Tafuta

2026.03.17 Papa Leone XIV Videomessaggio Ceama Amazzonia 2026

Papa Leo XIV kwa Chuo cha Kipapa cha Sayansi:Matumizi ya nguvu za kiteknolojia kuwa tishio la demokrasia

Katika ujumbe wa Papa Leo XIV kwa Chuo cha Kipapa cha Sayansi Jamii,ambacho kimanza mkutano wake mkuu kuanza tarehe 14 hadi 16 Aprili 2025 anabainisha kuwa Demokrasia lazima itegemee sheria ya maadili au tunahatarisha udhalimu.Mkusanyiko wa nguvu za kiteknolojia,kiuchumi na kijeshi mikononi mwa wachache unatishia ushiriki wa kidemokrasia wa watu na maelewano ya kimataifa.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Haki na ujasiri ni muhimu kufanya maamuzi sahihi na kutekeleza maamuzi.Demokrasia inabaki kuwa na ustawi tu, inapojikita katika sheria ya maadili na maono ya kweli ya mwanadamu. Tunapaswa kukumbuka kwamba utaratibu wa kimataifa wa haki na thabiti hauwezi kutokea kutokana na usawa wa nguvu au kutokana na mantiki ya kiteknolojia pekee. Nguvu ya kimungu haiongoi, bali huponya na kurejesha. Ni matumaini kuwa mkutano utachangia ujenzi wa utamaduni wa kimataifa wa upatanisho na amani ambayo si tu ukosefu dhaifu wa migogoro, bali tunda la haki, linalotokana na mamlaka yaliyowekwa kwa unyenyekevu kwa ajili ya huduma ya kila mwanadamu na familia nzima. Haya na mengine yamo katika ujumbe kwa lugha ya Kiingereza wa Baba Mtakatifu Leo XIV kwa washiriki wa Mkutano Mkuu wa Chuo cha Kipapa cha Sayansi Jamii, ulioanza wa siku mbili ya tarehe 14 hadi 16 2026, kwa kuongoza na mada: Matumizi ya Nguvu: Uhalali, Demokrasia, na Ufafanuzi Mpya wa Utaratibu wa Kimataifa.

Mada inayofaa kutafakari juu ya utumiaji wa mamlaka

Katika ujumbe huo,  Papa anaanza na salamu na kutoa shukrani zake kwa Kardinali Peter Turkson kwa huduma yake ya kujitolea kama Chansela wa Chuo hicho. Vile vile alimshukuru Rais wao  Sr Helen Alford, kwa kuchagua mada: "Matumizi ya Mamlaka: Uhalali, Demokrasia na Uandishi Mpya wa Utaratibu wa Kimataifa." Papa alisisitiza kwamba “Ni mada ya wakati unaofaa hasa, ikilenga tafakari yetu juu ya utumiaji wa mamlaka, ambayo ni kipengele muhimu cha kujenga amani ndani na miongoni mwa mataifa katika wakati huu wa mabadiliko makubwa ya kimataifa.” Mafundisho ya kijamii ya Kikatoliki hayazingatii mamlaka kama lengo lenyewe, bali kama njia iliyopangwa kuelekea manufaa ya wote. Hii ina maana kwamba uhalali wa mamlaka hautegemei mkusanyiko wa nguvu za kiuchumi au kiteknolojia, bali hekima na wema ambao unatumika (taz. KKK 1903).

Hekima inatuwezesha kutambua kufuata ukweli

Papa alikazia kusema kuwa "Kwa maana hekima inatuwezesha kutambua na kufuata kweli na mema, badala ya mema yanayoonekana na majivuno, katikati ya hali ya maisha ya kila siku. Hekima hii haitenganishwi na fadhila za maadili, ambazo huimarisha hamu yetu ya kukuza manufaa ya wote. Hasa, tunajua kwamba haki na ujasiri ni muhimu kwa kufanya maamuzi sahihi na kwa kutekeleza maamuzi."  Kiasi pia Papa alisema "kinathibitisha kuwa muhimu kwa matumizi halali ya mamlaka, kwani kiasi cha kweli huzuia kujikweza kupita kiasi na hufanya kazi kama kinga dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka. Uelewa huu wa nguvu halali ni mojawapo ya vielelezo vyake vya juu katika demokrasia halisi. Mbali na kuwa utaratibu tu, demokrasia inatambua utu wa kila mtu na inamtaka kila raia kushiriki kwa uwajibikaji katika kutafuta manufaa ya wote. Akionesha imani hii, Mtakatifu Yohane Paulo II alithibitisha kwamba Kanisa linathamini demokrasia kwa sababu linahakikisha ushiriki katika chaguzi za kisiasa na "uwezekano wa kuwachagua na kuwawajibisha wale wanaowaongoza, na kuwabadilisha kwa njia za amani inapobidi” (Centesimus Annus, 46).

