Tafuta

Papa Leo XIV:Wito kwa Wakatoliki wa Monaco kutangaza Injili kwa ubunifu na imani!

Katika Taifa dogo kama Monoco,lina wakazi mchanganganyiko kati ya watu mahalia na mataifa mengine tofauti.Katika Kanisa,tofauti hizo kamwe haziwi sababu ya mgawanyiko katika matabaka ya kijamii,kinyume chake,wote wanakaribishwa kama watu na watoto wa Mungu na wote ni wapokeaji wa zawadi ya neema inayohimiza ushirika,udugu na upendo wa pande zote.Kristo analiita Kanisa kwenye ushirika na ulinzi wa hadhi ya binadamu.

Na Angella Rwezula – Vatican.

Ni  muhimu kwamba tangazo la Injili na aina za imani, zilizojikita sana katika utambulisho  na jamii, zijilinde dhidi ya hatari ya kupunguzwa hadi kuwa tabia tu, hata iwe nzuri kiasi gani. Imani iliyo hai daima ni ya kinabii, inayoweza kuuliza maswali na kutoa uchochezi: je, kweli tunamtetea mwanadamu? Je, tunalinda heshima ya mtu katika kulinda maisha katika hatua zake zote? Je, mfumo wa sasa wa kiuchumi na kijamii ni wa haki na unaongozwa na mshikamano? Je, umejengewa maadili ya uwajibikaji, ambayo hutusaidia kupita zaidi ya "mantiki ya kubadilishana vitu sawa na faida kama lengo lenyewe" ili kujenga jamii yenye usawa zaidi? Haya yamo katika tafakari ya  Baba Mtakatifu Leo XIV aliyoitoa katika Jumuiya Katoliki ya Monaco, Katika Kanisa Kuu la Mama Asiye na dhambi ya Asili, Jumamosi asubuhi tarehe 28 Machi 2026 akiwa katika Ziara yake ya Kitume kwenye Nchi ndogo ya Bara la Ulaya.

Mkutano na Jumuiya ya Waktoliki wa Monaco
Mkutano na Jumuiya ya Waktoliki wa Monaco   (@Vatican Media)

Katika udhaifu wetu, tukiwa tumelemewa na mzigo wa dhambi unaoashiria ubinadamu wetu, Tumefikiwa na Mungu

Tukio hili ndani ya Kanisa Kuu ilikuwa ni katika  Masifu ya Kati ambapo mara baada ya somo, Baba Mtakatifu alianza kuzungumza kwa lugha ya Kifaransa kwamba, “ Kaka na dada, kwa Mungu na mbele za Mungu, tunaye mtetezi: Yesu Kristo, mwenye haki (taz. 1 Yh 2:1-2). Kwa maneno haya, Mtume Yohane anatusaidia kuelewa fumbo la wokovu.” Baba Mtakatifu aliendelea “katika udhaifu wetu, tukiwa tumelemewa na mzigo wa dhambi unaoashiria ubinadamu wetu, ambao hatuwezi kukumbatia ukamilifu wa maisha na furaha kwa nguvu zetu wenyewe pekee, tumefikiwa na Mungu mwenyewe kupitia Mwanae Yesu Kristo. Mtume anathibitisha, kuwa kama mwathirika wa kafara, alichukua uovu wa ubinadamu na ulimwengu, akaubeba  pamoja nasi na kwa ajili yetu, akapita ndani yake, akaubadilisha, na kutuweka huru milele.”

Yesu Kristo,mwenye haki,anayeombea wanadamu na Baba,anatupatanisha naye na sisi kwa sisi

