Papa Leo XIV:Kanisa linaishi kwa kuwasilisha matumaini kwa wote!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika barua iliyotiwa saini Dominika tarehe 12 Aprili 2026, Baba Mtakatifu aliwatumia Makardinali akiwashukuru kushiriki nao katika mkutano nao wa kwanza tangu mwanzo wa upapa wake, ambao ulifanyika Vatikani mnamo tarehe 7 na 8 Januari 2026, na ulilenga mada za sinodi na utume. Barua hiyo inasubiri mkutano mwingine wa siku mbili wa mnamo tarehe 26 na 27 Juni 2026, utakaofanyika mjini Vatican karibu na Maadhimisho ya Watakatifu Petro na Paulo kwa kuhitimishwa na Maadhimisho ya misa Takatifu itakayoongozwa na Papa Leo XIV.
Wosia wa Evangelii Gaudium unaendelea kuwakilisha hatua muhimu ya marejeo
Papa aliandika kuwa alithamini kazi huru na yenye matunda inayofanywa katika vikundi, kiasi kwamba inaunda "urithi wa thamani ambao," alitaka kuendelea kulinda na kuhamasisha katika utambuzi wa kikanisa." Katika barua hiyo pia anatafakari kuhusu Evangelii Gaudium, ambao ni Wosia wa Kitume wa Papa Francisko uliochapishwa mwaka 2013, ambao unalenga kutangaza Injili duniani. "Kutokana na michango yenu, ni wazi kwamba Wosia huu unaendelea kuwakilisha hatua muhimu ya marejeo: hauleti tu maudhui mapya, bali unalenga kila kitu kwenye kerygma kama moyo wa utambulisho wa Kikristo na wa Kanisa," Papa anabainisha.
Ubora wa maisha ya kiroho pia unaguswa, katika ubora wa sala
Papa Leo XIV alizungumzia pumzi mpya ya kweli, inayoweza kuanzisha michakato ya uongofu wa kichungaji na kimisionari, badala ya kutoa mageuzi ya kimuundo ya haraka, hivyo kuelekeza kwa kina njia ya Kanisa. Kwa hivyo huu ni mtazamo unaolitia changamoto Kanisa katika ngazi zote kwa sababu, unamtaka kila mtu aliyebatizwa kuhama kutoka imani aliyopokea hadi imani yenye uzoefu; katika safari hii, ubora wa maisha ya kiroho pia unaguswa, katika ubora wa sala, katika ushuhuda unaotangulia maneno, na katika mshikamano kati ya imani na maisha." Katika ngazi yaki jamii, ni mpito hadi huduma ya uchungaji wa kimisionari, huku jumuiya zikiitwa kuwa karimu, kuwa makini na ubora wa mahusiano na uwezo wa kutoa nafasi za kusikiliza, kusindikiza, na uponyaji."
Mwaliko wa kuunga mkono kwa dhati ujasiri wa kimisionari
Kwa mtazamo wa kijimbo, Papa Leo XIV aliwaalika wachungaji kuunga mkono kwa dhati ujasiri wa kimisionari, kuhakikisha kwamba haulemewi au kukandamizwa na kupita kiasi kwa shirika, na kuhimiza utambuzi unaosaidia kutambua kile kilicho muhimu. Papa alikumbusha kwamba kwa njia hii, utume uliounganishwa sana unajitokeza wazi zaidi: Ukristo na kerygma, iliyozaliwa kutokana na kukutana na Kristo kwa kubadilisha maisha na kuenea kwa mvuto badala ya ushindi. Utume kamili, unaowaleta pamoja, utangazaji wazi, ushuhuda, kujitolea, na mazungumzo, bila kujisalimisha kwa kishawishi cha kugeuza imani au mantiki ya uhifadhi au upanuzi rahisi wa kitaasisi.
Kanisa, linaitwa kuishi bila ugumu, kama kundi dogo linaloleta matumaini kwa wote
“Hata linapojitambua kama kundi dogo, Kanisa, linaitwa kuishi bila ugumu, kama kundi dogo linaloleta matumaini kwa wote, likikumbuka kwamba lengo la utume si kuishi kwake lenyewe, bali ni mawasiliano ya upendo ambao Mungu anaupenda ulimwengu." Kwa hivyo, Evangelii Gaudium lazima ianzishwe upya, kwanza kwa kuchunguza kwa uaminifu kile kilichokubaliwa na kile ambacho hakijatekelezwa kwa miaka mingi. Kisha, "tahadhari lazima itolewe kwa mageuzi muhimu ya njia za kuanzishwa kwa Kikristo."
Kuthamini ziara za Kitume na kichungaji kama fursa halisi za kutafakari ukuaji wa mahusiano
Baba Mtakatifu Leo XIV pia alihimiza kuthamini ziara za Kitume na kichungaji kama fursa halisi za kutafakari kwa kina na ukuaji wa ubora wa mahusiano. Kuhusu mawasiliano ya kikanisa, alisisitiza hitaji la kufikiria upya ufanisi wao, hata katika ngazi ya Vatican katika mtazamo wa kimisionari ulio wazi zaidi. Barua hiyo inahitimisha kwa shukrani kwa huduma na mchango kwa Kanisa na inarejea Mkutano Mkuu wa Makardinali , utakaofanyika tarehe 26-27, na kwa tangazo la mawasiliano ya kina zaidi ili kusindikizana vya kutosha na maandalizi yake.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
