Tafuta

Papa Leo XIV: Watu watakatifu wa Mungu wanashiriki utume wa Kinabii

“Sakramenti ya kwanza,ile inayotia muhuri utambulisho wetu milele na ambayo tunapaswa kujivunia kila wakati ni Ubatizo.Kanisa,kama ushirika wa waamini,ambao ni wazi unajumuisha wachungaji,haliwezi kukosea katika imani.Ni tafakari ya Papa Leo XIV katika Katekesi kwa mahujaji na waamini waliofika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Vatican Machi 18,kuhusu 'Kanisa kama watu wa Kikuhani na Kinabii' kwa mwendelezo wa mada ya Hati ya Mtaguso wa II wa Vatican:Lumen Gentium.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika katekesi ya Baba Mtakatifu Leo XIV kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Jumatano tarehe 18 Machi 2026 aliendelea na maada juu ya Hati ya Mtaguso wa II wa Vatican ya “Lumen gentium,” akuhusu Jumuiya ya Kikanisa kama watu wa kikuhani na Kinabii. Hii ni zawadi ambayo lazima kuishukuru lakini pia kuwa wawajibikaji. Alisisitiza  kwamba “kila Mbatizwa ni mhusika hai wa uinjilishaji kwa njia ya karama zilizotolewa na Bwana.”  

Papa Leo XIV wakati wa Katekesi
Papa Leo XIV wakati wa Katekesi   (@Vatican Media)

Kwa njia hiyo, Baba Mtakatifu  Leo XIV akianza tafakari hiyo alisema: “Ningependa kutafakari zaidi sura ya pili ya Katiba ya Mtaguso II  ya Lumen Gentium (LG), inayofafanua kuwa “Kanisa kama Watu wa Mungu.” Watu wa kimasiha (Lumen Gentium, 9), ambao hupokea kutoka kwa Kristo ushiriki katika kazi ya kikuhani, kinabii, na kifalme ambayo kupitia hiyo utume wake wa kuokoa unatimizwa. Mababa wa Mtaguso wanafundisha kwamba Bwana Yesu alianzisha, kupitia Agano jipya na la milele, ufalme wa kikuhani, kwa kuwaunda wanafunzi wake kuwa "kuhani wa kifalme" (1 Pt 2:9; rej. 1 Pet 2:5; Ufu 1:6). Ukuhani huu wa pamoja wa waaminifu umetolewa kwa Ubatizo, ambao unatuwezesha kumwabudu Mungu katika roho na kweli na "kukikiri hadharani imani tuliyopokea kutoka kwa Mungu kupitia Kanisa"(LG 11).

Sote tunafanya kuingia katika Kanisa kama watu walei

Papa aliendelea kusema kuwa “Zaidi ya hayo, kupitia sakramenti ya Kipaimara, wote waliobatizwa "wameunganishwa kikamilifu na Kanisa, wametajirishwa na nguvu maalum kutoka kwa Roho Mtakatifu, na kwa njia hiyo wanalazimika zaidi kueneza na kutetea imani kwa neno na tendo, kama mashuhuda wa kweli wa Kristo." Utakaso huu ndio msingi wa utume wa pamoja unaowaunganisha wahudumu waliowekwa wakfu na waamini walei. Katika suala hili, Papa Francisko alisema: "Kuwatazama watu wa Mungu ni kukumbuka kwamba sote tunafanya kuingia katika  Kanisa kama watu walei. Sakramenti ya kwanza, ile inayotia muhuri utambulisho wetu milele, na ambayo tunapaswa kujivunia kila wakati, ni Ubatizo.”

Papa akibariki wanandoa wapya
Papa akibariki wanandoa wapya   (@Vatican Media)

Watu Watakatifu wa Mungu pia wanashiriki katika utume wa kinabii wa Kristo

Kupitia hiyo na kwa upako wa Roho Mtakatifu, waamini "wametakaswa ili kuunda nyumba ya kiroho na ukuhani mtakatifu" (LG,10), Baba Mtakatifu aliongeza, “ili sote tuunde Watu watakatifu na waamini wa Mungu"(Barua kwa Rais wa Tume ya Kipapa ya Amerika Kusini, 29 Machi 2016). Utekelezaji wa ukuhani wa kifalme hutokea kwa njia nyingi, zote zikilenga utakaso wetu, kwanza kabisa kwa kushiriki kwa sadaka ya misa. Kupitia sala, kujinyima na upendo hai, hivyo tunashuhudia maisha yaliyofanywa upya kwa neema ya Mungu (taz. LG, 10). Kama Mtaguso unavyofupisha, "tabia takatifu na muundo kiungo cha jumuiya ya kikuhani huletwa kupitia sakramenti na fadhila"(LG, 11).

