Tafuta

Papa Leo XIV:Mungu hatuachi katika majaribu,humsaidia mtu dhaifu na mwenye huzuni!

Vita ni matunda ya ibada ya miungu.Ni hesabu ngapi zinazofanywa ili kuwaua wasio na hatia!Sisi ni mashuhuda wa harakati mbili zinazopingana:ufunuo wa Mungu,anayeonesha uso wake kama Bwana na mwokozi mwenye nguvu zote.Pili,matendo yaliyofichwa ya mamlaka yenye nguvu,tayari kuua bila aibu."Ni katika mahubiri ya Papa Leo XIV,wakati wa Misa Takatifu katika Uwanja wa Mchezo wa Louis II,ikiwa ni hatua ya mwisho ya Ziara ya Kitume katika Ufalme wa Monaco,Machi 28.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ni hesabu ngapi zinazofanywa duniani ili kuwaua wasio na hatia; ni sababu ngapi za uongo zinazodaiwa kuwaondoa. Kwa hivyo sisi ni mashuhuda wa harakati mbili zinazopingana: kwa upande mmoja, ufunuo wa Mungu, ambaye anaonesha uso wake kama Bwana na Mwokozi mwenye nguvu zote; kwa upande mwingine, vitendo vilivyofichwa vya mamlaka yenye nguvu, tayari kuua bila aibu. Je, si hivi ndivyo vinavyotokea leo hii? Kwenye makutano yao kuna ishara ya Yesu: kutoa uhai.” Ni katika mahubiri yenye nguvu wakati wa Misa Takatifu iliyoadhimishwa, ikifunga siku kali ya Ziara ya Baba Mtakatifu Leo XIV katika Ufalme wa Monaco, tarehe 28 Machi 2026.

Misa ya Papa huko Monaco
Misa ya Papa huko Monaco   (@Vatican Media)

Uwanja wa Louis II ukiwa unaangazwa na jua la jioni, kwa waamini waliokuwa wamekaa humo, Papa Leo XIV alianza mahubiri:"Kaka na dada wapendwa, Injili ambayo tumeisikia (Yh 11:45-57) inaripoti hukumu kali dhidi ya Yesu: inatuambia kuhusu siku ambayo washiriki katika baraza "tangu siku ile walifanya shauri la kumwua, (Yh 11, 53). Kwa nini hili linamtokea? Kwa sababu alimfufua Lazaro kutoka katika wafu; kwa sababu alimrudishia rafiki yake uhai, ambaye alilia mbele ya kaburi lake, akishiriki katika huzuni ya Martha na Maria. Yesu mwenyewe, ambaye alikuja ulimwenguni kutukomboa kutoka katika hukumu ya kifo, amehukumiwa kifo. Hili si suala la hatima, bali ni wosia sahihi na unaofikiriwa.”  Tukimwacha hivi, watu wote watamwamini; na Warumi watakuja, watatuondolea mahali petu na taifa letu.

Misa ya Papa huko Monaco
Misa ya Papa huko Monaco   (@Vatican Media)

Uamuzi wa Kayafa na Baraza unatokana na hesabu ya kisiasa, yenye mizizi katika hofu: ikiwa Yesu ataendelea kuhamasisha tumaini, akibadilisha maumivu ya watu kuwa furaha, "Warumi watakuja" na kuharibu nchi (Rej Yh 11,48). Badala ya kumtambua Mnazareti kama Masiha, Kristo aliyesubiriwa kwa muda mrefu, viongozi wa kidini wanamwona kama tishio. Mtazamo wao umepotoshwa, kiasi kwamba ni wataalamu wa Sheria wenyewe wanaouvunja. Kwa kusahau ahadi ya Mungu kwa watu wake, wanataka kuwaua wasio na hatia, kwa sababu nyuma ya hofu yao kuna tamaa ya madaraka. Lakini watu wakisahau Sheria inayowaamuru wasiue, Mungu hasahau ahadi inayoandaa ulimwengu kwa ajili ya wokovu. Uongozi wake hufanya uamuzi huo wa mauaji kuwa njia ya kuonesha nia kuu ya upendo: hata kama ni mbaya kiasi gani, Kayafa "alitabiri kwamba Yesu angekufa kwa ajili ya taifa (Yh 11. 51).

