Tafuta

Papa Leo XIV:Jihadhari na wezi wachochea uovu na kuiba mustakabali wa amani

Kabla ya sala ya Malkia wa Mbingu Papa alisitizia Kristo Mchungaji Mwema anayewajua kondoo na alionya dhidi ya wale wanaoingia moyoni kuiba maisha na kudhalilisha hadhi ya mtu.Ni pamoja na mawazo,ubaguzi na mitindo ya maisha inayoakisiwa na hutumiaji hovyo.“Tusisahau hata wezi wanaoiba rasilimali ardhi,kwa mapigano ya vita vya umwagaji damu,wanaiba mstakabali wa amani.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Tujiulize maswali: Je tunataka kuongozwa na nani katika maisha yetu? Ni wezi gani ambao walijaribu kuingia katika zizi letu? Je waliweza au tulikuwa na uwezo wa kuwasukumiza nje? Ni maswali ya Papa Leo XIV, Dominika ya Nne ya Pasaka ambayo inaitwa Dominika ya Mchungaji Mwema, sanjari na Siku ya 63 ya Kuombea Miito Duniani. Akiwa katika Dirisha la Jumba la Kitume, akidadavua Injili ya Siku kutoka Yohane. Kwa kuwageukia waamini na mahujaji waliokusanya katika Uwanja wa Mtakatifgu Petro, Papa alisema: “Wakati tukiendelea katika safari yetu ya kipindi cha Pasaka, Injili inatupeleka leo hii katika maneno ya Yesu ambaye anajifananisha kama Mchungaji mwema na baadaye katika Mlango wa Zizi(Yh 10,1-10).

Msimamo wa Yesu kuwa mchungaji mwema tofauti na mwizi anayeiba

Yesu anaweka msimamo wa kukubalika wa Mchungaji na mwizi. Kwa hakika anathibitisha: “Yeye asiyeingia kupitia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akakwea penginepo, huyo ni mwizi naye ni mnyang’anyi,”(Yh 10,1. Na mbele zaidi kwa njia ya wazi kabisa anasema: “Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele,”(Yh 10,10).” Utofauti huko wazi kabisa: mchungaji ana uhusiano maalum kwa kondoo wake, kwa hiyo anaweza kuingia kupitia mlango wa zizi; kinyume chake mmoja akiwa na shida ya kukwea zizi kwa hakika ni mwizi ambaye anataka kuiba kondoo.

Yesu ana uhusiano na sisi na kutoa maisha kwa ajili yetu

Yesu yuko anatueleza kuwa, Yeye anafungamana nasi,kwa kutuolea maisha na uhusiano wa kirafiki: Yeye anatujua, anatuita kwa jina, anatuongoza na kama mchungaji afanyavyo kwa kondoo wake, anakuja kwetu kututafuta,  wakati tunapopotea na kufunga majeraha yetu,  wakati tukiwa tunaumwa (Ez 34,16). Yesu haji kama mwizi, ili kuiba maisha yetu na uhuru wetu, bali  kutupeleka katika nyayo zilizo sahihi.Haji kututeka nyara au kulaghai dhamiri zetu, bali anakuja kuziangazia kwa mwanga wa hekima yake. Haji kama anayechafua furaha zetu za dunia, bali anazifungua katika furaha iliyo kamili zaidi na ya kudumu. Kwa anayemkabidhi Yeye hawezi kuogopa lolote: Yeye hafedheheshi maisha yetu, bali anakuja kuyatoa kwetu tele(Yh 10,10).

Kesheni kwa sababu kuna wezi wanaobadilisha sura nyingi

Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea kusema, “sisi tunaalikwa kutafakari na hasa kukesha juu ya zizi la moyo wetu na maisha yetu, kwa sababu anayekuja kuingia,  anaweza kuongeza furaha au kama mwivi anaweza kuiiba! “Wevi,” Papa Leo XIV alikazia kusema, “wanaweza kujibadilisha kwa sura nyingi: Ni wale ambao, licha ya ujuu juu wao, wanakandamizi uhuru wetu, au hawatuheshimu katika hadhi yetu; Ni washawishi, na kuwa na hukumu ambazo zinatuzuia kuwa na mtazamo wa utulivu kwa wengine na juu ya maisha: ni wenye mawazo potofu ambao wanaweza kutupelekea kutimiza chaguzi zilizo hasi; ni wa aina ya maisha ya kijuu juu au yaliyojaa matumizi ya hovyo, ambayo yanatuweka utupu wa ndani na kutusukuma kuhishia hata sisi daima kijuujuu.”

Tusisahau wanaoiba rasilimali ardhi kwa vita vya damu

Katika hilo Papa Leo XIV alitoa angalizo: “Tusisahau hata   wezi  wale wanaoiba rasilimali ardhi, kwa mapigano ya vita vya umwagaji damu, au kukuza ubaya kwa kila mtindo, hawafanyi zaidi ya kuibia wote uwezekano wa mstakabali  wa amani na utulivu.” Katika hilo, Papa ameomba kujiuliza maswali: Je tunataka kuongozwa na nani katika maisha yetu? Ni wezi gani ambao walijaribu kuingia katika zizi letu? Je waliweza au tulikuwa na uwezo wa kuwasukumiza nje Kwa kuhitimisha, Baba Mtakatifu Leo XIV alibanisha kuwa, “Injili ya leo,  inatualika kujikabidhi kwa Bwana: Yeye haji kutuibia lolote, badala yake ni Mchungaji mwema, ambaye anaongeza maisha kuwa tela na kutupatia yaliyo tele. Bikia Maria anatusindikize daima katika safari yetu na kwa ajili yetu na Ulimwengu mzima.

Tafakari kanla ya Sala ya Malkia

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.

26 Aprili 2026, 12:31