Parokia ya Torrevecchia inamsubiri Papa Leo XIV Dominika Machi 8
Na Benedetta Capelli –Vatican.
Mnara wa kengele wa chuma, ishara ya usanifu wa kisasa na wa siku zijazo, ndio kitu cha kwanza unachokiona mara tu unapofika Njia ya Torrevecchia 1104, nje kidogo ya magharibi mwa Roma. Kanisa la Uwasilishaji wa Mtakatifu Maria, ni mahali ambapo Papa Leo XIV atatembelea Dominika tarehe 8 Machi 2026. Kituo cha nne kati ya tano cha ziara zake kwenye Parokia za Roma kabla ya Pasaka, kinatoa ujumbe wazi hata katika mwonekano wake: "kuwa ishara, uwepo, ngome ya Kanisa lililo hai ambalo lipo." Kanisa linalokabili majeraha ya eneo la vitongoji, ugumu wa familia unaojaribiwa na ubaguzi wa kuishi mahali panapoonekana kuwa pagumu, lakini ni mahali ambapo kuna matumaini ya siku zijazo.
Ripoti za habari zimeonesha mara kwa mara, taswira mbaya ya Torrevecchia, iliyokumbwa na biashara ya dawa za kulevya na uhalifu. Vyombo vya habari vilivamia eneo hilo mwaka 2023 kufuatia mauaji ya kutumia kisu kwa Michelle Maria Causo mwenye umri wa miaka 17, ambaye mwili wake uliachwa karibu na dampo la takataka na muuaji. Huzuni kubwa kwa jamii inayofanya kazi kwa bidii. Hivi ndivyo Padre Paolo Stacchiotti, mwenye umri wa miaka 40, kutoka kitongoji cha Pisana, alivyoelezea, wito uliokuzwa katika Parokia hiyo na kustawi mwaka 2006.
Kuishi katika Vitongoji
Kardinali Baldo Reina, Makamu wa Papa, Jimbo Kuu la Roma alipomkabidhi uchungaji wa Torrevecchia, alimkabidhi kazi ya kuishi katika vitongoji na kuifanya iwe nzuri. "Nilihisi kualikwa kutoa kilicho bora," alisema Padre Stacchiotti, "ni kitongoji tata, lakini nina uhakika kitakuwa na mshangao mkubwa kwangu." Cha kwanza kilikuja miezi mitatu tu baada ya agizo lake, na tangazo la ziara ya Papa. "Bwana hafanyi mambo bila mpangilio. Ninafurahi kwa sababu ni fursa kwa eneo hili. Kuwa na Askofu wa Roma hapa ni usemi wa Kanisa ambalo halimwachi mtu yeyote."
![]()
Nyumba za vitongoji vya Bastogi
Njia panda za Ukweli
Padre Paolo aliendelea na ujirani mgumu lakini wenye nguvu na wenye shughuli nyingi. Parokia ya Uwasilishaji wa Mtakatifu Maria iko karibu na Basilika ya Mtakatifu Sofia, Kanisa la Kiukraine, Roma na moyo wa mshikamano usiokoma. Hatua chache kutoka hapo ni Bastogi, iliyojengwa miaka ya 1980 kama makazi ya umma, suluhisho la makazi ya muda huku ikisubiri makazi ya umma, ambayo kwa takriban watu elfu mbili bado hawajajengewa, ambapo wanategemea mitungi ya gesi kwa ajili ya kupasha joto na kupikia. Kwa kutazama kuelekea jirani na eneo la Primavalle, na karibu na Kanisa hilo kuna makazi ya Torrevecchia kando ya makazi ya umma, mchanganyiko ambao kwa Roma anaujua vyema.