Misa ya Baba Mtakatifu huko Monaco
Misa ya Baba Mtakatifu huko Monaco   (@Vatican Media)

Sisi ni mashuhda wa harakati mbili zinazopingana

Kwa hivyo sisi ni mashuhuda wa harakati mbili zinazopingana: kwa upande mmoja, ufunuo wa Mungu, anayeonesha uso wake kama Bwana na mwokozi mwenye nguvu zote, kwa upande mwingine, matendo yaliyofichwa ya mamlaka yenye nguvu, tayari kuua bila aibu. Je, si hivyo ndivyo inavyotokea leo? Katika makutano yao kuna ishara ya Yesu: kutoa uhai wa mtu. Ni ishara inayopata kivuli chake kwa  Lazaro aliyefufuka, unabii wa karibu zaidi wa kitakachomtokea Kristo katika mateso yake, kifo, na ufufuko. Katika Pasaka hiyo, Mwana atakamilisha kazi ya Baba kwa nguvu ya Roho Mtakatifu: kama vile mwanzoni mwa wakati Mungu alivyowapa uhai viumbe kutoka katika kitu, vivyo hivyo katika utimilifu wa wakati anakomboa uhai wote kutoka katika kifo, ambacho kinaharibu uumbaji. Kutoka katika ukombozi huu kuna furaha ya imani na nguvu ya ushuhuda wetu, kila mahali na kila wakati.

Misa ya Papa huko Monaco
Misa ya Papa huko Monaco   (@Vatican Media)

Historia ya Yesu kiukweli inafupisha historia yetu sote

Hakika, historia ya Yesu inafupisha historia yetu sote, ikianza na wadogo na waliokandamizwa zaidi: Hata leo, ni hesabu ngapi zinazofanywa duniani ili kuwaua wasio na hatia; ni sababu ngapi za uongo zinazodaiwa kuwaondoa! Hata hivyo, mbele ya kuendelea kwa uovu, haki ya milele ya Mungu inasimama, ambaye hutukomboa kila wakati kutoka makaburini mwetu, kama ilivyokuwa kwa Lazaro, na kutupatia uzima mpya. Bwana hutuweka huru kutokana na maumivu kwa kututia matumaini, hubadilisha ugumu wa moyo kwa kubadilisha nguvu kuwa huduma, hasa kama anavyoonesha jina la kweli la uweza wake mkuu: huruma. Ni huruma inayookoa ulimwengu: inajali kila mwanadamu, tangu wakati inapotungwa tumboni hadi mwisho wake, na katika udhaifu wake wote. Kama Papa Francisko alivyotufundisha, utamaduni wa huruma unakataa utamaduni wa kutupa na kubagua.

Sauti ya manabii:waabuduo miungu hawaoni mbali

Sauti ya manabii, ambayo tumesikia, inathibitisha jinsi Mungu anavyotekeleza mpango wake wa wokovu. Katika somo la kwanza, Ezekieli anatangaza kwamba kazi ya Mungu huanza kama ukombozi (Eze 37:23) na inatimizwa kama utakaso wa watu (Ez 37, 28): safari ya uongofu, kama ile tunayopitia wakati wa Kwaresima. Ni mpango unaovutia, si wa kibinafsi au wa mtu binafsi, unaobadilisha uhusiano wetu na Mungu na jirani yetu. Kwanza kabisa, ukombozi huchukua umbo la utakaso kutoka kwa "miungu," kutoka katika "machukizo" (Eze 37, 23). Ni nini? Kwa neno hilo, nabii anarejea vitu vyote vinavyofanya moyo kuwa mtumwa, vinavyoununua na kuuharibu. Neno miungu linamaanisha "wazo dogo," yaani, maono yaliyopungua, ambayo hupunguza si tu utukufu wa Mwenyezi, na kumgeuza kuwa kitu, bali pia akili ya mwanadamu. Kwa hivyo, waabudu miungu hawaoni mbali: wanaangalia kinachovutia macho yao, na kuyafunika.

