Papa Leo XIV aaga Ufalme wa Monaco na kurudi Roma
Vatican News
Helikopta iliyombeba Baba Mtakatifu Leo XIV ilianza safari yapata saa 11:25 jioni hivi. Zaidi ya saa nane baada ya kuwasili kwake, asubuhi ya Jumamosi tarehe 28 Machi 2026, Baba Mtakatifu alihitimisha Ziara yake ya Kitume ya kwenda Ufalme wa Monaco, ikiwa ni ziara yake ya pili ya Upapa kuwa nje ya nchi na ya kwanza barani Ulaya.
Hafla ya kuaga ilifanyika kwenye Uwanja wa Helikopta wa Monaco, kwenye mandhari nzuri ya bahari. Baada ya kuwasalimu wenyeji wake na ujumbe wa Monaco katika ukumbi, Papa Leo XIV alipitia Walinzi wa Heshima na kuwaaga: Mfalme Albert II na Malkia Charlene. Mazungumzo mafupi yalifanyika kati yao, ikifuatiwa na salamu na shukrani kwa makaribisho waliyopokea.
Kisha Papa Leo XIV alipanda helikopta. Ndege ilipaa kutoka ardhi ya Monaco yapata saa 11:30 jioni na ndani ya dakika chache ilikuwa iko juu ya usawa wa Bahari. Katika telegramu iliyotumwa kwa Mfalme Albert II, Papa Leo XIV alitoa shukrani zake za dhati kwa Mfalme, familia ya kifalme, serikali, na watu wote wa Monaco: "kwa mapokezi ya joto na ukarimu" uliotolewa wakati wa ziara yake ya kitume. "Ninaomba, kwamba Mungu Mwenyezi awabariki nyote kwa amani na nguvu," aliandika Papa na kuhitimisha kwa kuwapatia baraka zake. Helikopta aliyopanda ilitarajiwa kutua kwenye Uwanja wa Herikopta wa Vatican takriban masaa mawili ya safari.
Kwa njia hiyo Papa baada ya kuaga Ufalme huo, alisafiri na Helikopta iliyotua kwenye Uwanja wa Helikopta wa Vatican yapata saa 1:00 usiku, masaa ya Ulaya.
Habari hii imesasishwa saa 3.31 usiku, saa za Ulaya.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.
