Tafuta

Moshi na miali ya moto iliyoongeza kufuatia shambulio la Israel karibu na kambi ya mahema inayowahifadhi Wapalestina waliokimbia makazi yao huko Deir al-Balah. Moshi na miali ya moto iliyoongeza kufuatia shambulio la Israel karibu na kambi ya mahema inayowahifadhi Wapalestina waliokimbia makazi yao huko Deir al-Balah. 

Papa Leo XIV:njia za kuelekea amani lazima zifunguliwe Mashariki ya Kati

Kabla ya Sala ya Malaika Mkuu,Papa Leo XIV alikumbusha juu ya ukosefu wa ibada za kiutamaduni za Juma Takatifu katika Nchi za Mashariki ya Kati.Alionesha ukaribu wake na sala zake kwa wale wanaoteseka.Ni mateso ambayo yanapinga dhamiri ya kila mtu. Tusali sala yetu kwa Mfalme wa Amani ili kuwasaidia watu waliojeruhiwa na vita.Wazo ni kwa wahamiaji waliokufa baharini karibu na pwani ya Ugiriki.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV.  mara baada ya Misa Takatifu, na kabla ya Sala ya Malaika wa Bwana katika Dominika ya Matawi tarehe 29 Machi 2026, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, uliojaa waamini kutoka pande zote za Dunia, alianza kusema kuwa "Mwanzoni mwa Juma Takatifu, tuko karibu zaidi na Wakristo wa Mashariki ya Kati katika maombi, ambao wanateseka kutokana na matokeo ya mgogoro mbaya na katika visa vingi hawawezi kupata uzoefu kamili wa ibada za siku hizi takatifu.”

Misa ya Matawi Machi 29
Misa ya Matawi Machi 29   (@Vatican Media)

Hatuwezi kuwasahau wanaoshiriki mateso

Papa alisema kuwa “Hata Kanisa linapotafakari fumbo la Mateso ya Bwana, hatuwezi kuwasahau wale ambao leo wanashiriki kweli katika mateso yake. Jaribio lao linapinga dhamiri ya wote. Tunamwomba Mfalme wa Amani awasaidie watu waliojeruhiwa na vita na njia zilizo wazi za upatanisho na amani.

Papa awakabidhi kwa Bwana wahanga wa vita

Baba Mtakatifu Leo XIV aidha alisema “Pia nataka kuwakabidhi kwa Bwana mabaharia ambao ni wahanga wa vita. Ninawaombea marehemu, waliojeruhiwa, na familia zao. Dunia, anga, na bahari vimeumbwa kwa ajili ya uzima na amani. Na tunawaombea wahamiaji wote waliokufa baharini, hasa wale waliopoteza maisha yao katika siku za hivi karibuni nje ya kisiwa cha Crete,” huko Ugiriki.

Misa ya Matawi
Misa ya Matawi   (@VATICAN MEDIA)

Salamu kwa mahujaji wote na sala kwa Mama Maria

Papa alipenda pia kuwasalimia na kuwashukuru wote, kuanzia na warumi, mahujaji ambao wameshiriki katika sherehe hiyo. Kwa pamoja”, kuwaomba kumgeukia  Bikira Maria, huku “tukimkabidhi maombi yetu yote kwa maombezi yake.” Papa aliongeza kusema “Hebu tujiruhusu kuongozwa naye katika siku hizi takatifu ili kumfuata Yesu, Mwokozi wetu, kwa imani na upendo.”

BAADA YA MISA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

29 Machi 2026, 16:08