Papa Leo XIV aliongeza, “Kristo ndiye kitovu chenye nguvu, ni  moyo wa imani yetu na ni kutokana na kiini hiki ambacho ningependa kuwaelekea ninyi, huku nikimsalimu kwa uchangamfu Mtukufu Mfalme Albert, Askofu Mkuu Dominique-Marie David, mapadre  na wanaume na wanawake watawa waliopo, kwa kuelezea  ninyi nyote furaha ya kuwa hapa na kushiriki safari yenu ya kikanisa.” Kwa kumtazama Kristo kama "mtetezi," kuhusiana na usomaji ambao tumeusikia hivi punde, ningependa kuwapa tafakari.” Papa aliendelea; Ya kwanza inahusu zawadi ya ushirika. Yesu Kristo, mwenye haki, anayeombea wanadamu na Baba, anatupatanisha naye na  sisi kwa sisi. Haji kutekeleza hukumu inayohukumu, bali kutoa huruma yake kwa kila mtu, ambayo hutakasa, huponya, hubadilisha, na kutufanya kuwa sehemu ya familia moja ya Mungu. Asili yake ya huruma na rehema humfanya kuwa "mtetezi" wa kuwatetea maskini na wenye dhambi, hakika si kuunga mkono uovu, bali kuwaweka huru kutoka kwa ukandamizaji na utumwa na kuwafanya watoto wa Mungu na kaka na dada miongoni mwao.

Papa na Jumuiya ya Wakatoliki wa Monaco
Papa na Jumuiya ya Wakatoliki wa Monaco   (@Vatican Media)

Ishara za Yesu hazizuiliwi na uponyaji wa kimwili au kiroho wa mtu

Sio bahati mbaya Papa Leo XIV alisisitiza “kwamba ishara za Yesu hazizuiliwi na uponyaji wa kimwili au kiroho wa mtu, lakini pia zinajumuisha kipengele muhimu cha kijamii na kisiasa: mtu aliyeponywa anaunganishwa tena, katika hadhi yake yote, katika jamii ya kibinadamu na kidini ambayo, mara nyingi kwa sababu ya ugonjwa au dhambi yake, alikuwa ametengwa. Ushirika huu ni ishara bora ya Kanisa, linaloitwa kuwa tafakari katika ulimwengu wa upendo wa Mungu, ambao hauoneshi upendeleo (taz. Mdo 10:34). Kwa maana hiyo, Papa Leo alipenda kusema kwamba “Kanisa lenu, hapa katika Ufalme wa Monaco, lina utajiri mkubwa: kuwa mahali, ambapo ukweli, kila mtu anakaribishwa na kupokelewa katika mchanganyiko huo wa kijamii na kiutamaduni ambao ni alama yenu.”

Katika Kanisa, tofauti kamwe haziwi sababu ya mgawanyiko bali wote wanakaribishwa kama watoto wa Mungu

Ufalme wa Monaco, kiukweli, ni serikali ndogo, linalokaliwa na mchanganyiko tofauti wa (Wamonegasque,) Wazawa wa MonaCo, Wafaransa, Waitaliano, na watu wa mataifa mengine mengi. Serikali ndogo, yenye watu wengi, ambayo kwa aina mbalimbali za asili zinajumuishwa na tofauti zingine za kijamii na kiuchumi. Katika Kanisa, tofauti hizo kamwe haziwi sababu ya mgawanyiko katika matabaka ya kijamii bali, kinyume chake, wote wanakaribishwa kama watu na watoto wa Mungu, na wote ni wapokeaji wa zawadi ya neema inayohimiza ushirika, udugu na upendo wa pande zote. Hii ndiyo zawadi inayotoka kwa Kristo, mwombezi wetu mbele za Baba. Hakika, sote tumebatizwa katika Yeye, na kwa hivyo, Mtakatifu Paulo anathibitisha, "hakuna Myahudi wala Mgiriki, hakuna mtumwa wala huru, hakuna mwanamume wala mwanamke; kwa maana ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu" (Gal 3:28).

Papa na Jumuiya ya Wakatoliki wa Monaco
Papa na Jumuiya ya Wakatoliki wa Monaco   (@Vatican Media)

Kukuza maendeleo fungamani ya ubinadamu, ambayo yanaheshimu hadhi yake na utambulisho wake

