Tafuta

Furaha ya Waamini wa Cameroon kumpokea Papa Leo XIV

Nyimbo na ngoma,muziki wenye mdundo wa kusisimua,makofi makubwa ya kuelezea furaha ya kuwasili kwa Papa Leo XIV katika eneo hilo la Bamenda Kaskazini-Magharibi mwa Cameroon,wakiwa wamejeruhiwa na mivutano na vurugu,lakini mbele ya ugeni mkubwa huo,hakuna mwenye majonzi wala masikitiko ni furaha ya kukaa pamoja.

Na Salvatore Cernuzio - Mwakilishi huko Bamenda

Sherehe kubwa barani Afrika si kuhusu ibada za ibada za majivuno, mavazi ya thamani, uvumba, na wahudumu madhabahuni. Bali sherehe ya kubwa barani Afrika inahusu  mambo machache tu na madogo ambayo ni muhi sana, kama vile wanawake wenye tabasamu pana, wakiwa wamevaa wigi na majoho makubwa au kanzu zenye miundo ya kikabila na vitenge vyene uso wa Papa, wakiimba "Baba Mtakatifu" au wakipuliza vuvuzela (kumbukumbu isiyofutika ya Kombe la Dunia la 2010).

Papa akizungukia waamini
Papa akizungukia waamini   (@Vatican Media)

Hawa ni wanaume wakiwa wamelowa jasho, wakigonga balafon kila mara na aina ya marimba ya mbao ili kuendana na wenzao, waliokuwa wafanya mazoezi ya kucheza.Ni maua ya rangi tofauti, mapazia yaliyooza kidogo kwenye ngazi na nguzo, milipuko mikubwa zaidi ya nyuso za Yesu na Papa, mabango yanayoitaka amani ya kudumu kwa nchi hii ambayo imeachwa pembezoni na, hakika, imepuuzwa na vyombo vya habari za kimataifa.

Waamini
Waamini   (@Vatican Media)

Na kwa hivyo, kwa maana hiyo, Mkutano wa Amani ulioongozwa na Papa Leo XIV katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, katika eneo la Big Mankon la Bamenda, lililopewa jina la utani na Papa "mji ulio juu ya kilima," ulikuwa wa heshima.

Kiongozi wa kikabila
Kiongozi wa kikabila   (@Vatican Media)

Kuwatazama watu hawa wakiimba na kucheza, wakitabasamu na kurukaruka, inaonekana kana kwamba matatizo pekee maishani ni joto kali, udongo mwekundu ukiingia machoni na puani mwao, na mbu wenye nguvu kiasi kwamba hutoa kelele sawa na ndege zisizo na rubani. Lakini vita vipo, kama vile hatari, ukame, umaskini unaoonekana katika maduka na majumbani, wengi wao wakiwa si kitu zaidi ya miundo ya matofali mekundu.

Wapiga marimba na kucheza
Wapiga marimba na kucheza   (@Vatican Media)
Wanawake wakiimba kiutamaduni
Wanawake wakiimba kiutamaduni   (@Vatican Media)

Hata hivyo, leo Papa Leo XIV pia yuko hapa, "mjumbe wa amani," kama mabango yaliyotawanyika kando ya njia zenye vumbi za jiji yanavyotangaza.

Furaha ya kumpokea Papa inaonkana machoni na katika rangi
Furaha ya kumpokea Papa inaonkana machoni na katika rangi   (@Vatican Media)

Watu wanaamini kwamba anaweza kweli kuimarisha mchakato huu. Mkataba wa siku tatu wa kusitisha mapigano uliotangazwa na vikundi vya kujitenga tayari umewavutia wengine kama ishara kutoka kwa Mungu, ingawa jiji linabaki chini ya uangalizi wa hali ya juu.

Mabango na furaha
Mabango na furaha   (@Vatican Media)
16 Aprili 2026, 17:55