Tafuta

2026.03.25Ujumbe kutoka "Mpango wa Mahusiano ya Wakristo na Waislamu barani Afrika(PROCMURA), 2026.03.25Ujumbe kutoka "Mpango wa Mahusiano ya Wakristo na Waislamu barani Afrika(PROCMURA),   (@Vatican Media)

Papa Leo XIV:Wakristo na Waislam tujibidishe kukuza amani!

Akikutana na Uwakilishi wa Mpango wa Mahusiano ya Wakristo na Waislam barani Afrika,Jumatano Machi 25,kabla ya Katekesi ya Papa Leo XIV alisema:“Kanisa Katoliki linatoa wito wa uelewano na heshima kwa wafuasi wa dini zingine,likithibitisha kwamba"halikatai chochote kilicho cha kweli na kitakatifu katika dini hizo kwani "mara nyingi huakisi mwanga wa ukweli huo unaowaangazia wanaume na wanawake wote.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV kabla ya Katekesi yake, Jumatano asubuhi tarehe 25 Machi 2026, alikutana na Ujumbe wa “Mpango wa Mahusiano ya Wakristo na Waislam barani Afrika” (PROCMURA.) Katika hotuba yake kwa Lugha ya Kiingereza, aliwatakia amani na makaribisho ya joto kidugu. Alitoa shukrani zake kwa kujitolea kwao kukuza udugu kati ya Wakristo na Waislamu kupitia mpango huo,  yenye makao yake makuu nchini Kenya. Vile vile alilishukuru Baraza la Kipapa la Majadiliano ya Kidini kwa huduma yake ya kujitolea, ambayo huwezesha Kanisa kusonga mbele katika mazungumzo na wafuasi wa dini zingine, na kukuza amani na roho ya udugu miongoni mwa wote.

Mpango wa mahusiano ya wakristo na waislamu barani Afrika
Mpango wa mahusiano ya wakristo na waislamu barani Afrika   (@Vatican Media)

Baba Mtakatifu Leo XXIV alisema kuwa Kanisa Katoliki linatoa wito wa uelewano na heshima kwa wafuasi wa dini zingine, likithibitisha kwamba "halikatai chochote kilicho cha kweli na kitakatifu katika dini hizi," kwani "mara nyingi huakisi mwanga wa ukweli huo unaowaangazia wanaume na wanawake wote" (Nostra Aetate, n. 2). Hakika, kila safari halisi kuelekea umoja na ushirika inayofanywa na Wakristo na watu wenye mapenzi mema ni kazi ya Roho Mtakatifu na inahitaji mioyo iliyo wazi kukutana na mazungumzo ili kukumbatiana katika udugu wa kweli (taz. Unitatis Redintegratio, n. 4).

Mpango wa Wakristo na Waislamu Barani Afrika
Mpango wa Wakristo na Waislamu Barani Afrika   (@Vatican Media)

Katika suala hilo, Papa Leo XIV aliongeza kusema “mazungumzo yenu yanayoendelea na Baraza la Kipapa ni ishara chanya, ikiwaita Wakristo, wakiongozwa na upendo wa Kristo, kukuza ushirika na kuimarisha kujitolea kwetu kwa ushirikiano wa Wakristo na Waislamu kwa ajili ya manufaa ya wote.” Kupitia juhudi hizo, amani, haki na matumaini vitazidi kushamiri katika jamii za Kiafrika na kwingineko. “Vile vile ninaamini kwamba mikutano hii itazaa matunda kupitia kushiriki mipango ya msingi ili kukuza urafiki wa kijamii, kuimarisha ushirikiano, na utambuzi wa pamoja wa maeneo hayo yanayohitaji hatua za haraka.” Papa Leo XIV aidha alikazia kusema kuwa katika Ulimwengu unaozidi kuangaziwa na itikadi kali za kidini, mgawanyiko, na migogoro, ushuhuda wenu wa pamoja unaonesha kwamba inawezekana kuishi na kufanya kazi pamoja kwa amani na maelewano, licha ya tofauti za kiutamaduni na kidini.

Mpango wa Wakristo na Waislamu barani Afrika
Mpango wa Wakristo na Waislamu barani Afrika   (@Vatican Media)

Kama alivyowambia Wakuu na Wawakilishi wa Dini za Dunia katika maadhimisho ya miaka sitini ya Nostra Aetate, “tuna jukumu kubwa "la kuwasaidia watu wetu kujitenga na minyororo ya ubaguzi, hasira na chuki; kuwasaidia kuondoa ubinafsi; kuwasaidia kushinda uchoyo unaoharibu roho ya mwanadamu na dunia. Kwa njia hii, tunaweza kuwaongoza watu wetu kuwa manabii wa wakati wetu,  sauti zinazolaani vurugu na dhuluma, kuponya mgawanyiko, na kutangaza amani kwa kaka na dada zetu wote (Hotuba, 28 Oktoba 2025). Kwa mawazo hayo, Papa Leo XIV aliwakabidhi mipango yao kwa maongozi ya Mungu, akiwaombea  baraka nyingi, ili wapate kuwa mafundi wa amani, mashuhuda wa matumaini, na wajenzi wa udugu wa kweli. Na alihitimisha kwa kuelezea furaha yake ya kukutana nao asubuhi huo na kwamba. Mungu awabariki wote.

Mkutano wa Papa na Wwakilishi wa Mpango wa Wakristo na Waislami
Mkutano wa Papa na Wwakilishi wa Mpango wa Wakristo na Waislami   (@Vatican Media)
PAPA WAKRISTO NA WAISLAM

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

25 Machi 2026, 11:09