Tafuta

Papa Leo XIV:Bara la Afrika ligawe utajiri sawa na kushinda ufisadi!

Papa alieleza Ziara yake ya Kitume katika Katekesi ya Aprili 29,katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican:Algeria ni daraja la enzi ya matunda ya Mababa wa Kanisa,ulimwengu wa Kiislamu na bara la Afrika.Cameroon kuimarisha wito wa kufanya kazi pamoja,ya upatanisho na amani.Angola ilipitia kipindi cha misukosuko,kilichojaa damu ya vita vya ndani.Siwezi kusahau kilichotokea gerezani Bata,Guinea ya Ikweta:wafungwa waliimba wimbo wa shukrani kwa Mungu wakiomba kwa ajili ya dhambi zao na kuwa huru.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliongoza Katekesi yake  kwa kutaka kuelezea juu ya Ziara yake ya Kitume ya hivi karibuni akishirikisha waamini na mahujaji wapatao 25,000 waliohudhuria katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, mjini Vatican kuhusu Mikutano yake  iliyofanya huko Algeria, Cameroon, Angola, na Guinea ya Ikweta iliyoanza tangu tarehe 13 hadi 23 Aprili. Ni simuliizi ya  hisia na mawazo yake. Katika bara la Afrika, Papa alisema  ni muhimu kugawa utajiri kwa usawa, kushinda ufisadi, na kukabiliana na ukoloni mamboleo kwa ushirikiano wa kimataifa wenye mtazamo wa mbali, Papa aliweza pia kuonesha jinsi ambavyo hataweza  kuwasahau wafungwa wa gereza la Bata ambao, wakati wa mvua, waliomba maombi kwa ajili ya dhambi zao na uhuru wao: "Sijawahi kuona kitu kama hicho.”

Papa nchini Algeria
Papa nchini Algeria   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo Baba Mtakatifu Leo XIV mara baada ya somo la Injili alianza kusema: “Tangu mwanzo wa upapa wangu, nilikuwa nikifikiria kuhusu safari ya kwenda Afrika. Ninamshukuru Bwana ambaye ameniruhusu kufanya hivyo, kama Mchungaji, kukutana na kuwatia moyo watu wa Mungu; na pia kuishi kama ujumbe wa amani katika wakati wa kihistoria uliojaa vita na ukiukwaji mkubwa na wa mara kwa mara wa sheria za kimataifa.” Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa “Na ninatoa "shukrani" zangu za dhati kwa Maaskofu na mamlaka za kiraia walionikaribisha mimi na kwa wote walioshirikiana katika maandalizi hayo.” Mungu mpaji, Papa alisema “alitamani kwamba kituo cha kwanza kiwe nchi ambayo maeneo ya Mtakatifu Agostino yapo, yaani Algeria.

Kwa hivyo, nilijikuta, kwa upande mmoja, kuanzia mizizi ya utambulisho wangu wa kiroho na kwa upande mwingine, kuvuka na kuimarisha madaraja ambayo ni muhimu sana kwa ulimwengu na Kanisa leo hii yaani: daraja la enzi yenye matunda ya Mababa wa Kanisa; daraja la ulimwengu wa Kiislamu; na daraja la bara la Afrika. Nchini Algeria, nilikaribishwa kwa heshima na urafiki, na tuliweza kujionea na kuonesha ulimwengu kwamba inawezekana kuishi pamoja kama kaka na dada, hata wa dini tofauti, tunapotambuana kama watoto wa Baba mmoja mwenye huruma,”Papa alisisitiza. Zaidi ya hayo, Papa aliongeza “ilikuwa fursa nzuri ya kujifunza mafundisho ya Mtakatifu Agostino: kwa uzoefu wake wa maisha, maandishi yake, na hali yake ya kiroho, yeye ni mtaalamu katika utafutaji wa Mungu na ukweli. Ushuhuda huu ni muhimu zaidi leo hii  kuliko wakati mwingine wowote kwa Wakristo na kwa kila mtu.”

Nchi Tatu zilizofuata

Katika nchi tatu zilizofuata nilizotembelea, Papa Leo XIV aliendelea kudadavua kuwa “idadi ya watu ni Wakristo wengi, na kwa hivyo nilijikita katika mazingira ya kusherehekea imani na makaribisho ya joto, yaliyochochewa pia na sifa za kawaida za Kiafrika. Mimi pia, kama watangulizi wangu, nilipitia jambo ambalo Yesu alipitia kwa umati wa Galilaya: Aliwaona wakiwa na kiu na njaa ya haki, na akawatangazia: "Heri walio maskini, heri wapole, heri wapatanishi..." na, akitambua imani yao, alisema: "Ninyi ni chumvi ya dunia na nuru ya ulimwengu" (Mt. 5:1-16).

Papa Nchini Cameroon
Papa Nchini Cameroon   (@Vatican Media)

Cameroon

Baba Mtakatifu Leo XIV katika kuendelea na simulizi ya ziara yake ya Kitume alisema, “ Ziara yangu Cameroon  iliniwezesha kuimarisha wito wa kufanya kazi pamoja kwa ajili ya upatanisho na amani, kwa sababu nchi hiyo pia, kwa bahati mbaya, ina mvutano na vurugu. Nimefurahi kwenda Bamenda, katika eneo linalozungumza Kiingereza, ambapo niliwatia moyo kufanya kazi pamoja kwa ajili ya amani.”Cameroon inaitwa "uundaji wa Afrika ndogo," ikimaanisha aina na utajiri wa asili na rasilimali zake, lakini pia tunaweza kuelewa usemi huu kumaanisha kwamba mahitaji makubwa ya bara zima yanapatikana Cameroon: yale ya usambazaji sawa wa utajiri; ya kutoa nafasi kwa vijana, kushinda ufisadi ulioenea; ya kuhamasisha maendeleo fungamani na endelevu, kukabiliana na aina mbalimbali za ukoloni mamboleo kwa ushirikiano wa kimataifa wenye mtazamo wa mbali.” Baba Mtakatifu kwa njia hiyo alishukuru akisema “ Ninashukuru Kanisa nchini Cameroon na watu wote wa Cameroon, walionikaribisha kwa upendo mkubwa, na ninaomba kwamba roho ya umoja iliyooneshwa wakati wa ziara yangu ihifadhiwe hai na kuongoza maamuzi na vitendo vya baadaye.”