Hata hivyo, jambo la pili linaonekana kuwa muhimu kusisitiza: kutangazwa kwa Injili katika kutetea ubinadamu. Akitamani kwamba wote wapokee habari njema ya upendo wa Baba, Yesu anasimama kama "mtetezi," hasa katika kuwatetea wale wanaoonekana kutelekezwa na Mungu na kuhukumiwa kusahaulika na kutengwa, akiwa sauti na uso wa Mungu mwenye huruma ambaye "hutetea haki za wote wanaokandamizwa" (Zab 103:6). Papa Leo aliongeza kusema "Basi, kuhusu Kanisa, linaloitwa kuwa "mtetezi," yaani, kutetea ubinadamu: mtu mzima na wanadamu wote. Hii ni njia ya utambuzi muhimu na wa kinabii inayolenga kukuza "maendeleo fungamani ya ubinadamu, ambayo yanaheshimu hadhi yake na utambulisho wake halisi, pamoja na lengo lake kuu, ambalo linarejea fumbo la ushirika kamili na Mungu wa Utatu na miongoni mwetu" (Tume ya Kimataifa ya Kitaalimungu, Quo vadis, humanitas?, 22). Hii ndiyo huduma ya kwanza ambayo tangazo la Injili lazima itoe: kumwonesha mwanadamu na jamii hiyo, ili katika mwanga wa Kristo na Neno lake, waweze kugundua utambulisho wao wenyewe, maana ya maisha ya mwanadamu, thamani ya mahusiano na mshikamano wa kijamii, kusudi kuu la kuwepo, na hatima ya historia.

Mfumo wa sasa wa kiuchumi na kijamii ni wa haki na unaongozwa na mshikamano?

Katika suala hilo, Baba Mtakatifu alipenda kuwatia moyo kutoa huduma ya shauku na ukarimu katika uinjilishaji. Waangaze  Injili ya maisha, matumaini, na upendo; wapeleke nuru ya Injili kwa wote ili maisha ya kila mwanaume na mwanamke yaweze kulindwa na kukuzwa tangu kutungwa kwa mimba hadi kifo cha kawaida; kuchora ramani mpya za mwelekeo zinazoweza kuzuia shinikizo la usekula zinazohatarisha kumpeleka mwanadamu kwenye ubinafsi na kutegemea maisha ya kijamii katika uzalishaji wa utajiri. Papa alikazia kusema kuwa ni muhimu kwamba tangazo la Injili na aina za imani, zilizojikita sana katika utambulisho wao na jamii, zijilinde dhidi ya hatari ya kupunguzwa hadi kuwa tabia tu, hata iwe nzuri kiasi gani. Imani iliyo hai daima ni ya kinabii, inayoweza kuuliza maswali na kutoa uchochezi: je, kweli tunamtetea mwanadamu? Je, tunalinda heshima ya mtu katika kulinda maisha katika hatua zake zote? Je, mfumo wa sasa wa kiuchumi na kijamii ni wa haki na unaongozwa na mshikamano? Je, umejengewa maadili ya uwajibikaji, ambayo hutusaidia kupita zaidi ya "mantiki ya kubadilishana vitu sawa na faida kama lengo lenyewe" (Benedikto XIV,Waraka wa  Caritas in  Veritate, 38) ili kujenga jamii yenye usawa zaidi?

Papa amekutana na Jumuiya wa Wakatoliki huko Monaco
Papa amekutana na Jumuiya wa Wakatoliki huko Monaco   (@Vatican Media)

Imani inahitaji kutangazwa

Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alisema: “Wapendwa, tukimkazia macho Yesu Kristo, mtetezi wetu mbele ya Baba, huzaa imani yenye mizizi katika uhusiano wa kibinafsi naye, imani ambayo inakuwa shuhuda, inayoweza kubadilisha maisha na kuifufua jamii. Imani hii inahitaji kutangazwa kwa zana na lugha mpya, ikiwa ni pamoja na zile za kidijitali, na kila mtu lazima aielezwe na kufundishwa ndani yake kwa mwendelezo na ubunifu. Hii ni kweli hasa kwa wale wanaojifungulia kukutana na Mungu, kwa ajili ya wakatekumeni na wale wanaoanza tena, ambao ninawasihi mzingatie.” Mlinzi wao  Mtakatifu, bikira na shahidi Devota, awape msukumo kwa mfano wake, na Maria Mtakatifu  Sana na  Bikira Safi, awaombee na awaongoze katika njia kila wakati. Papa Leo alihitimisha.

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

28 Machi 2026, 12:18