Si mbali sana, unaweza pia kuona hema la sarakasi la Rony Roller, ambalo huwekwa kila mwaka kati ya Novemba na Januari, na hapa juma chache zilizopita, jambo lisilotarajiwa lilitokea. "Watu wa sarakasi walifika," alisema Padre Paolo, "kuniomba niadhimishe Komunyo ya Kwanza na Kipaimara cha watoto 11. Niliangalia katika ofisi za Vikariate na kugundua kwamba huduma hiyo sikuwahi kusikia. Kwa hiyo Makatekista wa Parokia waliwaandaa, na tukatoa sakramenti pamoja na Kardinali Konrad Krajewski, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Upendo ambaye alikuwa anawajua vyema. Jambo zuri lilikuwa kuona jinsi watoto hao walivyokaribishwa. Tuliadhimisha sakramenti ya kitubio pamoja, na nilihisi hitaji lao la kukutana na Yesu."
![]()
Maadhimisho ya Kipaimara na Komunio ya kwanza katika ukumbi wa Rony Roller
Mahali pa Imani
Miongoni mwa majengo katika eneo hili la pembezoni, hakuna uhaba wa uzoefu wa kutajirisha, makao ya imani" ya kweli, kama vile nyumba ya Silvia na Donatella, wanawake wawili wa kawaida wa Udugu wa Umwilisho ambao wameishi Bastogi kwa miaka 30. "Hapa," Paroko wa parokia alisisitiza, "unaweza kupata watu wakisimama kwa ajili ya kahawa, kuzungumza, au kusali katika Kanisa, ambapo wanatafakari Injili mara moja kwa Juma." Katika makazi ya umma ya Torrevecchia, kuna ukweli mwingine unaohusiana moja kwa moja na Parokia ya Uwasilishaji wa Mtakatifu Maria. Kutoka nje, unaweza kuonekana kama duka dogo lenye madirisha yaliyofunikwa na mapazia meupe, lakini ndani, unaweza kuona viti vya rangi nyepesi na altare: Ni kanisa lililowekwa wakfu kwa Mama Yetu wa Lourdes, ambapo Misa huadhimishwa kila siku, ama na Padre Paolo au na mapadre wawili anaoishi nao: Padre Jokens Antony, asili yake ni India, na Padre Richard Kenneth, ambaye anatoka Uganda. Kwa Padre Stacchiotti, ukweli huu ni "uendelezaji wa Parokia," makanisa madogo ya ndani yaliyojumuishwa katika historia ya eneo hili.
Muungano na Yohane Paulo II
Katika maandalizi ya ziara ya Papa Leo XIV, Padre Paolo aliandaa mkesha mnamo Februari 25 ili kumkaribisha Askofu wa Roma katika sala. Dominika tarehe 8 Machi 2026, ni ziara ya pili ya Papa: Mtakatifu Yohane Paulo II aliwasili katika Parokia hiyo mnamo tarehe 24 Oktoba 1982, lakini maisha ya shughuli za parokia wakati huo yalikuwa yakifanyika katika gereji. Paroko wa parokia wakati huo, Padre Pietro Beccaria, mwenye asili ya Mondovì, aliwasilisha barua kwa Papa Wojtyla mbele ya Katekesi mnamo tarehe 15 Novemba 1978, ambapo alisimulia ugumu wa kutokuwa na Kanisa na kwa usahihi akamwalika kutembelea Jumuiya hiyo. Miaka mingi ilipita, lakini hatimaye Papa wa Poland alifika, akitambua sifa ya Padre Pietro katika mahubiri yake ya Misa kwa kujenga "Parokia changa ya kimisionari ndani". "Parokia ya kawaida," mtoto alimwandikia Papa, "ambapo utapata upendo mwingi." Kulikuwa na uhusiano mwingine muhimu na Yohane Paulo II. Karol mdogo alibatizwa mnamo tarehe 20 Juni 1929, katika Kanisa la Wadowice, Poland, lililowekwa wakfu kwa Uwasilishaji wa Bikira Maria, jina lile lile la Parokia ya Torrevecchia.
Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here
