Barcelona,Papa akutana na wawakilishi wa MED26:changamoto nyingi katika Mediterrania
Vatican News
Papa alikuwa na mikutano kadhaa alasiri ya Jumanne tarehe 9 Juni 2026 hasa mara baada ya kufika katika Ukumbi wa Askofu Mkuu wa Barcelona. Kwa mujibu wa Ofisi ya Habari ya Vatican iliripoti hilo kupitia Telegram. Ulifanyika Mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Katalonya, Salvador Illa i Roca, ambao ulidumu kwa takriban dakika 15. Mwishoni, Papa Leo XIV pia aliwasalimu baadhi ya washirika wake.
Kuelekea bandari ambapo habari njema inasubiriwa
Takriban washiriki 200 wanahudhuria Mkutano wa Mediterania wa MED26, ambao kwa sasa unafanyika huko Barcelona, sambamba na Ziara ya Papa ya Hispania, na ambao Papa Leo XIV alikutana nao. Aliwahutubia, huku akiwatia moyo kusafiri, kijiografia na kiroho, hadi bandari hizo ambapo wanaume na wanawake wanasubiri habari njema. Kisha alitaja changamoto nyingi zinazokabili Mediterania, hasa Mashariki ya Kati, na kutoa shukrani na kutia moyo kwa kazi inayolenga kuifanya dunia kuwa mahali pazuri, katika kujenga mazungumzo, na kuona kwamba "kuna utajiri katika utofauti, na katika utofauti tunaweza kuungana." Mwishoni mwa mkutano, walisali pamoja na sala ya Baba Yetu.
Mkutano wa MED26 unaoongozwa na mada kwa ajili ya "ujenzi wa amani" katika Bahari ya Mediterania. Mnamo Machi 12, Papa Leo XIV ilikuwa amepokea ujumbe kutoka Ofisi ya Uratibu wa Kanisa la Mediterania, inayoongozwa na Kardinali Jean-Marc Aveline, huko Vatican akiwatia moyo waliohudhuria kuendelea na mipango yao ya kukuza elimu ya amani na utamaduni wa kukutana.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
