Tafuta

2026.03.26 Papa amemteua Askofu Mpya Msaidizi wa Jimbo Kuu la Nairobi Kenya Msh.Padre Obed Muriungi Karobia,O.F.M. Conv. 2026.03.26 Papa amemteua Askofu Mpya Msaidizi wa Jimbo Kuu la Nairobi Kenya Msh.Padre Obed Muriungi Karobia,O.F.M. Conv. 

Papa Leo XIV amemteua Askofu Msaidizi,Jimbo Kuu Katoliki la Nairobi,Kenya

Padre Obed Muriungi Karobia,O.F.M.Conv,ambaye hadi uteuzi huo alikuwa Mratibu Mkuu wa Chama cha Waamini Wafransiskani Walei wa Watumishi wa Malkia,Mama wa Upendo,Jimbo la Ngong,Kenya.Alizaliwa tarehe 29 Juni 1979.Alipewa Daraja la Upadre mnamo tarehe 28 Julai 2012.

Vatican News

Baba Mtakatifu Leo XIV tarehe 26 Machi 2026, amemteua Askofu Mpya Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Nairobi nchini Kenya, Mhesh.Padre Obed Muriungi Karobia,O.F.M. Conv,ambaye hadi uteuzi alikuwa Mratibu Mkuu Wafransiskani wa Jumuiya ya Watumishi wa Maria Malkia Mama wa Upendo inayunganisha mapadre na ndugu, Jimbo la Ngong, kwa kupewa makao ya Timida.

Wasifu wake

Padre Obed Muriungi Karobia, O.F.M. Conv., alizaliwa tarehe 29 Juni 1979. Majiundo yake: Falsafa katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Bonaventure huko Lusaka, nchini Zambia, alipata Shahada ya Kwanza katika Taalimungu kutoka Chuo Kikuu cha Tangaza (Kenya). Alijiunga na Conventi ya Kifransiskani ya Ndugu Wadogo Wakonvetuali na kufungua nadhiri za daima tarehe 10 Oktoba 20210 na   akapewa Daraja la Upadre mnamo tarehe 28 Julai 2012.

Nyadhifa

Ameshikilia nafasi mbali mbali, kuanzia na kuwa: Makamu Paroko wa Parokia (2012-2013) na Paroko (2013-2016) wa Parokia ya Mtakatifu Catherine wa Alexandria jijini Nairobi; Mkurugenzi wa Miito  na Msimamizi wa Ndugu Wadogo Wakonventuali, Kenya (2012-2019);

Msimamizi na Mweka hazina wa Nyumba ya Malezi ya Shirika lake,  jijini Nairobi (2016-2019); Mkuu wa Kanda ya Wakonventuali ya Ndugu Wadogo Wafransiskani,  Kenya (2019-2023); Rais wa Shirikisho la Afrika la  Ndugu Wadogo  Wakonventuali (2020-2023); Mwanafunzi wa Uzamivu katika Saikolojia, Chuo Kikuu cha Daystar jijini Nairobi; na tangu 2025, kwa agizo la Baraza la Kipapa la Uinjilishaji amekuwa Mratibu Mkuu wa Jumuiya ya Wafransiskani wa Watumishi wa Maria Malkia Mama wa Upendo Jimbo la Ngong(wanaunganisha mapadre na ndugu.

UTEUZI WA ASKOFU WA NAIROBI

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

26 Machi 2026, 17:12