Tafuta

2026.03.08 Angelus

Papa Leo XIV achukua umiliki wa nyumba katika Jumba la Kitume

Msemaji Mkuu wa Ofisi ya Habari ya Vatican alithibitisha hili kwa waandishi wa habari.Alasiri Machi 14 kulifanyika kuhama kutoka Jumba la Ofisi Takatifu,ambapo Papa Leo XIV aliishi wakati wa miezi 10 ya kwanza ya upapa wake.

Vatican News

"Mchana wa leo, Papa Leo XIV alihamia katika nyumba yake katika Jumba la Kitume, akiwa pamoja na washirika wake wa karibu, katika nafasi zilizokuwa zikikaliwa na watangulizi wake hapo awali." Hili limethibitishwa, Jumamosi alasiri tarehe 14 Machi 2026 na Bwana Matteo Bruni, Msemaji Mkuu wa  Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Kiti Kitakatifu.

Hadi sasa, Papa Leo XIV alikuwa akiishi katika Jumba la Ofisi Takatifu, ambapo aliishi alipokuwa Mkuu wa Baraza la Kipapa la  Maaskofu. Nyumba ya Papa, ambayo sasa imekarabatiwa, iko katika (loggia ya  Tatu ) yaani (jengo linaloonekana kwa nje) la Jumba la Kitume. Ina nafasi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na chumba cha faragha, ambapo Papa anafika kwa ajili ya kusali sala ya  Malaika wa Bwana katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, Maktaba, na kikanisa kidogo.

Papa wa kwanza kuisha katika nyumba hiyo alikuwa Pio X  (1903-1914)

Papa Leo XIV mnamo tarehe 11 Mei 2025 alikuwa amefungua tena Nyumba ya Papa katika Jumba la Kitume, akiondoa mihuri iliyobandikwa mnamo Aprili 21 kufuatia kifo cha Papa Francisko, ambaye alikuwa amechagua kuishi katika Nyumba ya Wageni ya Mtakatifu Marta. Na Papa wa kwanza kuanzaa kuishi katika maeneo haya ya Loggia  ya  Tatu,  alikuwa Mtakatifu Pio X (1903-1914).

PAPA KUHAMIA JUMBA LA KIPAPA

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here.

14 Machi 2026, 17:36