Tafuta

Papa Leo XIV:Hata sisi Yesu anapaza sauti,njoo huku nje,ondokana na ubinafsi na vurugu!

Katika Dominika ya 5 ya Kwaresima,Machi 22,2026,Papa akitafakari Injili ya Ufufuko wa Lazaro,alisema:“Simulizi hiyo inatualika kujiweka katika usikivu huo wa kina,hitaji na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu,kuondoa ndani mwetu mazoea,hali za kulazimishwa,na mitindo ya kufikiri ambayo kama jiwe la kusagia,tunajifungia katika kaburi la ubinafsi,vitu vya kimwili,vya vurugu na ujuujuu.Katika maeneo haya,hakuna maisha,bali ni mahangaiko tu,kutotosheka na upweke.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Dominika hii ya tano ya Kwaresima, katika Liturujia inatangazwa Injili ya Ufufuko wa Lazaro (Yh 11,1-45). Katika mchakato wa safari ya kwaresima, hii ni ishara ambayo inazungumza ushindi wa Kristo juu ya kifo na zawadi ya maisha ya milele ambayo tunapokea kwa Ubatizo (KKK 12.65). Yesu leo hii anatwambia hata sisi, kama Marta dada yake na Lazaro: “mimi ni ufufuko na uzima, aniaminiye mimi, hata akifa ataishi,” yeyote anaishi na kuniamini, hatakufa milele(Yh 11,25-26).

Umati wa waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro
Umati wa waamini katika Uwanja wa Mtakatifu Petro   (@Vatican Media)

Mahusiano ya muda mfupi yanatujaza mioyo yetu kana kwamba hatufi milele

Liturujia inatualika namna ya kuishi mwanga huu, katika Juma Takatifu ambalo linakaribia, matukio ya Mateso ya Bwana, kuingia Yerusalemu, Karamu Kuu, kushtakiwa, kusulibiwa, kuzikwa, ili kujua maana zaidi ya kina na kutufungulia neema ambayo inafungwa ndani mwake. Ni katika Kristo mfufuka kiukweli, Papa alisisitiza, mshindi katika mauti na anaishi ndani mwetu kwa neema ya ubatizo, ambao katika matukio hayo unapata ndani mwake ukamilifu, kwa ajili ya wokovu wetu na ukamilifu wa maisha.  Neema yake inaangazia ulimwengu huu, ambao unaonekana kutafuta mambo mapya na mabadiliko kila mara, hata kwa gharama ya kutoa vitu muhimu wakati, nguvu, maadili, mapendo, kana kwamba umaarufu, mali, burudani, mahusiano ya muda mfupi yanaweza kujaza mioyo yetu au kutufanya tusife milele.

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Simulizi ya Lazaro inatuweka kwenye usikivu wa kina

Ni dalili za hitaji lisilo na mwisho ambalo kila mmoja wetu analichukua ndani mwake, ambamo jibu lake, lakini haliwezi kukabidhiwa kile kinachopita. Hakuna cha mwisho ambacho hakitofautiani na kiu yetu ya ndani, kwa sababu sisi tumeumbwa kwa ajili ya Mungu na hatutapata amani hadi tutakapopumzika ndani mwake (Agostino-Maungamo I,1.1) Simulizi ya ufufuko wa Lazaro, kwa hiyo Baba Mtakatifu aliongeza, “inatualika kujiweka katika usikivu huo wa kina, hitaji na kwa nguvu ya Roho Mtakatifu, kuondoa ndani mwetu mazoea, hali za kulazimishwa, na mitindo ya kufikiri ambayo kama jiwe la kusagia, tunajifungia katika kaburi la ubinafsi, vitu vya kimwili, vya vurugu, na ujuujuu. Katika maeneo haya, hakuna maisha, bali ni mahangaiko tu, kutotosheka na upweke.”

Sala ya Malaika wa Bwana
Sala ya Malaika wa Bwana   (@Vatican Media)

Tutembee kama wanawake na wanaume wenye uwezo wa kitumaini na kupenda upeo

Papa Leo XIV aliendelea kukazia kwamba: “Hata sisi, Yesu anapaza sauti “Njoo huku nje! (Yohane 11,43), akituchochea kutoka nje, kwa kupyaishwa kwa neema yake kutoka nafasi zile nyembamba, ili kutembea katika mwanga wa upendo, kama wanawake na wanaume wapya wenye uwezo wa kutumaini, na kupenda ule mtindo wake wa upendo usio na mwisho, bila kuhesabu na bila  kupima.” Kwa kuhitimisha Baba Mtakatifu alisema Bikira Maria atusaidie kuishi namna hii siku hizi takatifu: kwa imani, kwa kumwamini, kwa uaminifu wake, ili nasi tupyaishwe kila siku, uzoefu angavu wa kukutana na Mwanae Mfufuka.

TAFAKARI PAPA 22 MACHI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

22 Machi 2026, 12:10