Papa Leo XIV,waathiriwa wa Nyuklia ya Chernobyl:Nguvu ya atomiki iwe ya amani
Na Angela Rwezaula – Vatican
Baba Mtakatifu Leo XIV, mara baada ya sala ya Malkia wa Mbingu akiwa katika Dirisha la Jumba la Kitume, Dominika tarehe 26 Aprili 2026 alikumbuka ajali mbaya iliyotokea huko Chernobyl nchini Ukraine ambayo "iliathiri dhamiri ya binadamu" na kusema: "Leo inaadhimishwa miaka 40 ya ajali mbaya ya Chernobyl, ambayo iliathiri dhamiri ya binadamu. Inabaki kuwa onyo la hatari zinazotokana na matumizi ya teknolojia zenye nguvu zaidi.”
Papa Leo XIV aliongeza: “Tunawakabidhi waathiriwa na wote ambao bado wanakabiliwa na matokeo hayo kwa huruma za Mungu. Kwa kugeukia ngazi za kimataifa, Papa aliongeza kusema: "Ninatumaini kwamba, katika ngazi zote za kufanya maamuzi, utambuzi na uwajibikaji vitashinda kila wakati, ili kila matumizi ya nishati ya atomiki yawe katika huduma ya maisha na amani.”
Salamu kwa mahujaji
Kisha Papa aliwageukia mahujaji na waamini kuanzia na Warumi na mahujaji kutoka nchi mbalimbali: na kuwakaribisha. Nawasalimu Shirika Kijeshi kike na kiume la Mtakatifu George, Shirika la Ulaya la Nyumba ya Habsburg-Lorraine. Nawasalimu watoto wa kikundi cha densi cha "Malva" kutoka Brovary, Ukraine; Kwaya ya ‘Cantica Sacra ya Jimbo Kuu la Trnava, Slovakia; waamini kutoka Vienna, Madrid, na Visiwa vya Canari;
Kadhalika Papa Pia aliwapa salamu Wakurugenzi na Walimu wa Shule ya "São Tomás" huko Lisbon. Nawasalimu kundi kubwa la watoto kutoka Val Camonica (Jimbo la Brescia) na wahudumu wa Altreni kutoka Biadene na Caonada; pamoja na waamini kutoka Treviso, Vicenza, Crotone na Cariati, Oria, na Lecce; na washiriki katika mkutano wa Chama cha Mitume wa Huruma ya Mungu.
Salamu kwa wazazi na marafiki wa Mapadre wapya wa Roma
Salamu maalum kwa familia na marafiki wa mapadre wapya wa Jimbo Kuu la Roma, ambao Papa aliwaweka wakfu Asubuhi ya Dominika Aprili 16 katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro ambapo Papa ameimba kwamba "daima wasindikizwe, hawa wahudumu vijana wa Injili kwa maombi." Alihitimisha kuwatakia Dominika Njema
Kuhusiana na ajali hii mbaya ya Chernobly
Ilikuwa yapata Saa 7:23 za usiku wa kuamkia tarehe 26 Aprili 1986, ambapo hitilafu katika mtambo wa nyuklia nambari 4 katika kiwanda cha nguvu za nyuklia cha Chernobyl ilittokea na kulipuka, karibu na Kyiev, mji wa Ukraine, na kusababisha ajali mbaya zaidi ya nyuklia katika historia ya nguvu za nyuklia. Mlipuko huo uliharibu sehemu ya ndani ya jengo, ukitoa wingu la moshi wenye mionzi angani. Kabla ya kuenea Ulaya yote, ulichafua maeneo makubwa ya Ukraine, Belarusi, na Urusi, na kulazimisha maelfu ya watu kuhama. Kuna watu ambao hawakurudi majumbani mwao, wakiacha kabisa eneo kubwa ambalo bado linachukuliwa kuwa "lisiloweza kukaliwa." Kwa hiyo ni baada ya miaka 40 ya kumbukumbu ya maafa mabaya zaidi ya nyuklia katika historia, ambayo yalisababisha uharibifu usiohesabika kwa afya ya binadamu na kasoro kubwa za kijenetiki kwa watoto ambao hawajazaliwa.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here.