Mababa wa Mtaguso kisha, wanafundisha kwamba Watu Watakatifu wa Mungu pia wanashiriki katika utume wa kinabii wa Kristo (taz. LG, 12). Katika muktadha huo, Mtaguso unaanzisha mada muhimu ya maana ya imani na makubaliano ya waamini. Papa Leo XIV aliendelea kusisitiza kuwa: “Tume ya Mafundisho ya Mtaguso ilibainisha kabisa kwamba sensus fidei yaani maana ya imani  hii ni kama kitovu cha Kanisa lote, kutokana na hilo, katika imani yake, inatambua ufunuo uliotolewa, kutofautisha kati ya kweli na uongo katika masuala ya imani, na wakati huo huo huipenya kwa undani zaidi na kuitumia kikamilifu zaidi maishani"(taz. Acta Synodalia, III/1, 199). Kwa hivyo, hisia ya imani ni ya waamini binafsi, si kwa haki yao wenyewe, bali kama washiriki wa Watu wa Mungu kwa ujumla. Lumen Gentium inazingatia kipengele hiki cha mwisho na inakihusisha na kutokukosa kwa Kanisa, ambapo inaingia kwa kuhudumia kwa Baba Mtakatifu wa Roma.

Papa na kundi la Maaskari
Papa na kundi la Maaskari   (@Vatican Media)

Kanisa,kama ushirika wa waamini,ambao ni wazi linajumuisha wachungaji

Baba Mtakatifu Leo XIV  aliendelea kukazia kuwa, "Ukamilifu wa waamini, waliopakwa mafuta Matakatifu (taz. 1 Yh 2:20, 27), hauwezi kukosea katika mambo ya imani. Sifa hii maalum hudhihirishwa kupitia utambuzi usio wa kawaida wa imani ya watu wote, wakati, kuanzia maaskofu hadi waamini walei, wanaelezea makubaliano yao ya ulimwengu katika mambo ya imani na maadili"(Lumen Gentium, 12). Kwa hivyo, Kanisa, kama ushirika wa waamini, ambao ni wazi unajumuisha wachungaji, haliwezi kukosea katika imani: Kiungo cha sifa hii, kilichojengwa juu ya upako wa Roho Mtakatifu, ni utambuzi usio wa kawaida wa imani ya watu wote wa Mungu, ambao unadhihirishwa katika makubaliano ya waamini. Kutokana na umoja huo, ambao Majisterio ya Kanisa inalinda, inafuata kwamba kila mtu aliyebatizwa ni mhusika hai wa uinjilishaji, aliyeitwa kutoa ushuhuda thabiti kwa Kristo kulingana na kipaji cha unabii ambacho Bwana huingiza katika Kanisa lake lote.

Viungo vya kikanisa hutoa mfano mzuri wa aina na kuzaa matunda

Roho Mtakatifu, anayetujia kutoka kwa Yesu Mfufuka, hutoa "miongoni mwa waamini wa kila daraja neema maalum, akiwapatia  vifaa na kuwaandaa kufanya kazi na huduma mbalimbali muhimu kwa ajili ya upyaisho na upanuzi mkubwa wa Kanisa"(Lumen Gentium, 12). Onesho la kipekee la uhai huu wa karama hutolewa na maisha yaliyowekwa wakfu, ambayo huchanua na kustawi kila mara kupitia nguvu ya neema. Viungo vya kikanisa pia hutoa mfano mzuri wa aina na kuzaa matunda ya kiroho kwa ajili ya kuwajenga Watu wa Mungu. Baba Mtakatifu Leo XIV kwa kuhitimisha alisema kuwa“   “Tuamshe ndani yetu ufahamu na shukrani kwa kupokea zawadi ya kuwa sehemu ya Watu wa Mungu; na pia jukumu ambalo hili linahusisha,” alihitimisha.

Papa akibariki makundi ya wanahija
Papa akibariki makundi ya wanahija   (@Vatican Media)
Papa Katekesi Machi 19

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

18 Machi 2026, 12:25