Tafuta

2026.05.11 Washiriki wa Kongamano lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Taasisi ya Kifalme ya Mafunzo  ya Dini Mbalimbali,Jordan. 2026.05.11 Washiriki wa Kongamano lililoandaliwa na Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini na Taasisi ya Kifalme ya Mafunzo ya Dini Mbalimbali,Jordan.  (@VATICAN MEDIA)

Papa Leo XIV:Wakristo na Waislamu lazima wafanye kazi pamoja ili kufufua ubinadamu!

Papa Leo XIV akikutana na washiriki wa Kongamano la VIII la dini mbalimbali mjini Vatican alisema "Ingawa ni kweli tumeunganishwa zaidi kuliko hapo awali,mtiririko wa mara kwa mara wa picha na video za shida za wengine unaweza kudhoofisha mioyo yetu badala ya kuzichochea."Wakristo na Waislamu wanaitwa kutumia utajiri wa tamaduni zao ili kushiriki dhamira ya pamoja kufufua ubinadamu ambapo na kutoa sauti kwa wale wanaoteseka na kubadilisha kutojali kuwa mshikamano."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu  Leo XIV alikutana mjini Vatican, Jumatatu tarehe 11 Mei 2026  na wajumbe wa  Baraza la Kipapa la Mazungumzo ya Kidini na wa Taasisi ya Kifalme ya Jordan ya Mafunzo  ya Dini Mbalimbali. Taasisi ya Kifalme, ilianzishwa chini ya ufadhili wa Mkuu wa Jordan,  Hasan bin Talal, wakiwa katika fursa ya Kongamano la VIII kuhusu mada ya: "Huruma ya Kibinadamu na Huruma katika Nyakati za Kisasa," lililoandaliwa na Taasisi zote mbili.

Papa na washiriki wa Kongamano la Kidini
Papa na washiriki wa Kongamano la Kidini   (@VATICAN MEDIA)

“Al-Ra'uf inatukumbusha kuwa huruma daima huanzia kwa Mungu mwenyewe"

Katika hotuba yake, kwa lugha ya kiingereza Baba Mtakatifu Leo XIV alibainisha kuwa huruma na upole ni mitazamo muhimu ya Ukristo na Uislamu. Katika utamaduni wa Kiislamu, Papa alifafanua, kwamba huruma (ra'fa) ni zawadi iliyotolewa na Mungu katika mioyo ya waamini, huku kuingizwa kwa al-Ra'uf ('Mwenye huruma daima') miongoni mwa majina tisini na tisa ya kimungu kunatukumbushwa kwamba "huruma daima huanzia kwa Mungu mwenyewe."

Kwa Wakristo huruma inagusika kupitia nafasi ya Yesu

Katika utamaduni wa Kikristo, kwa upande mwingine, Papa Leo XIV alisema, huruma hii ya kimungu huonekana na kugusika katika nafsi ya Yesu. Kwa kuchukua mwili wa mwanadamu, Mungu "hupita zaidi ya kuona na kusikia" mateso ya mwanadamu, na huyapitia Yeye Mwenyewe, na kuwa "mfano hai wa huruma.” Kwa hivyo, huruma na upole, sio kitu cha ziada au cha hiari kwa Wakristo na Waislamu. Hakika, vina matokeo ya kijamii kwa waamini katika dini zote mbili.

Washiriki wa Kongamano la Kidini
Washiriki wa Kongamano la Kidini   (@VATICAN MEDIA)

Athari za kiteknolojia leo hii

Kwa mtazamo wa Kikristo, Papa Leo XIV kadhalia alifafanua kwamba “upendo kwa maskini na kiukweli kushiriki mateso yao ni muhimu sana. Katika suala hilo  Baba Mtakatifu alitoa shukrani zake kwa juhudi za ukarimu za Ufalme wa Jordan za kuwakaribisha wakimbizi. Katika hotuba yake  Baba Mtakatifu vile vile  alitafakari  juu ya athari za teknolojia kwenye huruma na upole leo hii. “Ingawa ni kweli kwamba tumeunganishwa zaidi kuliko hapo awali, mtiririko wa mara kwa mara wa picha na video za shida za wengine unaweza kudhoofisha mioyo yetu badala ya kuzichochea, alisisitiza."

Kutojali mateso ya wengine:tubadili kutojali kuwa mshikamano

Baba Mtakatifu Leo XIV akinukuu mahubiri ya Papa Francisko, alionya kwamba: "tumezoea mateso ya wengine kwa kuamini kwamba hayatuathiri, hayatugus na kwamba  si kazi zetu." Katika muktadha huo, alisema, “Wakristo na Waislamu badala yake wanaitwa kutumia utajiri wa tamaduni zao ili kushiriki katika dhamira ya pamoja ile ya kufufua ubinadamu pale ambapo umekufa,  kutoa sauti kwa wale wanaoteseka na kubadilisha kutojali kuwa mshikamano."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

11 Mei 2026, 15:27