Tafuta

2026.04.14 Viaggio Apostolico in Algeria - Santa Messa nella Basilica di Santâ  Agostino

Papa XIV:Katika ulinzi wa watoto,Kanisa halipaswi kuogopa kashfa bali kutafuta ukweli

Katika ujumbe wa Aprili 10,uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Parolin,katika Mkutano wa pili wa Kitaifa wa Wawakilishi Mahalia kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto na Watu Wazima Walio Katika Mazingira Hatarishi,Papa alibainisha kwamba"heshima kwa watoto haiwezi kupunguzwa hadi seti ya sheria zinazopaswa kutumika kwa sababu inaashiria aina ya hekima kwa jinsi mamlaka inavyotumika."Alihimiza kuacha"kuhojiwa na maumivu ya wale walioteseka."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV ametoa mwaliko katika ujumbe wake uliondikwa tarehe 10 Aprili 2026,  na kuchapishwa tarehe 16 Aprili 2026, uliosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican Kardinali Pietro Parolin, wakati wa Mkutano wa pili wa Kitaifa wa Wawakilishi Mahalia nchini Italia  kwa ajili ya Ulinzi wa Watoto na Watu Wazima walio katika Mazingira Hatarishi, ulianza mjini Roma kuanzia Aprili 16 hadi 18 Aprili 2026. Papa alibainisha kwamba “Unapokabiliwa na maumivu, uliza maswali badala ya kujitetea. Kiri maumivu badala ya kuyapunguza. Usijifungie kwa kuogopa kashfa, bali kubali njia zinazodai ukweli, haki na uponyaji."

Pasipo na heshima mahusiano ni duni

Papa alimwelekeza Kardinali Matteo Zuppi, Rais wa Baraza la  Maaskofu Italia (CEI), akizingatia mada ya mkutano huo, "Kuzalisha Mahusiano Halisi." Mada hiyo inaongoza kazi "muhimu" ya jumuiya za Kikristo, parokia, vyama, vya Kanisa na harakati katika kutambua utu wa kila mtu na kulinda uhuru wake. Hata hivyo, pale ambapo heshima haipo, mahusiano huwa duni, yamepotoshwa, na yanaweza kusababisha madhara makubwa. Katika maono ya Kikristo, Papa aliandika, heshima haizuiliwi na usahihi tu, bali huinuka hadi "aina ya hisani inayodai" ambayo inalinda wengine "bila kuwatumia," inawasindikiza "bila kuwatawala," na kuwahudumia "bila kuwadhalilisha."

Malezi hayawezi kueleweka kama seti tu ya sheria zinazopaswa kutumika au taratibu zinazopaswa kuzingatiwa badala yake  yanahitaji hekima inayoathiri mtindo wa jamii, jinsi mamlaka inavyotumika, mafunzo ya waelimishaji, uangalifu wa mazingira, na uwazi wa tabia. Kwa hiyo Papa Leo XIV, alibainisha kwamba uwepo wa watoto na watu walio katika mazingira magumu ndani ya Kanisa, unapinga dhamiri ya Kanisa, ukipima uwezo wake wa kuonesha "utunzaji halisi," ambao unaoneshwa kupitia ulinzi, kusikiliza, kuzuia, na kutomwacha mtu peke yake." Kwa sababu hiyo, kazi ya wale wanaohamasisha mafunzo, utambuzi, uratibu, na utendaji bora inawakilisha mchango muhimu katika maendeleo ya jamii zinazokaribisha na zenye ufahamu zaidi.

Jumuiya ya Kikristo inapata uongofu wa kiinjili ikiwa haijitetei

Kisha Papa alisisitiza umakini "maalum" unaopaswa kutolewa kwa wale waliotendewa vibaya, ambao majeraha yao yanahitaji ukaribu wa dhati, usikilizaji wa unyenyekevu, na uvumilivu katika kutafuta "kile kilicho cha haki na kinachowezekana kurekebisha." Jumuiya ya Kikristo hupata uongofu wa kiinjili wakati haijitetei kutokana na maumivu ya wale walioteseka, lakini hujiruhusu kuhojiwa; wakati haipunguzi uovu, lakini inakubali; wakati haijifungi kwa hofu ya kashfa, lakini inakubali njia zinazodai za ukweli, haki, na uponyaji.

"Na nitakutunza"

Kwa hivyo mkutano unaofanyika Roma unazidi kiwango cha utendaji," Papa alihitimisha, akilitaka Kanisa kukua katika"utamaduni wa kuzuia," ambao kwanza kabisa ni "utamaduni wa ulinzi wa kiinjili." Hii itaendelezwa na kipindi cha "And I Will Care for You," “ Na Nitakutunza”, ambacho kitaoneshwa kwa mara ya kwanza wakati wa mkutano: safari ya kisanii na kimuziki inayoleta uhai wa janga la nyanyaso katika mazingira ya kikanisa, na kutoa sauti kwa maumivu ya waathiriwa.

 

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

16 Aprili 2026, 18:00