Tafuta

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Askofu Msaidizi Wilbroad Henry Kibozi, wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma kuwa Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Kondoa, kufuatia kifo cha Askofu Bernardin Francis Mfumbusa wa Kondoa. Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Askofu Msaidizi Wilbroad Henry Kibozi, wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma kuwa Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Kondoa, kufuatia kifo cha Askofu Bernardin Francis Mfumbusa wa Kondoa. 

Askofu Msaidizi Wilbroad Henry Kibozi Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki Kondoa

Papa Leo XIV amemteuwa Askofu Msaidizi Wilbroad Henry Kibozi, wa Jimbo Kuu la Dodoma kuwa Msimamizi wa Kitume Jimbo la Kondoa, kufuatia kifo cha Askofu Bernardin F. Mfumbusa kilichotokea tarehe 14 Aprili 2026. Huyu ni Askofu aliyekuwa na vipaji vingi, kiasi cha Papa Benedikto XVI kumteuwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo la Kondoa. Papa Leo XIV kwa kutambua na kuthamini karama na mapaji haya tarehe 9 Aprili 2026 alikuwa amemteua kuwa mjumbe!

Na Sr. Ernestina Patrick Lasway, SAC., Kondoa, Dodoma, Tanzania

Baba Mtakatifu Leo XIV amemteuwa Askofu Msaidizi Wilbroad Henry Kibozi, wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma kuwa Msimamizi wa Kitume Jimbo Katoliki la Kondoa, kufuatia kifo cha Askofu Bernardin Francis Mfumbusa kilichotokea tarehe 14 Aprili 2026 Majira ya Saa 11:45 asubuhi kutokana na ugonjwa wa shambulio la moyo kwenye Hospitali ya Benjamin Mkapa, BMH iliyoko Jijini Dodoma alikokuwa amepelekwa kwa matibabu ya dharura. Askofu Mfumbusa amezikwa kwenye Kanisa kuu la Roho Mtakatifu Jimbo la Kondoa Jumatano tarehe 22 Aprili 2026 katika Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Askofu mkuu Beatus Kinyaiya wa Jimbo kuu la Dodoma. Uteuzi huo ulioandikwa kwa niaba ya Baba Mtakatifu Leo XIV na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican umesomwa na Askofu mkuu Angelo Accattino Balozi wa Vatican nchini Tanzania.

Askofu Mfumbusa 1962 hadi 14 Aprili 2026
Askofu Mfumbusa 1962 hadi 14 Aprili 2026

Akitoa salam za rambirambi kutoka kwa Baba Mtakatifu Leo XIV Askofu mkuu Angelo Accattino Balozi wa Vatican nchini Tanzania amesema, kifo cha Askofu Bernardin Francis Mfumbusa kimekuwa ni cha ghafla, kiasi cha kuwashtusha watu wengi. Huyu ni Askofu aliyekuwa na karama na vipaji vingi, kiasi cha Baba Mtakatifu Benedikto XVI kumteuwa kuwa Askofu wa kwanza wa Jimbo Katoliki la Kondoa. Baba Mtakatifu Leo XIV kwa kutambua na kuthamini karama na mapaji haya, tarehe 9 Aprili 2026 Baba Mtakatifu Leo XIV alikuwa amemteua Askofu Bernardin Francis Mfumbusa, kuwa ni Mjumbe wa Baraza la Kipapa la Mawasilianiano ya Jamii. Askofu Mfumbusa alikuwa pia ni Rais wa Kamati ya Mawasiliano ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar, “Pan African Episcopal Conference For Social Communication, CEPACS,” kwa kuchaguliwa kwa nafasi hii kunako mwezi Agosti 2025, huko Kigali nchini Rwanda na angemaliza muda wa uongozi wake mwaka 2028.

Askofu Mfumbusa atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa
Askofu Mfumbusa atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa

Katika kipindi hiki cha uongozi wake amekazia sana umuhimu wa vyombo vya mawasiliano ya jamii sanjari na mitandao ya kijamii, kujikita katika mchakato wa uinjilishaji wa tamaduni na utamadunisho wa Injili unaoiwezesha Habari Njema ya Kristo Yesu kuingia na kupenyeza mizizi yake katika tamaduni mbalimbali, ikiikubali, ikiisafisha, na kuipatia maana mpya bila kuharibu utambulisho wa watu. Lengo ni kufanya Injili ya Kristo Yesu uwe ni ujumbe unaozungumza lugha na uzoefu wa watu mahalia Barani Afrika. Kwa hakika Kanisa limempoteza Askofu na mtaalam mbobezi wa Mawasiliano ya Jamii. Rais wa Kamati ya Mawasiliano ya Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu Afrika na Madagascar, “Pan African Episcopal Conference For Social Communication, CEPACS.”

Msimamizi wa Kitume Kondoa
22 Aprili 2026, 17:04