Demokrasia inabaki kuwa na ustawi inapojikita katika sheria ya maadili na maono ya mwanadamu

Hata hivyo, Papa alisema demokrasia inabaki kuwa na ustawi tu, inapojikita katika sheria ya maadili na maono ya kweli ya mwanadamu. Kwa kukosa msingi huu, ina hatari ya kuwa udhalimu wa wengi au kinyago cha kutawala wasomi wa kiuchumi na kiteknolojia. Kanuni zile zile zinazoongoza utumiaji wa mamlaka ndani ya mataifa lazima pia zieleze utaratibu wa kimataifa,  ukweli ambao ni muhimu sana kukumbuka wakati ambapo ushindani wa kimkakati na miungano inayobadilika inabadilisha uhusiano wa kimataifa.” “Tunapaswa kukumbuka kwamba utaratibu wa kimataifa wa haki na thabiti hauwezi kutokea kutokana na usawa wa nguvu au kutokana na mantiki ya kiteknolojia pekee.”

Wingi wa Teknolojia, kiuchumi na kijeshi kuwa mikononi mwa wachache ni tishio la ushiriki wa demokrasia

Mkusanyiko wa nguvu za kiteknolojia, kiuchumi na kijeshi katika mikono michache unatishia ushiriki wa kidemokrasia miongoni mwa watu na makubaliano ya kimataifa. Katika suala hilo Papa alibainisha kwamba watangulizi wake  wameelezea hitaji la taasisi zilizosasishwa na mamlaka ya ulimwengu (taz. Yohane Paulo II, Centesimus Annus, 58; Pacem in Terris, 137), iliyoainishwa na kanuni (taz. Benedikto XVI, Caritas in Veritate, 57). Ukuzaji wa jumuiya kama hiyo ya udugu wa kimataifa unahitaji "aina bora ya siasa, moja inayohudumia kiukweli manufaa ya wote" (Francisko, Fratelli Tutti, 154). Kikweli, "ni muhimu zaidi kuliko hapo awali kufikiria upya kwa ujasiri njia za ushirikiano wa kimataifa" (Ziara ya Makao Makuu ya FAO katika Siku ya Chakula Duniani, 16 Oktoba 2025, 7).


Nguvu ya kimungu haiongoi,bali huponya na kurejesha

Hatatima Baba Mtakatifu alieleza kuwa "wakati mamlaka za kidunia zinapotishia utulivu wa amani,  ufafanuzi wa kawaida wa Agostino  kuhusu amani,  lazima tupate tumaini kutoka kwa Ufalme wa Mungu, ambao, ingawa si wa ulimwengu huu, unaakisi mambo ya ulimwengu huu na kufichua maana yake ya mwisho wa dunia. Katika mtazamo huu wa imani, tunakumbushwa kwamba uweza wa Mungu unaoneshwa hasa katika huruma na msamaha (taz. Thomas Aquinas, Summa Theologiae, I, q. 25, a. 3, ad 3); nguvu ya kimungu haiongoi, bali huponya na kurejesha. Ni mantiki hii hasa ya upendo ambayo lazima ihuishe historia, kwani shughuli za kibinadamu zilizoongozwa na upendo husaidia kuunda "mji wa kidunia" katika umoja na amani, na kuufanya , hata kama haujakamilika, matarajio na mfano wa "Mji wa Mungu"(taz. Benedict XVI, Caritas in Veritate, 7).

Kazi itachangia ujenzi wa utamaduni wa kimataifa wa upatanisho na amani ambayo si ukosefu wa migogoro,bali tunda la haki

Imani kama hiyo huimarisha azimio letu la kujenga utamaduni wa upatanisho unaoweza kushinda mitego ya kutojali na kutokuwa na nguvu (tazama Hotuba mbele ya Viongozi wa Kidini, 28 Oktoba 2025). Kwa hisia hizi, ni matumaini ya Baba Mtakatifu kwa  dhati kwamba tafakari zao katika siku hizi zitatoa maarifa muhimu ya kufafanua matumizi halali ya madaraka, vigezo vya demokrasia halisi na aina ya utaratibu wa kimataifa unaotumikia manufaa ya wote. Kwa njia hiyo, kazi yao itachangia kwa maana katika ujenzi wa utamaduni wa kimataifa wa upatanisho na amani yaani amani ambayo si ukosefu dhaifu wa migogoro, tu bali tunda la haki, linalotokana na mamlaka yaliyowekwa kwa unyenyekevu kwa ajili ya huduma ya kila mwanadamu na familia nzima ya wanadamu. Roho Mtakatifu, chanzo cha upendo wote na kifungo cha umoja na amani, awaangazie akili zao na kutegemeza juhudi zao. Papa anawaombea wote baraka tele za Mungu kwa hiari.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

14 Aprili 2026, 17:45