Mambo muhimu katika siku ya sita ya Papa Leo XIV barani Afrika
Vatican News
Jumamosi asubuhi tarehe 18 Aprili 2026, Pap Leo XIV aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Ndege wa Yaoundé-Ville, katika siku yake ya mwisho kati ya tatu alizotumia nchini Cameroon, na kwa siku yake ya sita ya Ziara yake ya kitume barani Afrika.
Baada ya kufika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Yaoundé-Nsimalen, aliaga mamlaka ya kiraia na kidini ya nchi hiyo na saa 6:47 mchana saa za huko aliondoka kuelekea Luanda, mji mkuu wa Angola, ambapo alitua katika Uwanja wa Ndege wa "4 de Fevereiro" yapata saa 8:45 mchana saa za huko(ikiwa ni saa 9:45 alasiri saa za Roma).
Katika Uwanja wa Ndege alipokelewa na Rais wa Jamhuri hiyo Bwana João Manuel Gonçalves Lourenço, na vile vile katika Ikulu ya Rais na kukutana na mamlaka, asasi za kiraia, na kikundi cha kidiplomasia cha nchi hiyo.
Yapata saa 1:00 usiku kwa saa za huko, Papa alifanya pia mkutano wa faragha na Maaskofu Katoliki wa Angola.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwenye jarida letu la kila siku. Just click here
