Tafuta

2025.10.03 I rappresentanti dei vescovi cattolici dell'Africa orientale visitano l'Etiopia, riunione sulla sinodalità

Uteuzi wa Mwandamizi wa Kitume wa Gambella (Ethiopia)

Baba Mtakatifu Leo XIV amemtueuwa Mhes. Padre Hailemariam Medhin Tesfay, S.D.B., kuwa Mwandamizi Msimamizi wa Kitume wa Gambella (Etiopia).

Vatican News

Tarehe 21 Machi 2026 Papa Leo amemteua Mhesh.Padre Hailemariam Medhin Tesfay, S.D.B., kuwa Mwandamizi wa Kitume wa Gambela nchini Ethiopia.  Alizaliwa tarehe 1 Oktoba 1973 na wazazi wake Medhin Tesfay na Amlesu Weldeselassie huko Alitena (Etiopia). Baadaye alijiunga na Shirika la Kimisionari la Wasalesiani wa Don Bosco huko Gotera(Addis Abeba), na kufunga nadhiri za daima mnamo 2001 huko Addis Abeba.

Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 4 Meo 2003 huko Adigrat.

Alifunika nyadhifa mbali mbali na kuendelea na masomo ya juu: Paroko na Mweka Hazina wa Adwa (2003-2006); cheti cha Taalimungu  kutoka Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salesian cha Roma(2006-2009); Mkufunzi wa Taalimungu huko Utume (Kenya) (2009-2013); Shahada ya Udkatari  wa Taalimungu katika Chuo Kikuu cha Kipapa cha Salesiani Roma (2013-2016); Gambera na Paroko wa  Mekanissa (Addis Abeba) (2016-2019);  Mkuu wa Provinsi ya “Kidane Meheref’ Etiopia-Eritrea (2019-2025); Rais wa Baraza la Wakuu wa Shirika nchini Ethiopia (2020-2025).

21 Machi 2026, 13:54