la Maaskofu kufuatia kifo cha Papa Francisko, kwani katika mkutano Mkuu ulioanza alasiri tarehe 7 Mei 2025, siku iliyofuata, katika kura ya nne, Kardinali Prevost alichaguliwa kuwa Papa wa 267 na akachukua jina la Leo XIV, kwa heshima ya Papa Leo XIII. Kwa hivyo akawa Papa wa pili kutoka bara la Amerika, baada ya mtangulizi wake Papa Francisko, na pia wa kwanza katika historia kutoka Marekani na wa Shirika la Mtakatifu Agostino.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
