Tafuta

Baba Mtakatifu Leo XIV ametumia fursa hii, kutoa wito kwa pande zinazohusika kuchukua jukumu la kimaadili, ili kusitisha wimbi hili la vurugu za kivita. Baba Mtakatifu Leo XIV ametumia fursa hii, kutoa wito kwa pande zinazohusika kuchukua jukumu la kimaadili, ili kusitisha wimbi hili la vurugu za kivita.  (ANSA)

Papa Leo XIV: Sitisheni Vita Iran! Rejeeni Kwenye Diplomasia

Baba Mtakatifu Leo XIV ametumia fursa hii, kutoa wito kwa pande zinazohusika kuchukua jukumu la kimaadili, ili kusitisha wimbi hili la vurugu za kivita na kuhakikisha kwamba, diplomasia inachukua mkondo wake, kwa kukuza wema wa watu wanaotamani kuishi katika mazingira ya amani inayosimikwa katika msingi wa haki. Vuguvugu la vita kati ya Marekani, Israeli na Irani tayari imekwisha onesha madhara makubwa katika maisha ya watu huko Mashariki ya Kati.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Kifo cha Kiongozi mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, kimetangazwa rasmi na vyombo vya habari vya serikali mapema Dominika tarehe Mosi Machi 2026. Taarifa hiyo ilithibitishwa na televisheni ya taifa pamoja na Shirika la Habari la IRNA. Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 86 aliuawa katika mashambulizi makubwa ya anga yaliyoendeshwa na Marekani na Israel. Taarifa zaidi zinabainisha kwamba, katika shambulio hilo, Binti yake, Mkwe na Mjukuu wake wamefariki dunia katika shambulio la makombora 30.

Papa Leo XIV amezitaka pande zinazohusika, kusitisha mara moja vita
Papa Leo XIV amezitaka pande zinazohusika, kusitisha mara moja vita   (AFP or licensors)

Kamanda mkuu wa Majeshi ya Iran naye amepoteza maisha katika shambulio hilo. Marekani na Israel zinasema lengo la mashambulio hayo ni kuharibu kabisa miundo mbinu ya Iran ya kutengeneza silaha za maangamizi, lakini pia kubadilisha uongozi wa nchi hiyo! Iran pia imeendelea kujibu mashambulizi kwa nchi jirani za: Ghuba, Qatar, Israel, Bahrain, Kuwait, Iraq, Oman na Saudi Arabia. Kimsingi hali ni tete huko Mashariki ya Kati na huko nchini Iran. Ni katika muktadha wa vuguvugu la vita huko Mashariki ya Kati, Baba Mtakatifu Leo XIV wakati wa Sala ya Malaika wa Bwana ameonesha wasiwasi wake mkubwa kwa Jumuiya ya Kimataifa kukabiliana na maafa makubwa na hivyo watu wengi kupoteza maisha.

Maafa makubwa yameendelea kujitokeza katika vita: Iran, USA na Israeli
Maafa makubwa yameendelea kujitokeza katika vita: Iran, USA na Israeli   (AFP or licensors)

Baba Mtakatifu Leo XIV ametumia fursa hii, kutoa wito kwa pande zinazohusika kuchukua jukumu la kimaadili, ili kusitisha wimbi hili la vurugu za kivita na kuhakikisha kwamba, diplomasia inachukua mkondo wake, kwa kukuza wema wa watu wa Mungu wanaotamani kuishi katika mazingira ya amani inayosimikwa katika msingi wa haki. Baba Mtakatifu anawaalika waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema kuendelea kusali kwa ajili ya kuombea amani sehemu mbalimbali za dunia.

Vita ina madhara makubwa katika maisha ya watu
Vita ina madhara makubwa katika maisha ya watu   (AFP or licensors)

Wakati huo huo, Baba Mtakatifu Leo XIV amesikitishwa na habari za mapigano kati ya Pakistan na Afghanistan na kwamba, anawataka viongozi wa pande hizi mbili kurejea tena kwenye majadiliano yanayosimikwa katika ukweli na uwazi; ustawi na maendeleo ya wengi. Baba Mtakatifu anakumbusha kwamba, amani ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu na ndiyo pekee inaweza kuponya majeraha kati ya watu.

Vita Iran

 

01 Machi 2026, 14:57