Tafuta

Papa Leo XIV:Matatizo ni mengi bali Bwana yu karibu na waliopondeka moyo!

Papa Leo XIV katika mahubiri yake katika Misa ya Amani na Haki iliyoadhimishwa katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda,Kaskazini Magharibi mwa Cameroon,Aprili 16,alieleza matatizo ndani kuanzia chuki na vurugu na yaongezwa na ya nje ambapo,kwa jina la uwekezaji,wanaendelea kuishambulia bara la Afrika ili kulinyonya na kulipora.Alihimiza uangalifu dhidi ya njia zinazochanganya imani na ushirikina au kumkana Mungu kwa njia za kiuchumi.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Pamoja na mioyo iliyojeruhiwa na migoro ya kizamani na mipya ya ukosefu wa usalama wa maisha na ugumu wa kuishi katika bara zuri ambalo linatendewa vibaya,  kwa hakika imeonesha roho ya wakazi wa Cameroon ambao Baba Mtakatifu Leo XIV wameonekana wakimshangilia kwa  furaha na amani. Ni katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda, mji mkuu wa eneo la Kaskazini Magharibi mwa Cameroon,  eneo la mgogoro kwa miaka kumi kati ya vikosi vya serikali kuu huko Yaoundé na vikundi vya kujitenga ambapo misa ilifanyika ambayo,  awali ilitanguliwa na ziara ndefu katika  Kigari cha Kipapa cheupe akizunguka  na kwa shauku ya waamini wapatao elfu ishirini, kwa  nyimbo za kiutamaduni, bendera za Cameroon  na Vatican, na matawi  yakipeperushwa juu ambayo ni mila na tamaduni za nchi hiyo  na kama ishara ya kukaribishwa, kuzaliwa upya, na maisha.

Misa katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda
Misa katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda   (@Vatican Media)

Kushirikishana ugumu na matumaini

Baba Mtakatifu Leo IV akiwa jukwaa la altare, mara baada ya masom alianza mahubiri kuwa: “Kama Mwahija wa amani na umoja, ninakuja katikati yenu na kuelezea furaha ya kujikuta hapa kutembelea Mkoa wenu na hasa kwa kushirikishana na safari yenu, ugumu na matumaini yenu.”  Papa aliendelea, “Sherehe zinazoambata na  furaha inayosindikiza liturujia zenu, na furaha ambayo inabubujika kutoka katika sala ambayo mnainua kwa Mungu, ni ishara ya kujikabidhi kabisa kwa imani kwake, kutokana na  imani yenu isiyoanguka,  ya kushikilia kwenu, kwa nguvu zote, upendo wa Baba ambaye anakuwa karibu na kutazama kwa huruma  mateso ya watoto wake.”

Papa wakati wa Ibada ya Misa huko Bamenda
Papa wakati wa Ibada ya Misa huko Bamenda   (@Vatican Media)

Bwana yu karibu na waliovunjika:Matatizo ni mengi

Katika Zaburi ambaye wamesali pamoja, na kuomba kwa imani katika Yeye Papa alisema  “leo hii tunaitwa kupyaisha: “Bwana yu karibu nao waliovunjika moyo, Na waliopondeka roho huwaokoa(ZAb 34,18 au 19).” Kwa njia hiyo  alisema sababu ni nyingi  na hali ambayo inavunja moyo na kutuingiza katika  ushirika katika: Matumaini ya wakati ujao ya amani na upatanisho, kiukweli, ambamo kila mmoja anaheshimia katika hadhi yake na kila mmoja yanahakikishwa haki ya lazima, inayokaushwa   kila mara na matatizo mengi  ambayo yanaikumba nchi hii nzuri kama vile: Mitindo mingi ya umaskini, ambayo hata ya hivi karibuni imehusisha watu wengi kwa mgogoro wa chakula unaondelea; ufisadi wa kimaadili, kijamii na kisiasa, unohusu hasa uendesha wa utajiri ambao unazuia maendeleo ya kitaasisi na miundo yake, matatizo makubwa na yanayoendelea ambayo yanahusiana na mfumo wa kielimu na ule wa kiafya, kama ilivyo sehemu kubwa ya uhamaji wa kwenda nje ya nchi kwa namna ya pekee vijana.”

Misa katika Uwanja wa Bamenda
Misa katika Uwanja wa Bamenda   (@Vatican Media)

Matatizo ya ndani kuanzia chuki na vurugu yaongezwa na ya nje

Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa “Na kwenye matatizo ya ndani, ambayo mara nyingi huchochewa na chuki na vurugu, yanaongezwa uovu unaosababishwa kutoka nje, na wale ambao, kwa jina la uwekezaji, wanaendelea kuishambulia bara la Afrika ili kulinyonya na kulipora.” Haya yote yanahatarisha kutufanya tujisikie hatuna nguvu na kuharibu imani yetu. Hata hivyo, “huu ni wakati wa mabadiliko, wa kubadilisha historia ya nchi hii.” Leo, si kesho, sasa, si katika siku zijazo, wakati umefika wa kujenga upya, kuunganisha tena picha nzuri  ya umoja kwa kuunganisha utofauti na utajiri wa nchi na bara, ili kujenga jamii ambapo amani na upatanisho vinatawala.

