Tafuta

Papa Leo XIV:Mwaliko wa Yesu hauna udanganyifu

"Bwana anatuamuru kupendana kama alivyotupenda sisi kwa sababu ni upendo wa Yesu unaofanya upendo ukue ndani yetu.Kristo mwenyewe ndiye kigezo,kiwango cha upendo wa kweli:upendo ambao ni mwaminifu milele,safi na usio na masharti.Upendo usiojua "lakini" wala"labda,"upendo unaotoa bila kutafuta umiliki,upendo unaotoa maisha bila kuchukua chochote kama malipo."Ni katika tafakari ya Injili aliyofanya Papa Leo XIV kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu Dominika Mei 10.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza tafakari yake, kabla ya Sala ya Malkia wa Mbingu akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume Dominika tarehe 10 Mei 2026. Akiwageukia waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, alianza kwa salamu na kuwatakia Dominika njema. Kisha Papa alisema: “Leo hii katika Injili tuliyosikia ni baadhi ya maneno ambayo Yesu aliwageukia mitume wake wakati Karamu yake Kuu. Wakati anaweka mkate na divai kuwa ishara hai ya upendo wake, Kristo anasema: “ikiwa mnanipenda, zishikeni amri zangu(Yh 14,15).

PAPA LEO XIV WAKATI WA SALA YA MALKIA WA MBINGU
PAPA LEO XIV WAKATI WA SALA YA MALKIA WA MBINGU   (@Vatican Media)

Tunazishika Amri kweli kwa mapenzi ya Mungu

Uthibitisho huu unatuondolea mkanganyiko,  yaani kutoka katika wazo la kuwa sisi tunapendwa ikiwa tunazishika amri zake: haki yetu ingekuwa kuwekewa hali fulani ya upendo wa Mungu. Papa alisema "Kinyume chake, upendo  wa Mungu ni hali kwa ajili ya haki yetu. Tunazishika amri zake kweli kwa mujibu wa mapenzi ya Mungu, ikiwa tunatambua upendo wake kwa ajili yetu, na hivyo kama Kristo anavyouonesha ulimwenguni." Maneno ya Yesu kwa hiyo Papa alisisitiza "ni mwaliko kwa uhusiano, sio udanganyifu wowote  au kusitishwa kwa mashaka." Na ndiyo maana Bwana anatuamuru tupendane sisi kwa sisi kama Yeye alivyotupenda (Yh 13,34): ni upendo wa Yesu unaofanya kuzaliwa ndani mwetu upendo. Kristo mwenyewe ni sababu, na ni kanuni ya Upendo kweli: Ule mwaminifu wa kweli, safi na usio na masharti. Ule ambao haujuhi kusema,“lakini” wala  “labda", ule ambao unajitoa bila kutaka kumiliki, ule ambao unatoa maisha bila kuchukua lolote la kubadilishana nalo.

MAKUNDI YA MAHUJAJI KATIKA UWANJA WA MTAKATIFU PETRO
MAKUNDI YA MAHUJAJI KATIKA UWANJA WA MTAKATIFU PETRO   (@Vatican Media)

Amri za Bwana ni kanuni ya maisha

Papa Leo XIV alisisitiza tena  kwamba kwa kuwa Mungu anatupenda akiwa wa kwanza, hata sisi lazima tupendane; na tunapompenda Mungu kweli, tunapendana kweli kati yetu. Inajitokeza kama kwa kila maisha: ni yule aliyepokea tu anaweza kuishi, na hivyo aliyependwa anaweza kupenda tu. Papa Leo XIV alisisitiza kwamba "Amri za Bwana,  kwa hiyo ni kanuni ya maisha ambayo yanatusafisha dhidi ya mapendo ya uongo; ni mtindo wa kiroho, ambao ni njia ya wokovu."  Kwa kuwa anatupenda, "Bwana hatuachi peke  yetu katika majaribu ya maisha: anatuahidi Msaidizi, yaani Wakili Mtetezi, Roho wa kweli (Yh 14,17)." Papa alibanisha kwamba " Ni zawadi ambayo “Ulimwengu  hauwezi kuipokea,"  kwa sababu unaendelea katika ubaya ambao unakandamiza masikini, unabagua mdhaifu, unaua hasiye na hatia." Kinyume chake Papa Leo XIV aliongeza: “anayejibu upendo ambao Yesu anao kwa wote, anapata Roho Mtakatifu katika mshikamano ambao haukosi kamwe: “Nyinyi mnajua, anasema Yesu, kwa sababu Yeye anakaa nanyi na atabaki nanyi.”

Kwa kutoa upendo kwetu, Yesu anashirikishana nasi utambulisho wake

Baba Mtakatifu Leo XIV alisema kwamba "Daima na kila mahali tunaweza kwa hiyo kushuhudia Mungu ambaye ni upendo: neno hili halina maana ya wazo la kiakili na kibinadamu, lakini ni ukweli wa maisha ya Kimungu, ambaye kila kitu kimeundwa kutoka katika utupu na Wokovu kutoka katika kifo." kwa njia hiyo "kwa kutoa upendo kwetu wa kweli na milele, Yesu anashirikishana nasi utambulisho wake wa Mwanao mpendwa: “Mimi ni katika Baba yangu na ninyi ndani mwangu na ninyi ndani mwenu(Yh 14,20)." Uunganishwaji huu wa muungano wa maisha unakanusha mshtaka, yaani mpinzani wa mpanishi, Roho tofauti na mtetezi wetu."

MWONEKANO WA WAAMINI KATIKA UWANJA WA MTAJATIFU PETRO
MWONEKANO WA WAAMINI KATIKA UWANJA WA MTAJATIFU PETRO   (@Vatican Media)

Kiukweli  Papa Leo XIV alisema, "wakati Roho Mtakatifu ni nguvu ya maisha, mshtakiwa ni “baba mdanganyifu”(Yh 8,44,) anayetaka kukinzana na mwanadamu kwa Mungu na watu kati yao: ni kinyume hasa na kile anachofanya Yesu, kwa kutuokoa na ubaya na kutuunganisha kama watu,  kaka na dada katika Kanisa." Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alisema "kwa kujazwa na shukrani ya zawadi hiii, tumkabidhi maombezi ya Bikira Maria Mama wa Upendo wa kimungu."

TAFAKARI YA PAPA LEO XIV 10 MEI 2026

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

10 Mei 2026, 12:14