Ziara ya Papa Leo XIV:Taifa dogo la Ulaya linaweka ustawi katika huduma ya ubinadamu,sheria na haki
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa na Familia ya Kifalme, akiwageukia watu waliokusanyika katika Uwanja wa Jumba la Ufalme, mara baada ya Mfalme kuzungumza alianza kutoa hotuba yake kwa lugha ya kifaransa, Jumamosi tarehe 28 Machi 2026. Papa alionesha furaha ya kuwa miongoni mwao, kuwa wa kwanza kati ya Warithi wa Mtume Petro katika nyakati za kisasa kutembelea Ufalme wa Monaco, Jiji la Serikali linalotambulika kwa dhamana kubwa inayoliunganisha na Kanisa la Roma na imani ya Kikatoliki. "Kwa kutazama nje ya Bahari ya Mediterania na katikati ya nchi mwanzilishi wa umoja wa Ulaya, ardhi yenu ndani yaje ina uhuru wake, wito wa kukutana na kukuza urafiki wa kijamii, leo hii unaotishiwa na hali ya hewa iliyoenea ya kufungwa na kujitosheleza." Kwa njia hiyo Papa alisema "Zawadi ya udogo na urithi hai wa kiroho unatoa utajiri wenu kwa huduma ya sheria na haki, hasa wakati katika historia ambapo kujionyesha kwa nguvu na mantiki ya ukandamizaji huharibu ulimwengu na kuathiri amani."
Baba Mtakatifu aliendelea kudadavua kwamba, "Katika Biblia, kama unavyojua, watoto wadogo huandika historia! Mambo ya kiroho halisi huweka ufahamu huu hai. Lazima tuamini katika maongozi ya Mungu hata wakati hisia ya kutokuwa na nguvu au kutofaa inapotawala, kwa sababu tunaamini kwamba Ufalme wa Mungu ni kama mbegu ndogo inayokua na kuwa mti (taz. Mt 13:31-32). Kwa kawaida, imani hii hubadilisha ulimwengu tu ikiwa hatutashindwa katika majukumu yetu ya kihistoria," kwa njia hiyo "Muundo wa jamii yenu mnaojumuisha watu wengi ambao hufanya nchi hii kuwa ndogo, ambayo ustawi wake unachangiwa na wachache wenye nguvu wa watu wa eneo hilo na raia wengi kutoka nchi zingine kote ulimwenguni. Miongoni mwa hawa, wengi wana nafasi zenye ushawishi mkubwa katika nyanja za kiuchumi na kifedha, wengi hufanya kazi za huduma, na wengi pia ni wageni na watalii. Kuishi hapa kunawakilisha fursa kwa baadhi, na wito maalum kwa wote kuhoji nafasi yao duniani."
Papa Leo XIV alisisitiza kwamba " Machoni pa Mungu, hakuna kinachopokelewa bure! Kama Yesu anavyopendekeza katika mfano wa talanta, kile ambacho tumekabidhiwa hakipaswi kuzikwa chini ya ardhi, bali kinapaswa kusambazwa na kuzidishwa ndani ya upeo wa Ufalme wa Mungu. Upeo huu ni mpana kuliko wa faragha na hauhusishi ulimwengu wa ndoto: Ufalme wa Mungu, ambao Yesu alijitolea maisha yake, uko karibu, kwa sababu unakuja kati yetu na kutikisa miundo isiyo ya haki ya nguvu, miundo ya dhambi ambayo huunda pengo kati ya maskini na matajiri, kati ya wenye upendeleo na waliotengwa, kati ya marafiki na maadui."
Kila kipaji, kila fursa, kila jema lililowekwa mikononi mwetu lina hatima ya ulimwengu wote, hitaji la ndani sio la kuhifadhi, bali kusambazwa tena, ili maisha ya kila mtu yawe bora zaidi. Hii ndiyo sababu Yesu alitufundisha kuomba: "Utupe leo mkate wetu wa kila siku" (Mt 6:11); na wakati huo huo anasema: "Tafuta kwanza ufalme wa Mungu na haki yake" (Mt 6:33). Mantiki hii ya uhuru na kushiriki iko katika msingi wa mfano wa Hukumu ya Mwisho, ambayo inawaweka maskini katikati yake: Kristo Hakimu, aketiye kwenye kiti cha enzi, anajitambulisha na kila mmoja wao (Rej. Mt 25:31-46).
Imani ya Kikatoliki, Papa alisema ambayo wao ni miongoni mwa nchi chache duniani kuwa nayo kama dini yake ya serikali,inatuweka mbele ya Ufalme wa Yesu, ambaye anawakabidhi Wakristo kuwa ufalme wa kaka na dada duniani. Uwepo usioponda bali huinua, ambao hautenganishi bali huunganisha, tayari kulinda kwa upendo kila maisha ya mwanadamu, kila wakati na katika kila hali, ili mtu yeyote asiondolewe kwenye meza ya udugu. Kwa njia hiyo huu " ndio mtazamo wa ikolojia fungamani, ambayo “ninajua ni ya thamani sana kwenu. Ninaikabidhi kwa Ufalme wa Monaco, kwa sababu ya kifungo kikubwa kinachoiunganisha na Kanisa la Roma, kujitolea maalum sana kwa kuimarisha Mafundisho Jamii ya Kanisa na kuendeleza desturi bora za ndani na kimataifa zinazoonyesha nguvu yake ya mabadiliko."
Papa aidha alisema kuwa "Hata katika utamaduni ambao si wa kidini sana na usiojali sana dini, mbinu ya kutatua matatizo ya kawaida ya mafundisho ya kijamii inaweza kufichua mwanga mkubwa ambao Injili huleta kwa wakati wetu, wakati ambapo watu wengi wanaona ni vigumu sana kutumaini. Shukrani kwa imani ya kale, mtakuwa wataalamu katika mambo mapya: si kwa kufuata mali zinazopita, mara nyingi mambo mapya ambayo huchakaa baada ya muda, bali kwa kuwa tayari kukabiliana na changamoto ambazo hazijawahi kutokea, ambazo zinaweza kukabiliwa tu kwa moyo huru na akili iliyoelimika."
"Mnaelewa vizuri sana," alisema Mtakatifu Paulo VI katika maadhimisho ya miaka 75 ya Rerum Novarum, "kwamba katika kutembea, nuru inahitajika; kukuza maendeleo ya kijamii, mafundisho yanahitajika [...]; inadhaniwa kwamba huongoza maisha; na ikiwa mawazo yanaonesha ukweli, ukweli kuhusu mwanadamu, ulimwengu, historia, vitu, basi safari inaweza kuendelea kwa uhuru na haraka; ikiwa sivyo, safari inakuwa polepole, isiyo na uhakika, ngumu, au isiyo ya kawaida." Kwa kuongezea Papa alisema "Maneno haya ni ya wakati unaofaa sana! Kwa sababu hii, tunamwomba Maria, Kiti cha Hekima na Sababu ya furaha yetu, ili aweze kutuongoza kila wakati kwa akili zetu, mioyo yetu, na chaguo zetu kwa Kristo, Mfalme wa Amani. Pax vobis! Que la paix soit avec vous ! "Amani iwe nanyi" kwa lugha ya kilatini na kifaransa, Papa Leo alihitimisha.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.
