Tafuta

Mitra na kikofia cha kiaskofu Mitra na kikofia cha kiaskofu 

Papa Leo XIV amemteua Pd.Coulibaly,kuwa Askofu wa Sikasso,Mali

Askofu Mteule Noël Bernard Coulibaly,alizaliwa tarehe 17 Desemba 1976.Baada ya majiundo yake ya kikuhani alipewa daraja la upadre tarehe 6 Julai 2002,kwa ajili ya Jimbo la Sikasso nchini Mali.

Vatican News

Baba Mtakatifu tarehe 19 Machi 2026 alimteua Padre Noël Bernard Coulibaly, kuwa Askofu wa Jimbo Katoliki la Sikasso nchini Mali, na  ambaye hadi uteuzi huo alikuwa ni Mwekahazina na Mratibu wa Caritas Jimbo.

Wasifu wake

Mheshimiwa Padre Noël Bernard Coulibaly alizaliwa tarehe 17 Desemba 1976, huko Niono, katika Jimbo la Sikasso (Mali). Alisoma Falsafa na kupata Shahada ya Kwanza katika Taalimungu katika Seminari Kuu ya Mtakatifu Agostino  huko Bamako.

Alipewa daraja la Upadre mnamo tarehe 6 Julai  2002, kwa ajili ya Jimbo la  Sikasso.

Alifunika nyadhifa mbalimbali huku akiendelea na masomo kama ifuatavyo: Parokia ya Mama Yetu wa Fatima, Jimbo la Sikasso (2002-2003); Msimamizi (2003-2004) na Paroko (2004-2006) wa Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Lourdes huko Sikasso (2003-2004); Shahada ya Uzamili katika Uhandisi wa Maendeleo ya Mitaa katika Chuo Kikuu Katoliki cha Lyon; Mshirika katika Parokia ya Mtakatifu Christophe Lès Annonay, Jimbo la  Viviers, Ufaransa (2006-2009); hadi uteuzi huo alikuwa Mwekahazina wa Jimbo la Sikasso na Mratibu wa Caritas Jimbo (tangu 2009).

19 Machi 2026, 16:28