Tafuta

Ziara ya Kitume ya Papa Leo XIV huko Monaco:Papa amefika!

Muda mfupi tu baada ya saa 3:00 asubuhi,helikopta iliyokuwa imembeba PapaLeo XIV ilitua kwenye Uwanja wa(Heliport)wa Monaco.Mfalme Albert II na Malkia Charlene walimkaribisha Baba Mtakatifu.

Vatican News

Helikopta iliyokuwa imembeba Baba Mtakatifu Leo XIV ilitua muda mfupi baada ya saa 3:00 asubuhi, tarehe 28 Machi 2026, katika kituo cha Helikopta cha Monaco. Papa alikaribishwa na Mfalme Albert II na Malkia Charlene. Hii inaashiria mwanzo wa Ziara yake ya pili ya Kitume ya Papa  Leo XIV kwenda katika Ufalme huo, moja ya Nchi kongwe zaidi duniani na ya pili kwa ukubwa baada ya Jiji la Vatican. Baada ya Mkuu wa Ulinzi kumpatia heshima, salamu zilifuatia kwa mizinga 21, na uwasilishaji wa wajumbe husika kwa pande zote mbli, Papa Leo XIV alielekea Ikulu ya Mfalme kwa ajili ya sherehe ya kumkaribisha, ambayo ilifuatiwa na ziara ya heshima kwa Mfalme mwenyewe Albert II.

Makaribisho kutoka kwa Wafalme wa Monaco
Makaribisho kutoka kwa Wafalme wa Monaco   (@Vatican Media)

Mfalme, pamoja na mkewe na watoto wake, walimkaribisha Papa katika Uwanja wa Heshima ambapo sherehe ya kumkaribisha ilifuatia.

Kisha nyimbo za taifa, gwaride la Walinzi kwa Heshima, na heshima ya kupandishwa bendera ya Ufalme huo na Vatican na uwasilishaji wa wajumbe husika.

Kutua na heshima katika Ufalme
Kutua na heshima katika Ufalme   (@Vatican Media)

Saa 3:45 asubuhi, Papa na Mkuu wameingia Ikulu kwa ziara ya heshima. Hili ni tukio la kwanza la ziara yake, litafuatiwa na mkutano na jumuiya ya Wakatoliki katika Kanisa Kuu la Mama Maria Asiye na dhambi ya Asili na mkutano na vijana na wakatekumeni katika uwanja mbele ya Kanisa la Mtakatifu Dévote. Kisha, alasiri, Misa katika Uwanja wa Louis II.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

28 Machi 2026, 09:55