Misa ya Papa huko Monaco
Misa ya Papa huko Monaco   (@Vatican Media)

Onyo kuhusu makuu na mema kugeuka miungu na utumwa

Na hivyo, vitu vikubwa na vizuri vya dunia hii vinakuwa miungu, vikibadilishwa kuwa aina za utumwa si kwa wale wanaovikosa, bali kwa wale wanaojifurahisha navyo, na kuwaacha wengine katika taabu na huzuni. Kwa hivyo uhuru kutoka katika miungu ni ukombozi kutoka nguvu ambayo imekuwa utawala, kutoka utajiri unaogeuka kuwa uchoyo, kutoka katika uzuri uliofichwa kama ubatili. Mungu hatuachi katika majaribu haya, lakini huwasaidia wanyonge na wenye huzuni, wanaoamini kwamba miungu za ulimwengu zinaweza kuokoa maisha yao. Kama Mtakatifu Agostino anavyofundisha, "Mwanadamu huwekwa huru kutoka katika utawala wao anapomwamini Yule ambaye, ili kumwinua, alitoa mfano wa unyenyekevu."(De civitate Dei, VII, 33). Mfano huu ni maisha halisi ya Yesu, Mungu alimfanya mwanadamu kwa ajili ya wokovu wetu. Badala ya kutuadhibu, anaangamiza uovu kwa upendo wake, akitimiza ahadi nzito:"Nitawasafisha; watakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wao" (Ezekieli 37:23). Bwana hubadilisha historia ya ulimwengu kwa kutuita kutoka kwenye ibada ya miungu hadi imani ya kweli, kutoka kifo hadi uzima.

Mbele ya ukosefu wa haki

Kwa hivyo, Papa alisisitiza kwamba, mbele ya dhuluma nyingi zinazowajeruhi watu na vita vinavyowagawanya mataifa, sauti ya nabii Yeremia inainuka kila mara, ikitangazwa leo kama zaburi:"maana nitageuza masikitiko yao kuwa furaha, nami nitawafariji, na kuwafurahisha waache huzuni zao (Yer 31:13).

Utakaso kutoka  ibada ya miungu, unaowafanya watu kuwa watumwa wa wengine, unatimizwa kama utakaso, zawadi ya neema inayowafanya watu kuwa watoto wa Mungu,kaka na dada kwa kila mmoja. Zawadi hii inaangazia wakati wetu wa sasa, kwa sababu vita vinavyomwaga damu ni matunda ya ibada ya miungu ya nguvu na pesa. Kila maisha yaliyovunjika ni jeraha kwa mwili wa Kristo. Tusije tukazoea mapigano ya silaha, na picha za vita! Amani si usawa tu wa nguvu; ni kazi ya mioyo iliyosafishwa, ya wale wanaomwona mwingine kama ndugu wa kulindwa, si adui wa kushindwa.

Misa ya Papa huko Monaco
Misa ya Papa huko Monaco   (@Vatican Media)

Kanisa la Monaco linatwa kutoa ushuhuda kwa kuishi amani katika baraka

Kanisa la Monaco Papa alisema limeitwa kutoa ushuhuda kwa kuishi katika amani na baraka za Mungu: kwa hivyo, amewaomba wapendwa hao, wafurahisheni wengi kwa imani yao wakionesha furaha ya kweli, ambayo haipatikani kwa kamari, bali kwa kushirikishwa kupitia upendo. Chanzo cha furaha hii ni upendo wa Mungu: upendo kwa maisha, wadogo na wahitaji, wa kukaribishwa na kutunzwa daima; upendo kwa maisha, vijana kwa wazee, wa kutiwa moyo katika majaribu ya kila kizazi; upendo kwa maisha, wenye afya njema na wagonjwa, wakati mwingine peke yao, wanahitaji utunzaji kila wakati. Bikira Maria, Msimamizi , awasaidie kuwa mahali pa kukaribishwa, pa heshima kwa wadogo na maskini, pa maendeleo kamilifu na fungamani.

Misa ya Papa huko Monaco
Misa ya Papa huko Monaco   (@Vatican Media)

Katika Kwaresima ndefu ya dunia

Katika Kwaresima ndefu ya dunia, kama vile hasira mbaya na ibada za miungu zinavyofanya mioyo isijali, Bwana huandaa Pasaka yake. Ishara ya tukio hili ni mwanadamu: ni Lazaro, aliyeitwa kutoka kaburini; ni sisi, tuliosamehewa wenye dhambi; ni Aliyesulubiwa na Kufufuka, mwanzilishi wa wokovu. Yeye ndiye "njia, kweli, na uzima" (Yn 14:6), anayedumisha hija yetu na utume wa Kanisa duniani: kutoa uzima wa Mungu. Kazi tukufu na isiyowezekana bila kutoa maisha yetu kwa wengine. Kazi yenye shauku na matunda, wakati Injili inaangazia hatua zetu,” Papa alihitimisha.

MISA PAPA HUKO MONACO

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

28 Machi 2026, 16:44