Tafuta

Papa Leo XIV,Angola:Mambo muhimu,Aprili 19,kusali Rozari na Misa

Mamã Muxima,mahali pa kale pa ibada asili yake inaanzia karne ya 17,ambapo ilikuwa sehemu ya wakoloni wa Ureno walipopanga bidhaa na kuwapeleka watu watumwani Brazil.Ni hapo alasiri Aprili 19,Papa aliongoza Sala Takatifu ya Rozari na kuomba kumpenda kila mtu kwa moyo wa kimama,kwa uthabiti na ukarimu na kujitoa hasa kwa maskini zaidi.Aliwaalika vijana kujenga Ulimwengu bora mahali ambapo hakutakuwa na dhuluma tena.

Na Angella Rwezaula - Vatican.

Ni takriban kilomita 130 kutoka mji Mkuu Luanda nchini, kwenye kingo za Mto Kwanza, mkubwa zaidi nchini Angola, ambao una mimea mingi kwenye kingo zote mbili, na kwa karne nyingi Bikira amekuwa Mamã Muxima, maana yake Moyo wa Mama, kama anavyoitwa katika lugha ya Kimbundu. Ni eneo la Kihistoria ambalo lilikuwa ni sehemu ya wakoloni wa Ureno walipopanga watu kama bidhaa, kwa kuwauza na kuwapeleka utumwani nchini Brazil.

Papa akisali katika Madhabahu ya Mama Maria huko Muxima
Papa akisali katika Madhabahu ya Mama Maria huko Muxima   (@Vatican Media)

Kila mwaka panaheshimika mahali hapo patakatifu, pa karne ya 17 penye sanamu ya kale ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya Asili. Madhabahu hiyo ilitangazwa kuwa kituo cha hija kitaifa kunako 1924, na ndiyo madhabahu inayopendwa zaidi na watu wengi nchini Angola. Maelfu ya Mahujaji humiminika kwa wingi kutoka nchini kote Angola, wakitafuta neema, uponyaji, upatanisho wa kifamilia, amani ya ndani, na ulinzi kutokana na hatari za maisha. Ni eneno kwa hiyo la kumkabidhi Mama Maria wasiwasi na huzuni zao, furaha na matumaini yao.

Waamini waliofika kusali Rozari
Waamini waliofika kusali Rozari   (@Vatican Media)

Kwa kawaida na kama mtindo karibu wa kiafrika, wanapofika hapo wengine hukaa hata siku nyingi karibu na Moyo wa Mama, wakipiga kambi karibu na kuvumilia hata magumu kama ishara ya upendo wao kwake. Na ndiyo ilikuwa wakati wanamsubiri Papa ambapo walikesha kwa sala na kupiga kambi.

Kambi zilipigwa na waamini wakimsubiri Papa
Kambi zilipigwa na waamini wakimsubiri Papa   (@Vatican Media)
Waamini kwa imani kuu walipiga kambi kumsubiri Papa ili kusali Rozari
Waamini kwa imani kuu walipiga kambi kumsubiri Papa ili kusali Rozari   (@Vatican Media)
Mama Maria utuombee
Mama Maria utuombee   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo, katika fursa ya Ziara ya Baba Mtakatifu Leo XIV nchini Angola imekuwa tena furaha kubwa Dominika tarehe 19 Aprili 2026 kushiriki kama mhujaji kwenye sala ya Rozari Takatifu na waamini wapatao takribani 30,000 huko Muxima, katika Jimbo Katoliki la  Viana, ili kumwomba Maria.

Palipo na Mama Maria kuna hata Msalaba.
Palipo na Mama Maria kuna hata Msalaba.   (@Vatican Media)
Papa alisali Rozari na waamini
Papa alisali Rozari na waamini   (@Vatican Media)
Mtoto akiongoza fungu la Rozari
Mtoto akiongoza fungu la Rozari   (@Vatican Media)
Mama Maria Utuombee
Mama Maria Utuombee   (@Vatican Media)
Waamini kwa ajili ya sala ya Rozari
Waamini kwa ajili ya sala ya Rozari   (@Vatican Media)
Waliofika kusali Rozari
Waliofika kusali Rozari   (@Vatican Media)
Hata Watoto walifika na wazazi wao kusali Rozari na Papa
Hata Watoto walifika na wazazi wao kusali Rozari na Papa   (@Vatican Media)

Kabla ya kufika Baba Mtakatifu Waamini walimsubiri Papa kwa hamu kubwa na maandalizi mazuri.

Kabla ya kufika Papa maandalizi katika madhabahu ya huko Muxima
19 Aprili 2026, 18:33