Tafuta

Papa Leo XIV:Mungu anakataa vita,hakuna kumtumia kuhalalisha vita

Baba Mtakatifu aliongoza Ibada ya Misa Takatifu katika Uwanja wa Mtakatifu Petro,Mama Kanisa akiadhimisha Dominika ya Matawi,kuanza Juma Kuu la Mateso,Kifo na Ufufuko wa Bwana.Papa alisisitiza 'upole wa Yesu,unapingana na ukatili na unyanyasaji wa wanadamu:Hakujihami,hakujitetea.Mungu hasikilizi maombi ya wanaopigana vita na ambao mikono yao inamwaga damu.Mungu hukataa vurugu kila wakati.Huyu ndiye Mungu wetu:Yesu,Mfalme wa Amani.'

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Uwanja wa Mtakatifu Petro ulijaa waamini na mahujaji kutoka sehemu mbali mbali kwa ajili ya Misa ya Dominika ya  Matawi, tarehe 29 Machi 2026, ikiwa inaashilia kuingia katika Juma Kuu Takatifu ambalo linatupeleka katika Mateso, kifo na Ufufuko wa Bwana. Awali ya yote, maandamao yalifanyika kuanzia katikati ya Uwanja huo, wawakilishi wa waamini watu wa Mungu, mapadre, maaskofu, Makardinali na Papa Leo XIV na wahudumu wake wakiwa wameshikilia matawi ya mitende hadi kwenye Jukwa lenye Altare mbele ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro.

Kabla ya kuanza maandamano
Kabla ya kuanza maandamano   (@Vatican Media)

Baada ya Masomo yote na Injili ya Mateso, Baba Mtakatifu Leo XIV alianza kusema kuwa “Wakati Yesu anapitia njia ya Msalaba, tunajiweka nyuma yake kwa kufuata hatua zake. Na tutembee na yeye, kwa kutafakari mateso yake kwa ajili ya ubinadamu, moyo wake unavunjika, maisha yake yanayo kuwa zawadi ya upendo.” Tutazame Yesu ambaye anajiwakilisha kama Mfalme wa amani, wakati karibu Naye wako wanaandaa vita. Yeye ambaye anabaki na msimamo katika uyenyekevu, wakati wengine wanawasi wasi katika vurugu.

Misa ya Matawi, Vatican
Misa ya Matawi, Vatican   (@VATICAN MEDIA)

Tumtazame Yesu anayejiwakilisha kama Mfalme

Yeye anayejitoa kama bembelezo kwa ajili ya ubinadamu, wakati wengine wanamwelekea upanga na miundu. Yeye ambaye ni mwanga wa Ulimwengu, wakati giza liko linafunika dunia. Yeye ambaye alikuja kuleta maisha, wakati wakitimiza mipango ya kumhukumu kifo.  Kama Mfalme wa Amani, Yesu anataka kupatanisha ulimwengu katika mkumbatio wa Baba na kuangusha kila aina ya kuta ambazo zinatutenganisha na Mungu na jirani, kwa sababu Yeye ni amani yetu(Ef 2,14). Kama Mfalame wa Amani, anaingia Yerusalemu, akiwa amepanda Punda, na siyo farasi, kwa kutimiza unabii ambao ulikuwa unatabiri kushangilia Masiha: “Tazama, mfalme wako anakuja kwako; Ni mwenye haki, naye ana wokovu; Ni mnyenyekevu, amepanda punda, Naam, mwana-punda, mtoto wa punda. Na gari la vita nitaliondoa liwe mbali na Efraimu, na farasi awe mbali na Yerusalemu, na upinde wa vita utaondolewa mbali; naye atawahubiri mataifa yote habari za amani;(Zak 9,9-10).”

Misa ya Matawi mjini Vatican
Misa ya Matawi mjini Vatican   (@VATICAN MEDIA)

Waushikao upanga wataangamia kwa upanga

Kama Mfalme wa amani wakati mmoja wa mitume wake alipochomoa upanga kwa ajili ya kumlinda na akampiga mtumwa wa Kuhani Mkuu, akamkata sikio, Yeye kwa haraka alimsimamisha akisema: “Rudisha upanga wako mahali pake, maana wote waushikao upanga, wataangamia kwa upanga(Mt 26,52). Kama Mfalme wa Amani, huku akiwa ametwikwa mateso yetu na kuchomwa kwa ajili ya dhambi zetu, "hakufungua kinywa chake; alikuwa kama mwana-kondoo kwenda kuchinjwa, na kama kondoo aliyekimya mbele ya wakata manyoya wake" (Isaya 53:7). Hakujivika silaha, hakujitetea, hakupigana vita yoyote. Alifunua uso mpole wa Mungu, ambaye hukataa vurugu kila wakati, na badala ya kujiokoa, alijiruhusu kupigiliwa misumari msalabani, ili kukumbatia misalaba yote iliyopandwa kila wakati na mahali katika historia ya mwanadamu.

