Tafuta

Msako wa magaidi nchini Mali Msako wa magaidi nchini Mali  (AFP or licensors)

Wasiwasi wa Papa Leo kuhusu mashambulizi ya kigaidi katika maeneo ya Sahel

Wasiwasi kuhusu habari za ongezeko la vurugu katika eneo la Sahel,hasa Chad na Mali,zilizokumbwa na mashambulizi ya kigaidi hivi karibuni,siku ya Urafiki kati ya Kanisa la Kikopti na Kikatolki,salamu kwa mahujaji na visiwa vya Canari,ni kiini cha mawazo ya Papa Leo XIV,mara baada ya Sala ya Malkia wa Mbingu,Dominika Mei 10 kwa mahujaji na waamini waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

“Nawahakikishia maombi yangu kwa ajili ya waathiriwa na ukaribu wangu na wote wanaoteseka. Ninatumaini aina zote za vurugu zitaisha na kuhimiza kila juhudi kwa ajili ya amani na maendeleo katika nchi hiyo pendwa." Haya ni maneno ya  wasi wasi  na kutia moyo ya Baba Mtakatifu  Leo XIV, aliounesha mara baada ya sala ya Malkia wa Mbungu, akiwa katika dirisha la Jumba la Kitume, kwa kuwageukia waamini na mahujaji waliotoka pande za dunia wakiwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Dominika tarehe 10 Mei 2026. 

Wasi wasi wa Papa Leo XIV kwa Eneo la Sahel huko Chad na Mali
Wasi wasi wa Papa Leo XIV kwa Eneo la Sahel huko Chad na Mali   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akianza alisema:  “Kaka na dada wapendwa, nimepokea kwa wasiwasi kuhusu habari za ongezeko la vurugu katika eneo la Sahel, hasa Chad na Mali, zilizokumbwa na mashambulizi ya kigaidi ya hivi karibuni. Papa Leo XIV aliendelea: “Nawahakikishia maombi yangu kwa ajili ya waathiriwa na ukaribu wangu na wote wanaoteseka.Ninatumaini aina zote za vurugu zitaisha na kuhimiza kila juhudi kwa ajili ya amani na maendeleo katika nchi hiyo pendwa.”

Siku ya Kirafiki kati ya Kanisa la Kikopti na Kikatoliki

Kila mwaka, ifikapo Mei 10 huadhimishwa "Siku ya Urafiki wa Wakopti na Wakatoliki." Baba Mtakatifu Leo XIV aliongeza: “Ninatoa salamu za kidugu kwa Patriaki Tawadros II na kuwahakikishia Kanisalote pendwa la Wakopti maombi yangu, na kwa matumaini kwamba safari yetu ya urafiki itatuongoza kwenye umoja kamili katika Kristo, aliyetuita ‘marafiki.’”(Yh 15,15).

Patriaki Tawadros II
Patriaki Tawadros II

Kisha Papa alitoa salamu zake kwa wote kuanzia na warumi, na mahujaji kutoka Nchi mbalimbali. Kwa nama ya pekee aliwasalimu Kikundi cha “Walinzi wa Heshima cha Moyo Mtakatifu wa Yesu,” kutoka sehemu mbali mbali za Italia. Watu wa “kujitolea kwa ajili ya Uinjilishaji,” kinachohusiana na Familia ya Radio Maria; Chama cha Kujitolea cha “Komen Italia”, ambacho kinajikita na kuhamasisha kuzuia sarani za matiti.

Watu wa kujitolea wa Radio Maria
Watu wa kujitolea wa Radio Maria   (@Vatican Media)

Papa kwa lugha ya kispanyola alisema:  “Ninapanda  kutoa shukrani zangu kwa ukaribisho wa joto unaowatambulisha watu wa Visiwa vya Canari, na kuruhusu meli ya kitalii ya Hondius kutia nanga na wagonjwa wa hantavirus. Ninafurahi kuweza kukutana nanyi mwezi ujao wakati wa ziara yangu kwenye visiwa hivyo.”

Umati katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Umati katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Siku ya Mama

Papa Leo XIV katika muktadha wa siku ya Mama  alisema:  “Wazo pia maalum linawageukia Mama wote. Kwa maombezi ya Maria, Mama wa Yesu na wetu, tuombe kwa upendo na shkrani kwa kila mama, hasa kwa wale wanaoishi katika hali ngumu zaidi. Asante. Mungu awabariki!

Heri na siku  ya Mama
Heri na siku ya Mama

Hatimaye Papa aliwatakia Dominika njema na kuwaaga.

PAPA LEO XIV KWA CHAD NA MALI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here.

 

10 Mei 2026, 12:14