Papa Leo XIV:Tuombe tuone mateso ya wengine na majeraha ya Ulimwengu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika Injili ya Dominika ya IV ya Kwaresima inasimulia juu ya uponyaji wa mwanaume kipofu tangu kuzaliwa(Yh 9,1-14). Kwa njia ya ishara ya tukio hilo, Mwinjili Yohane anatueleza Huduma ya wokovu. Wakati tulikuwa katika giza, wakati ubinadamu ulikuwa ukitembea gizani (Is 9,1), Mungu alimtuma Mwanae kama nuru ya Ulimwengu, ili kuwafungua macho vipofu na kutuangazia maisha yetu. Ndivyo Baba Mtakatifu Leo XIV alivyoanza tafakari yake kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana, Dominika tarehe 15 Machi 2026, kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican.
Na sisi ni vipofu
Papa Leo XIV aliendelea kusema kuwa, Manabii walikuwa wametangaza kuwa Masiha angewafungua macho vipofu (Is 29,18; 35,5; Za 146,8). Yesu mwenyewe anathibitisha utume wake akionesha kwamba, vipofu wanapata kuona(Mt 11,4); na anajiwakilisha akisema kuwa: “ Mimi ni nuru ya Ulimwengu”(Yh 8,12). Kwa hakika Papa aliongeza “ tunaweza kusema kuwa sisi ni “vipofu tangu kuzaliwa,” kwa sababu sisi peke yetu hatuwezi kuona kwa kina fumbo la maisha. Kwa hiyo Mungu alifanyika mwili katika Yesu, ili tope la ubinadamu wetu liweze kuchanganywa na pumzi ya neema yake, tuweze kupokea nuru mpya, wenye uwezo wa kujiona hatimaye sisi wenyewe, wengine na Mungu katika ukweli.
Kuwasiliana na Kristo macho yanafunguka
Papa Leo XIV aidha alisisitiza kwamba inashangaza kuona kwamba katika karne nyingi limeenea na lipo bado sasa, kwa mujibu wa imani kwamba ingekuwa aina ya “kuruka karibu giza,” wazo la kukataa, hivyo kwamba kuwa na imani kungemaanisha kuamini "kipofu." Kinyume chake Injili inatuambia kuwa, kuwasiliana na Kristo, macho yanafunguka, kiasi kwamba mamlaka ya kidini, yanaomba kwa msisitizo kipofu aliyepona: “Macho yako yalifumbuliwaje?(Yh 9,10) na tena Alikufumbua macho jinsi gani?
Kupoteza mtazamo kutoka duniani
Kwa njia hiyo Papa alisisitiza tena kuwa“ hata sisi, kwa kuponeshwa na upendo wa Kristo, tunaalikwa kuishi ukristo wa “macho yaliyofunguliwa.” Imani siyo tendo la kipofu, au kujiuzulu kwa dini, mfumo kwa namna ya uhakika wa kidini ambao unafanya kupoteza mtazamo kutoka duniani. Kinyume chake, imani inatusaidia kutazama “kutoka katika mtazamo wa Yesu, kwa macho yake: ni ushiriki wa mtindo wake wa kutazama,(LG,18) na hivyo tumuombe tufungue macho kama alivyokuwa anafanya Yeye, hasa juu ya mateso ya wengine na juu ya majeraha ya Ulimwengu.”
Umakini wa kinabii
Kwa namna ya pekee leo hii, mbele ya maswali ya moyo wa Binadamu na majanga ya hali ya ukosefu wa haki, ya vurugu , ya mateso ambayo yanakabili wakati wetu, Baba Mtakatifu alisema, kuna uhitaji wa imani inayonesha, umakini na kinabii, ambayo ifungue macho juu ya giza la ulimwengu na kupeleka nuru ya Injili kwa njia ya jitihada ya amani, ya haki na ya mshikamano. Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV alisema”Tuombe Bikira Maria ambaye atuombee sisi ili mwanga wa Kristo ufungue macho ya moyo wetu na tunaweza kutoa ushuhuda wake kwa urahisi na ujasiri.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.