Mtaomba mara nyingi sitasikia, mikono yenu imejaa damu

Baba Mtakatifu Leo alisisitiza kwamba, huyu ndiye Mungu wetu: Yesu, Mfalme wa Amani. Mungu anayekataa vita, ambaye hakuna mtu anayeweza kumtumia kuhalalisha vita, ambaye hasikilizi maombi ya wale wanaopigana vita na kuvikataa, akisema: "Ingawa mtaomba mara nyingi, sitasikia; mikono yenu imejaa damu" (Isaya 1:15). Kwa kumtazama Yeye, aliyesulubiwa kwa ajili yetu, tunaona wasulubiwa wa ubinadamu. Katika majeraha Yake, tunaona majeraha ya wanawake na wanaume wengi wa leo. Katika kilio Chake cha mwisho kwa Baba, tunasikia vilio vya waliovunjika moyo, wasio na matumaini, wagonjwa, wapweke. Na zaidi ya yote, tunasikia kilio cha maumivu ya wale wote wanaokandamizwa na vurugu na waathiriwa wote wa vita.

Misa ya Matawi
Misa ya Matawi   (@VATICAN MEDIA)

Sala kwa Mama Maria:machozi ya waathiriwa wote wa vurugu yatakauka

Kristo, Mfalme wa Amani, analia tena kutoka msalabani Mwake: Mungu ni upendo! Kuwa na huruma! Weka silaha zako chini, kumbuka kwamba ninyi ni ndugu! Kwa maneno ya Mtumishi wa Mungu, Askofu Tonino Bello, Papa leo XIV alipenda kumkabidhi kilio hiki Maria Mtakatifu sana ambaye anasimama chini ya msalaba wa Mwanae na pia analia miguuni pa wale waliosulubiwa leo: “Maria Mtakatifu, mwanamke wa siku ya tatu, utupe uhakika kwamba, licha ya kila kitu, kifo hakitatushika tena. Kwamba dhuluma za watu zina siku zilizohesabiwa. Kwamba mwanga wa vita uko unafifia hadi giza. Kwamba mateso ya maskini yamefikia pumzi zao za mwisho. […] Na kwamba, hatimaye, machozi ya waathiriwa wote wa vurugu na maumivu yatakauka hivi karibuni, kama baridi kali na jua la masika. (Sala kutoka Maria, mwanamke wa siku zetu).

Misa ya Matawi
Misa ya Matawi   (@Vatican Media)

Na katika sala ya Ulimwengu wote zilizosomwa kwa lugha mbali mbali

Kwa Kifaransa: Kwa ajili ya Kanisa la Mungu Mchumba na Mfuasi wa Kristo chini ya Msalaba: Litambue kuweka matumaini ya kiinjili miongoni mwa waliokata tamaa

Kwa lugha ya Kiswahili: Kwa Wakristo wanaoteswa, wanaoishi unyenyekevu wa Kristo Yesu, katika mateso yake: wasikatishwe tamaa, na majaribu, bali waendelee kutumaini kwa imani katika ahadi ya Baba.

Kwa Lugha ya Kireno: kwa ajili ya watu wote, kwa kuunanishwa na Msalaba mmoja wa Kristo: wawe ishara za amani na za maridhiano kwa kushinda ubinafsi na utashi wa kujitosheleza.

Kwa lugha ya Kitagalog: Kwa  walio katika mateso, umaskini, kwa kuungana na uchungu wa Kristo Msulibiwa: waweza kufanya uzoefu katika msaada wa wote wa uwepo na faraja ya Baba.

Misa ya Matawi
Misa ya Matawi   (@Vatican Media)

Kwa kijerumani: Kwa ajili ya Mkusanyiko wetu wa kiliturujia, uliojaa fumbo la Msalaba na ufufuko wa Kristo: waamini katika Jina moja ambalo limewekwa ahadi ya wokovu.

Misa ya Matawi
Misa ya Matawi   (@Vatican Media)
MAHUBIRI YA PAPA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

29 Machi 2026, 13:35