Misa katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda
Misa katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda   (@Vatican Media)

“Mungu hutufanya watu jasiri ambao,kwa kupinga uovu,hujenga mema”

Baba Mtakatifu aliendelea kusema kuwa “Ni kweli kwamba hali inapoimarika kwa muda fulani, hatari ni kujiuzulu na kutokuwa na msaada, kwa sababu hatutarajii chochote kipya. Hata hivyo, Papa aliongeza kuwa “ Neno la Bwana hufungua nafasi mpya na hutoa mabadiliko na uponyaji. Lina uwezo wa kuchochea moyo, kupinga mtiririko wa kawaida wa mambo ambayo tunahatarisha kwa urahisi kuyazoea, na kutufanya kuwa wahusika wakuu wa mabadiliko. Tukumbuke hili: Mungu ni mpya, Mungu huumba vitu vipya, Mungu hutufanya watu jasiri ambao, kwa kupinga uovu, hujenga mema.”

Wanakwaya katika Misa huko Bamenda
Wanakwaya katika Misa huko Bamenda   (@Vatican Media)

Imetupasa Kumtii Mungu

Hii tunaona kwenye ushuhuda wa Mitume, ambao Somo la Kwanza lililosikika: Wakati  Baraza lilikuwa likiwauliza mitume na kuwakaripia na kuwatishia ili wasitaangaze adharani Kristo, wao walijibu: Imetupasa kumtii Mungu kuliko wanadamu. Mungu wa baba zetu alimfufua Yesu, ambaye ninyi mlimwua mkimtundika katika mti,” (Mdo 5,29-30). Ujasiri wa mitume, unafanya ukosoaji wa dhamiri, unafanya unabii, unakataa mabaya, na hiyo ndiyo hatua ya kwanza ya kufanya mabadiliko ya mambo. Kutii  Mungu kiukweli si tendo la kujinyenyekeza kwamba anatukandamiza au anaondoa uhuru wetu; kinyume chake, utii kwa Mungu, kunatufanya kuwa huru, kwa sababu una maana ya kukaribishi maisha yetu kwake na kuacha  Neno lake lituhuishe, namna yetu ya kufikiri na kutenda.

Maaskofu walioshiriki Ibada ya Misa Takatifu
Maaskofu walioshiriki Ibada ya Misa Takatifu   (@Vatican Media)

Anayetii Mungu hawezi kujikabidhi kwa mabaya

Kwa njia hiyo Papa alisema kuwa “ kama tulivyosikia kutoka katika Injili ambayo imetupeleka katika sehemu ya mwisho ya mazungumzo kati ya  Yesu na Nikodemu kwamba: “ Yeye ajaye kutoka juu, huyo yu juu ya yote. Yeye aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, naye anena mambo ya duniani. Yeye ajaye kutoka mbinguni yu juu ya yote,”( Yh 3,31). Anayetii kwa Mungu zaidi ya watu, na ana namna ya kufirikia kibina damu na kidunia, anapata uhuru wake wa ndani, anaweza kugundua thamani ya wema na hawezi kujikabidhi kwa mabaya, anagundua njia  ya maisha, anageukia kuwa mjenzi wa amani na udugu.

Misa katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda
Misa katika Uwanja wa Ndege wa Bamenda   (@Vatican Media)

Ni kutii Mungu na siyo binadamu

Baba Mtakatifu Leo XIV alisisitiza kuwa kmfuata kkwa walio na  mioyo iliyovunjika na matumaini katika kubadilisha jamii, vyote vinawezekana ikiwa tunamkabidhi Mungu na Neno lake. Ni wito wa  Mtume Petro. Lakini lazima na daima kutunza katika moyo na kupeleka katika maisha yetu ya kumbu kumbukumbu kwamba:“kutii Mungu na siyo binadamu.” Kutii Yeye kwa sababu Yeye ni Mungu. Na huo ndiyo mwaliko wa kuhamasisha, utamadunisho wa Injili na kukesha kwa umakini, hata juu ya udini wetu, ili tusije kuangukia katika ulaghai wa kufuata njia ambazo zinanyanya ukatoliki na imani nyingine, na mila za kishirikiana au za kiagnostiki (wale wanaodai kumiliki elimu ya juu,si bila Mungu)ambazo kiukweli mara nyingi zinaishia  katika kusudi la sera za kisiasa na kiuchumi.

Zawadi ya Papa kwa Bamenda
Zawadi ya Papa kwa Bamenda   (@Vatican Media)

Ni Mungu tu ambaye anaokoa

Ni Mungu tu ambaye anaokoa, ni neno lake tu ambao linafungua nyayo za uhuru, ni Roho wake tu, anatufanya kuwa watu wapya ambao wanabadilisha Nchi hii.” Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu Leo XIV alisema anavyowasindikiza kwa sala zake kila siku na kuwabariki kwa namna ya pekee Kanisa: Mapadre, wengi, wamisionari, watawa, walei wanaofanya kazi ili kuwa “kisima cha faraja na matumaini.” Papa aliwatia moyo kuendelea katika njia hiyo na kuwakabidhi kwa Maombezi ya Maria Mtakatifu, Malkia wa Mitume na Mama wa Kanisa.

Kwaya
Kwaya   (@Vatican Media)
Sehemu ya Mahubiri huko Bamenda

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

16 Aprili 2026, 17:52