Papa Nchini Angola
Papa Nchini Angola   (@Vatican Media)

Hatua ya Tatu Angola

Kituo cha tatu katika Ziara Papa Leo XIV aliendelea, “kilikuwa Angola, nchi kubwa kusini mwa ikweta, yenye tamaduni ya Kikristo ya karne nyingi iliyohusishwa na ukoloni wa Ureno. Kama nchi nyingi za Afrika, baada ya kupata uhuru, Angola ilipitia kipindi cha misukosuko, kilichojaa damu kutokana na vita vya ndani vya muda mrefu. Katika historia hii, Mungu aliongoza na kulitakasa Kanisa, akiligeuza zaidi kuwa huduma ya Injili, maendeleo ya kibinadamu, upatanisho, na amani. Kanisa huru kwa watu huru! Katika Madhabahu ya Maria ijulikanayo "Mamã Muxima,  maana yake: "Mama wa Moyo", nilihisi moyo wa watu wa Angola ukidunda.”

Madhabahu ya Maria Mama Muxima
Madhabahu ya Maria Mama Muxima   (@Vatican Media)

Na katika mikutano mbalimbali, kwa furaha nimewaona wanaume na wanawake wengi wa watawa wa kila kizazi, unabii wa Ufalme wa Mbinguni miongoni mwa watu wao; nimewaona makatekista wanaojitolea kikamilifu kwa ajili ya mema ya jamii zao; Nimewaona nyuso za wazee, zilizoundwa kwa kazi ngumu na mateso na wazi kwa furaha ya Injili; nimewaona wanawake na wanaume wakicheza kwa mdundo wa nyimbo za sifa kwa Bwana aliyefufuka, msingi wa tumaini linalopinga tamaa zinazosababishwa na itikadi na ahadi tupu za wenye nguvu.” Papa Leo XIV alisisitiza kwamba “Tumaini hili linahitaji kujitolea kwa dhati, na Kanisa lina jukumu, kupitia ushuhuda na utangazaji wa ujasiri wa Neno la Mungu, kutambua haki za wote na kukuza heshima yao yenye ufanisi. Kwa mamlaka za kiraia za Angola, lakini pia kwa zile za nchi zingine, niliweza kuwahakikishia kuhusu nia ya Kanisa Katoliki ya kuendelea kutoa mchango huu, hasa katika nyanja za afya na elimu.”

Guinea ya Ikweta
Guinea ya Ikweta   (@Vatican Media)

Hatua ya Mwisho Gueine ya Ikweta

Hatua ya Nchi ya mwisho niliyotembelea ilikuwa Guinea ya Ikweta, miaka 170 baada ya uinjilishaji  wa kwanza. Kwa hekima ya tamaduni na mwanga wa Kristo, watu wa Guinea wamepitia mabadiliko ya historia yao, na katika siku za hivi karibuni, mbele ya Papa, walifufua kwa shauku kubwa azimio lao la kutembea pamoja kuelekea mustakabali wa matumaini.” Kwa njia hiyo Papa Leo XIV aliongeza “Siwezi kusahau kilichotokea gerezani huko Bata, Guinea ya Ikweta: wafungwa waliimba wimbo wa shukrani kwa Mungu na Papa kwa nguvu zao zote, wakiomba maombi "kwa ajili ya dhambi zao na uhuru wao." Sikuwahi kuona kitu kama hicho. Na kisha wakasali "Baba yetu" pamoja nami katika mvua iliyokuwa ikinyesha. Ishara halisi ya Ufalme wa Mungu!”

Papa akikutana na Wafungwa huko Bata Guinea ya Ikweta
Papa akikutana na Wafungwa huko Bata Guinea ya Ikweta   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV alieleza tena kuwa: “Na mkutano mkubwa na vijana katika uwanja wa Bata ulianza katika mvua iliyokuwa ikinyesha. Sherehe ya furaha ya Kikristo, pamoja na ushuhuda wa kugusa kutoka kwa vijana ambao wameipata katika Injili njia ya ukuaji huru na wa uwajibikaji. Sherehe hii ilifikia kilele katika sherehe ya Misa, siku iliyofuata, ambayo kama ipasavyo iliweka taji la ziara ya Guinea ya Ikweta na pia Ziara nzima ya Kitume.” Kwa kuhitimishwa Papa alisema “Wapendwa kaka na dada, ziara ya Papa ni fursa kwa watu wa Afrika kutoa sauti zao, kuelezea furaha ya kuwa watu wa Mungu na matumaini yao ya mustakabali bora, heshima kwa kila mmoja wetu. Ninafurahi kuwapatia fursa hii, na wakati huo huo ninamshukuru Bwana kwa kile walichonipatia, zawadi isiyo na kifani kwa moyo wangu na huduma yangu.”

KATEKESI YA PAPA APRILI 29

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here

29 Aprili 2026, 11:38