Tafuta

2026.04.16 Papa Leo XIV alikutana na Kundi la Viongozi wa Kiislam katika ubalozi wa Vatican nchini Cameroon. 2026.04.16 Papa Leo XIV alikutana na Kundi la Viongozi wa Kiislam katika ubalozi wa Vatican nchini Cameroon.  (@Vatican Media)

Papa Leo XIV akutana na baadhi ya viongozi wa Kiislamu,Cameroon

Baada ya kurudi Yaoundé,Papa Leo XIV alikutana na wawakilishi kadhaa wa Jumuiya za Kiislamu za Cameroon,akiwahimiza watu wa imani zote kufanya kazi kwa amani inayotegemea heshima ya pande zote.

Vatican News

Papa Leo XIV alikutana Alhamisi jioni tarehe 16 Aprili 2026 na kundi la wawakilishi 12 wa jumuiya kadhaa za Kiislamu za Cameroon ambao baadhi yao aliwapokea Roma mnamo Desemba 2025. Kulingana na Matteo Bruni, Msememaji mkuu wa  Ofisi ya Vyombo vya Habari Vya Vatican,  mkutano huo ulifanyika katika Ubalozi wa Vatcina huko  Yaoundé, baada ya Papa kurudi kwa ndege kutoka Bamenda, ambapo alikaa siku hiyo.

Jumuiya zinazowakilishwa na viongozi wa Kiislamu zinafanya miradi kadhaa ya kukuza haki ya kijamii na ushirikiano ili kuwasaidia watu maskini zaidi wa idadi ya watu wa Cameroon, kwa kushirikiana na Kanisa Katoliki la eneo hilo. Bwana Bruni alisema Papa alimsalimia kila mtu mmoja mmoja na kusikiliza maneno ya makaribisho na shukrani zilizoelekezwa kwake na wale waliokuwepo. Viongozi wa Kiislamu walielezea shukrani kwa kazi iliyofanywa pamoja na Kanisa, kwa ziara ya Papa, na kwa maneno yake kuhusu mazungumzo na amani yaliyotolewa Alhamisi huko Bamenda. Kisha Papa Leo XIV alishiriki furaha yake ya kukutana nao na akatoa shukrani zake kwa makaribisho ya joto aliyopokea kutoka kwa kila mtu nchini Cameroon. Wakristo, Wakatoliki na wasio Wakatoliki, Waislamu, na watu wa dini za kiutamaduni.

Mkutano wa Papa na viongozi wa Kiislamu huko Cameroon
Mkutano wa Papa na viongozi wa Kiislamu huko Cameroon   (@Vatican Media)

Papa piaalizungumzia kuhusu migawanyiko ambayo wakati mwingine huingia miongoni mwa imani na dini, na kwamba lazima kila mtu akumbatie jukumu linalotokana na kukutana. Aliwahimiza Wakameruni wote kuendelea "kuwasilisha hamu ya kila mtu ya kupata amani, si amani ya kutojali, si amani inayoondoa utajiri wa tofauti, bali amani inayozaliwa tunapotambua kwamba sisi sote ni kaka na dada, viumbe vyote vya kipekee vya mmumba mmoja  na wote tumeitwa kuheshimu utu wa wote."

Nchini Cameroon Papa alielezea, kuna uwezekano mkubwa wa kutimiza ndoto hii, kama hamu ambayo inakuwa kujitolea. Papa Leo XIV aliwahimiza waliohudhuria kuendelea na njia hii ya mazungumzo na kuleta ujumbe na ndoto sawa kwa wengine, kwa Waislamu, na kwa wale wote ambao hawaelewi lakini wanaweza kujifunza kuona uzuri wa udugu, na kuleta faida kubwa kwa Kamerun yote.

Papa alikutana na viongozi wa Kiislamu
Papa alikutana na viongozi wa Kiislamu   (@Vatican Media)

Bwana Bruni alibainisha kuwa, Jumatano jioni tarehe 15 Aprili 2026, Papa alikutana na Maaskofu wa Cameroon. Wakati wa mkutano huo, Papa alisisitiza thamani kubwa ya ushirika, akiiita zawadi ya kukumbatiwa ndani ya Kanisa na kushiriki katika ulimwengu uliogawanyika na kupasuka kwa migogoro na mgawanyiko, pamoja na thamani ya maisha ya kiroho ya wachungaji, ambayo huwafanya kuwa mashahidi wa kweli.

Maaskofu wa Cameroon
Maaskofu wa Cameroon   (@Vatican Media)

Alizungumzia baraka inayotokana na miito mingi nchini Cameroon na changamoto inayotokana ya kuwafunda vijana kwa uwajibikaji, katika viwango vya kiroho, kiakili, na kihisia, kama mapadre ambao mamlaka yao pekee ni huduma, baada ya mfano wa Kuosha Miguu uliofanywa na Yesu na kurudiwa Alhamisi Kuu. Bwana Bruni alisema Papa alijibu maswali kadhaa kutoka kwa Maaskofu waliohudhuria na kujikita na mada mbalimbali zenye umuhimu mkubwa wa sasa kwa Cameroon.

Maaskofu wa Cameroon
Maaskofu wa Cameroon   (@Vatican Media)
PAPA NA VIONGOZI WA KIISLAMU

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here

17 Aprili 2026, 08:45