Papa Leo XIV:Algeria inatoa fursa nzuri ya kujenga madaraja na mazungumzo
Salvatore Cernuzio-Algiers/Yaoundé na Angella Rwezaula–Vatican.
Baba Mtakatifu Jumatano tarehe 15 Aprili 2026 akiwa katika Ndege ya kuelekea Cameroon kama kawaida aliwasalimia na kuzungumza na waandishi wa habari. Kwa mujibu wa Mwandishi wetu wa Vatican News aliyekuwa kwenye ndege hiyo Salvatore Cernuzio, alibainisha kwamba,“ awali yote alitumaini kwamba wote walipumzika na kuwa tayari katika hatua nyingine za safari yao.” Alionesha furaha ya kuwasalimia moja kwa moja huku akitafakari kuwa imekuwa safari nzuri iliyo barikiwa sana huko Algeria. Kadhalika alipenda kutoa shukrani zake kwa Mamlaka ya Algeria ambao waliwawezesha ziara hiyo.
Shukrani kwa Kanisa dogo na jamii ya Algeria
Kama walivyoona, waliweza hata kuwasindikiza na salamu, wakati wao wanaondoka kwenye uwanja wa Algeria. Hii ni ishara ya wema, ya ukarimu na ya heshima ambayo watu wa Algeria na Serikali waliwezesha kuonesha, kwa Kiti Kitakatifu na kwake mwenyewe binafsi. Papa Leo XIV aliongeza: “kwa hiyo ninatamani kueleza neno moja la shukrani na kama ilivyo pia neno la “utambuzi wa uwepo mdogo na wenye maana wa Kanisa Katoliki nchini Algeria.”
Baba Mtakatifu Leo XIV kadhalika alisema: “Tumehitimisha kama tunavyojua, baadhi ya ziara maalum sana iwe katika Basilika ya Mama yetu wa Afrika jana, huko Annaba, Basilika ya Mtakatifu Agostino katika kilima ambacho kinatawala mji wa kisasa wa Annaba, na iwe magofu ya Mji wa kirumi ya Hippo.” Hii ningesema, aliongeza “ni ishara yenye maana, kwa sababu Mtakatifu Agostino ambaye kama mjuavyo alikuwa Askofu wa Hippo kwa zaidi ya miaka therathini, kiukweli ni sura iliyopo wakati uliopitia na kwa hivyo inazungumza nasi mapokeo, inazungumza nasi kuhusu maisha, ya Kanisa na jinsi Kanisa lilivyokuwa katika karne za mwanzo.”
Mwaliko wa Mtakatifu Agostino wa kumtafuta Mungu
Na bado leo hii, Papa Leo XIV alisisitiza kuwa, ni taswira muhimu sana kwa sababu maandishi yake, mafundisho yake, tasaufi yake, mwaliko wake wa kutafuta Mungu na ukweli, ni kitu ambacho tunaitaji sana leo hii, ujumbe wa sasa kwa sisi sote leo hii, kama Waamini katika Yesu Kristo, lakini pia hata kwa watu wote.” Papa Leo XIV alisema kama walivyoona, hao waandishi, kwamba “hata watu wa Algeria ambao sehemu kubwa ni wale wasio wakristo, wanaheshimu na kujali kwa kina kumbukumbu ya Mtakatifu Agostino kama mmoja wa Mtoto wa ardhi yao. Kwa njia hiyo ilikuwa ni baraka maalum “kwangu kurudi tena kwa mara nyingine jana huko Annaba, lakini pia hata kwa kutoa Mtazamo kwa Kanisa na Ulimwengu ambao Mtakatifu Agostino anatupatia, kwa maana ya kutafuta Mungu, na jitihada za kujenga Jumuiya, kutafuta umoja kati ya watu, na kuheshimu watu wote, licha ya kuwepo tofauti.
Licha ya tofauti inawezekana kuishi kwa amani
Katika mhtasari huo wa Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea: “kwa namna hiyo siku mbili akiwa Algeria, anaamini walikuwa na fursa ya kuona maajabu ya kuendelea kujenga madaraja, na ikiwa inawezakana kusema na kuhamasisha mazungumzo. Katika hilo alikumbusha kuwa “kutembelea Msikiti ilikuwa na maana sana kwa sababu, “ilijionesha licha ya kuwa na imani tofauti, kuwa na namna tofauti ya kusali, na pamoja kuwa na mtindo tofauti wa kuishi, inawezakana kuishi pamoja kwa amani.” Na Papa anaamini kwamba, kuhamasisha aina hiyo ya picha ni jambo ambalo Ulimwengu unahitaji leo hii, na kwamba “ pamoja tunaweza kuendelea kwa kutoa ushuhuda wetu, wakati tunawendelea katika ziara yetu ya kitume” Kwa kuhitimsha aliwatakia safari njema kwamba “ Ni vizuri kuonana tena.”Asante kwa huduma yenu.”
Telegram
Mara baada ya kuaga katika Uwanja wa Kimataifa, wa Algeria kuelekea Yaoundé, Baba Mtakatifu Leo XIV alituma telegramu zake kwa mataifa mbali mbali aliyopitia katika anga zake. Na katika baraka zake waliwatakia “Amani na furaha,” “nguvu na maelewano,” “maridhiano na umoja na hekima na umoja.”
Algeria
Akimwandikia Rais wa Jamhuri ya Algeria Bwana Abdelmadjid Tebboune alibainisha kwamba akiwa anaondoka kutoka “kwa Watu wa Jamhuri huko mji mkuu Algiers,” anaeleza “shukrani za kina kwa Yeye na watu wote wapendwa wa Algeria kwa makaribisho ya joto na ukarimu mpana kwake wakati wa ziara yake.” Kwa kuwahakikisha sala zake, alitoa baraka za Mwenyezi Mungu za amani na furaha kwa taifa hilo
Niger
Na wakati anapitia juu ya anga la Nchi ya Niger, Baba Mtakatifu pia alituma salamu zake kwa Rais wa Jamhuri ya Abdourahamane Tchiani, huko Niamey. Papa alisema, “ninapopitia juu ya Nchi yake katika Ziara yangu ya Kitume kuelekea Jamhuri ya Cameroon, ninatuma salamu zangu za dhati kwako wewe mheshimiwa na watu wote wa Niger, kwa pamoja nikiwahakikishia sala zangu kwamba Mwenyezi atawapatia baraka za nguvu na maelewano.”
Chad
Papa akipitia Juu ya nchi ya Chad, alituma salamu zake kwa Rais Mahamat Idriss Déby Itno
Wa Jamhuri hiyo , huko N’Djamena mji Mkuu wa Chad. Papa Leo XIV aliandika kuwa: nikiwa nanaingia nafasi ya anga ya Chad katika ziara ya Kituma kueleka Jamhuri ya Cameroon,” alitoa sala zake za wema kwa Mheshimiwa na kwa “wazalendo wake wote, huku akiombea taifa hilo baraka za Kimungu za maridhiano na umoja.”
Nigeria
Papa Leo Vile vila baada ya kuinga katika anga la Nigeria, alimwandikia telegram Rais Bola Ahmed Tinubu wa Jamhuri ya Shirikisho la Nigeria huko Abuja katika mji Mkuu wa nchi hiyo: “Ninakutumia salamu wewe Mheshimiwa na Watu wa Nigeria wakati ninapitia juu ya nchi yangu nikiwa katika ziara yangu ya Kitume kuelekea Jamhuri ya Cameroon. Ninakuhakikishia sala zangu, kwa utashi ninaombea Taifa baraka nyingi za Mwenyezi Mungu za hekima na umoja.”
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
