Kardinali Simoni akutana na Papa Leo XIV:Nilimpatia masalia ya mashahidi wa Albania
Pd.Davide Djudjaj – Vatican.
"Furaha yote, matumaini yote." Hivi ndivyo Kadinali Ernest Simoni, mwenye umri wa miaka 97, wa Albania, alivyosema hata baada ya kuteswa nchini mwake wakati wa utawala wa kikomunisti, akizungumza na mwandishi wa habari wa Vatican News, kuhusu mkutano wake na Papa Leo XIV, mnamo tarehe 27 Aprili 2026. Mbali na Kadinali huyo, alikuwa amezungukwa karibu wanafamilia wake arobaini, waliomsindikiza katika Ukumbi wa Mapapa mjini Vatican. "Ilikuwa mazingira ya furaha yote, matumaini yote, kutazama uso wa Baba Mtakatifu, ambao unawakilisha uso wa Yesu, kuwatangazia watu wote habari za Mbinguni, za amani, za udugu, na za upendo kwa watu wote wa dunia," Kardinali Simoni alibainisha.
"Shahidi Aliye Hai"
Tayari kunako tarehe 5 Aprili iliyopita, ya Dominika ya Pasaka, Kardinali wa Albania alikuwa pamoja na Kadinali Protodeacon Dominique Mamberti, pamoja na Papa Leo XIV wakati wa ujumbe na baraka ya Urbi et Orbi kutokea kwenye Dirisha la katikati ya Basilika ya Mtakatifu Petro, mjini Vatican. Kardinali wa Jimbo Kuu la Shkodra-Pult (Scutari), aliyesherehekea miaka 70 ya kuwekwa wakfu kwake mnamo Aprili 7, aliteswa nchini Albania. Alipokamatwa wakati wa Noeli 1963, alihukumiwa kwanza kifo na kisha kufanya kazi ya kulazimishwa katika mifereji ya maji taka ya Shkodra, na baadaye akatekeleza huduma yake kwa siri hadi kuanguka kwa utawala wa kikomunisti.
Papa Francisko alikuwa amesikiliza ushuhuda wake wakati wa Ziara yake ya Kitume yake kwenda Albania mnamo Septemba 2014, akionekana kuguswa na kutokwa machozi na maneno ya Padre huyo, ambaye alimwita "shahidi aliye hai." Na mnamo 2016, Papa Francisko alimuumba kuwa Kardinali, kwa heshima huku akimshukuru kwa ushuhuda huu "ambao ni mzuri kwa Kanisa."
Kukutana na Papa ni neema maalum
Kwa hivyo, Mkutano huo na Papa Leo VIX: "Hakika ilikuwa neema maalum niliyopewa na Roho Mtakatifu," alisema Kardinali Simoni, "na pia na Baba Mtakatifu, kutangaza pamoja, kwa watu wote wa ulimwengu, amani itokayo Mbinguni, amani tamu zaidi, furaha ya kiroho, na furaha ya ufufuko. Na kila kitu kiko hapa: imani, pamoja na ufufuko, itakuwa na furaha ya milele ambayo Yesu aliandaa kwa kumwaga damu yake yote kwa watu wote wa ulimwengu na wa rika zote."
Kardinali, ambaye, licha ya umri wake, aliishi Firenze kwa miaka kadhaa na anaendelea kusafiri ulimwenguni, alimpatia Papa zawadi maalum mwishoni mwa kutano na kusema kwamba: "Nikija Italia kutoka Albania, mawazo yangu yako pamoja na mashahidi," na hivyo Kardinali Simoni aliwasilisha "msalaba na masalia ya mashahidi wa Albania waliotoa maisha yao kwa ajili ya uaminifu, kwa ajili ya upendo wa Yesu, kwa ajili ya wokovu wa watu wa Albania, ili kuwaona watu wote wakitabasamu Mbinguni."
Imesasishwa tarehe 28 Aprili 2026, saa 4.59 asubuhi na Angella Rwezaula.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku: Just click here
