Picha za dakika moja za siku ya tano ya Papa barani Afrika
Vatican News
Papa Leo XIV aliondoka katika mji mkuu wa Yaoundé asubuhi ya ijumaa Aprili 17 ili kuruka hadi kituo cha mwisho kati ya vituo vitatu katika ziara yake ya kitume kwenda Cameroon
Douala
Alitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa jiji la Doual lenye watu wengi zaidi nchini humo saa 3:24 asubuhi kwa saa za huko. Aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Japoma, iliyohudhuriwa na waamini zaidi ya 120,000 kwa furaha kubwa na kisha akaendelea hadi Hospitali Katoliki ya Mtakatifu Paulo. Baada ya ziara hiyo ya faragha, alielekea uwanja wa ndege tena wa Douala na kurudi Yaoundé. Mara tu aliporudi katika mji mkuu, alikutana na jumuiya ya wasomi katika Chuo Kikuu Katoliki cha Afrika ya Kati saa 11:30 jioni kwa saa za huko.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
