2026.03.20 Jukwaa la Greenaccord 2026 huko treviso, Italia. 2026.03.20 Jukwaa la Greenaccord 2026 huko treviso, Italia. 

Papa Leo XIV:Jukumu la kiikolojia lisiwe takwimu za kiufundi

Katika ujumbe wa Papa Leo XIV kwa washiriki wa Jukwaa la 17 la Kimataifa la Greenaccord kuhusu mada:"Kujenga Mustakabali Pamoja-Ubinadamu Mpya Wenye Kiu ya Mustakabali,"huko Treviso alibainisha kuwa Jukumu kubwa zaidi la ikolojia linahitajika kwa ajili ya mustakabali bora.Kwa Katibu Mkuu wa Vatican,alifafanua Wimbo wa Mtakatifu Francis kuwa:"Viumbe ni diplomasia ya tamaduni."

Marina Tomarro - Treviso na Angella Rwezaula - Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV aliwatumia ujumbe washiriki wa Jukwaa la Kimataifa la Greenaccord katika telegramu iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa Vatican, Kardinali Pietro Parolin, akinukuu barua yake ya kitume ya( Disegnare nuove mappe di speranza)-Kuchora Ramani Mpya za Matumaini, ya Oktoba 2025 kwamba:"Uwajibikaji wa ikolojia hauzuiliwi na data ya kiufundi pekee. Ni muhimu lakini haitoshi. Tunahitaji elimu inayohusisha akili, moyo, na mikono. Tabia mpya, mitindo ya jamii, na mazoea mema." Kwa njia hiyo Papa anaandika kuwa "Kwa kushughulikia migogoro ya sasa pamoja, tunaweza kukuza mazingira ya kijamii yenye heshima na jumuishi, ili kuhakikisha mustakabali bora kwa vizazi vijavyo."

Kard.Parolin: Kuvuka Kizingiti cha Kulinda Uumbaji

Mkutano huo,ambao umefanyika Treviso kuanzia tarehe----, pia unahudhuriwa na Kardinali Beniamino Stella, Mwenyekiti Mstaafu wa Baraza la Kipapa la Makleri ambaye wakati huo, alisoma hotuba ya Kardinali Parolin kuhusu maadhimisho ya miaka 800 ya Wimbo wa sifa ya Viumbe na maadhimisho ya miaka 800 ya Kifo cha Mtakatifu Francis wa Assisi. "Ikiwa kujenga mustakabali pamoja ndio lengo letu lililotangazwa,"Kardinali Parolin, akinukuu mada ya Jukwaa, alielezea kuwa "inahitaji, kwanza kabisa, 'kuvuka kizingiti' na 'kuingia katika nyumba mpya': hali ambazo bila hizo ulinzi wa uumbaji unahatarisha kubadilika-badilika kati ya itikadi na ufundi, kati ya msisitizo wa kihisia na ubaridi wa utaratibu, kati ya usemi wa kujenga na usimamizi usio na roho." Na akikumbuka miaka mia nane ya Wimbo wa Viumbe, Kardinali anasisitiza kwamba maadhimisho haya si maadhimisho ya kuhifadhiwa katika kumbukumbu, bali ni tukio zuri la kugundua upya neno, linaloweza kuzalisha ujumuishaji na ushirika.

"Wimbo hauonyeshi  hisia za asili tu," aliandika Katibu Mkuu wa Vatican, bali, "unawasilisha maneno ya kibinadamu yanayosababisha mkao wa kiroho na kiakili ambao, kwa kuondoa ubinadamu kutoka kwa uthibitisho wa kibinafsi na wa ulaghai, huiweka katika wito wa kudumu wa malezi."


Uzoefu wa Wafransiskani na Akili fungamani

Kardinali Parolin alisisitiza kwamba kuita kile ambacho mtu hana "kaka" na "dada" ni kitendo cha "malezi" ya hali ya juu, na inamaanisha kutambua kwamba ukweli kwanza kabisa ni uhusiano na kwamba kuwa, kabla ya kuwa rasilimali ya kutumiwa na kuliwa, ni zawadi ya kutambuliwa na kukaribishwa. "Kuanzia hapa, kipimo halisi cha kifalsafa cha Wafransiskani kinatokea,"alisisitiza Kardinali Parolin.

Miongoni mwa mada zilizogusiwa, akili unde haiwezi kukosekana, ikionekana kama mtihani wa ukomavu wetu wa anthropolojia. Kwa mara nyingine tena, Kardinali Parolin alirejea uzoefu wa Wafransiskani, ambao unasukuma kuelekea akili kamili. "Si marekebisho yanayotafutwa kwa haraka," alielezea, "bali ni mwelekeo unaoweza kuathiri uchaguzi wa awali, wa kupanga, mifumo ya utawala, uwazi, ufuatiliaji wa maamuzi, na uwajibikaji mzuri wa wale walio na zana na data."

Wimbo wa Francis: "Diplomasia ya Tamaduni"

Akifikia moyo wa Wimbo, Kardinali Parolin aliakisi  jinsi unavyojifunua kama kiroho cha mazungumzo na, kwa hivyo, kama "diplomasia ya tamaduni" kwa maana ya juu zaidi. Kwa sababu kiini cha wakati wetu si tu shinikizo kwenye mifumo ikolojia, bali pia kupoteza uaminifu kati ya watu, vizazi, na jamii. Ushirikiano wa pande zote," alielezea katika hotuba yake iliyosomwa na Kardinali Stella, "sio 'ubaba wa walioshiba': ni muunganisho ambapo hakuna mtu anayeokolewa peke yake. Uelewa wa pande zote si 'ujasusi' au 'uchochezi wa kuona': ni mbinu na kigezo, kwa sababu huondoa dhana potofu zinazotumikia ubora wa utambulisho na kuzuia wingi kuwa mfereji wa msuguano wa kudumu.

“Kulinda na Kujenga Amani na Haki

Maneno ya Wimbo pia yanatafuta kuonyesha kwamba amani na dunia na amani miongoni mwa wanadamu ni ahadi moja. "Pale ambapo uumbaji unajeruhiwa, jamii huvunjika; pale ambapo heshima inadhalilishwa, asili inakuwa mawindo; pale ambapo mahusiano yanaharibika, teknolojia inakuwa nguvu inayotenganisha." Na ni neno "linda" ambalo Mwaka wa Jubilei wa Wafransiskani katika Wimbo wa Sifa kwa Viumbe, Jukwaa hilo lilikabidhi. Kulinda uumbaji kama kitendo cha haki; kulinda wengine katika hadhi yao isiyoweza kuondolewa; kulinda sayansi ili ibaki kuwa hekima; kulinda teknolojia ili ibaki kuwa chombo; kulinda mustakabali kama muungano kati ya vizazi.

"Ikiwa Safari ya Mtakatifu wa Assisi inatukumbusha kwamba maisha ya mwanadamu yanafikia ukamilifu wake yanapotolewa," Kardinali Parolin anahitimisha, na ikiwa Wimbo unatufundisha kuuita ulimwengu kama udugu na si kama mali au mawindo, basi 'kujenga mustakabali pamoja' hakuwezi kuwa lengo la utendaji lililokabidhiwa kuchukua hatua: lazima iwe njia ya maisha kwa roho na kwa Taasisi, diplomasia ya amani inayoanza na lugha, inajaribiwa kwa ushirikiano, na inathibitishwa katika ulinzi wa walio hatarini."

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

 

20 Machi 2026, 17:06