Tafuta

Papa Leo XIV kwa vijana ajibu maswali:Jihadhari na misisimko na msiogope kujitoa!

Papa Leo XIV akijibu maswali ya vijana wa Monaco kuhusu imani na mashaka,wakiwa mbele ya Kanisa la Mtakatifu Devota aliwashauri kusikiliza na kujitoa kikamilifu kwa Bwana na wengine.Mfano wa Carlo Acutis na Mtakatifu Devota uwasaidie kufika kuabudu “Ekaristi kama njia kuu ya kwenda Mbinguni.”

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Leo XIV akiwa katika Ziara yake ya Kitume katika Ufalme wa Monaco, Jumamosi tarehe 28 Machi 2026, alikutana na Vijana waliokusanyika katika Uwanja wa Kanisa la Mtakatifu Devota huko Monaco. Akianza hotuba yake mara baada ya kusikiliza maswali ya wawakilishi wa vijana, awali ya yote alielezea alivyofurahi kuwa pamoja nao na kuwasalimia wote. “Ninamshukuru Askofu Mkuu kwa maneno yake mazuri. Kama alivyosisitiza, Kanisa ambalo tumekusanyika limejitolea kwa ajili ya Mtakatifu Devota, Mlinzi Mtakatifu wa Ufalme wa Monaco: mwanamke kijana jasiri aliyeshuhudia imani yake mbele ya vurugu za watesaji wake, hata kufikia hatua ya kuuawa kishahidi. Mwili wake, kutoka Corsica, ulifika hapa kwa njia ya Mungu, katika kile ambacho sasa ni pwani ya Wamonaco."

Papa kwa vijana na wakatekumeni wa Monaco
Papa kwa vijana na wakatekumeni wa Monaco   (@Vatican Media)

Kanisa la Mtakatifu Devota limeunganishwa na Mtakatifu Carlo Acutis,kijana aliyempenda Yesu

Papa Leo XIV aliendelea kuwa,  “walitaka kumwangamiza, kufuta kumbukumbu zote zake, na badala yake sadaka yake ilibeba ujumbe wa Injili wa amani na upendo zaidi. Hii inatusaidia kutafakari ukweli kwamba wema una nguvu kuliko uovu, hata wakati, mwingine, unaonekana kuwa mbaya zaidi ya hali hiyo. Zaidi ya hayo, pia inatukumbusha kwamba ushuhuda wa imani ni mbegu inayoweza kufikia na kurutubisha mioyo na maeneo ya mbali  zaidi ya matarajio na uwezekano wetu wenyewe.”  Papa Leo XIV alisema,  “katika Kanisa hili, kumbukumbu ya Mtakatifu Shahidi Devota hivi karibuni iliunganishwa na ile ya Mtakatifu Carlo Acutis, kijana mwingine aliyempenda Yesu, mwaminifu kwa urafiki wake na Kristo hadi mwisho, licha ya nyakati na njia tofauti kabisa: katika upendo, katika utume wa mtandaoni, ambao tunamheshimu kama mlinzi, na hatimaye katika ugonjwa.

Papa akimsalimia mmoja wa Kijana aliyeuliza swali
Papa akimsalimia mmoja wa Kijana aliyeuliza swali   (@Vatican Media)

Benjamin:Namna gani ya kuepuka visumbufu vya ulimwengu?

Wapendwa vijana, Papa Leo XIV aliendelea,   watakatifu hawa wawili wanatutia moyo na kutuhimiza kuwaiga. Hata leo, kiukweli, kama ilivyokumbukwa, imani hukutana na changamoto na vikwazo, lakini hakuna kinachoweza kuficha uzuri na ukweli wake. Ushuhuda wa hili ni idadi inayoongezeka ya wanaume na wanawake wa rika zote wanaotamani kumjua Bwana na kutafuta Ubatizo.

"Umezungumzia haya yote katika ushuhuda wako, Papa alimgeukia  “Benjamin, ambaye ninamshukuru kwa alichoshirikisha, kwani yeye anauliza jinsi ya kuepuka kuvutwa kutoka kwetu, kutoka kwa wengine, na kutoka kwa Mungu na masumbufu ya ulimwengu, wetu, unaoendelea kubadilika. Swali lake ni muhimu, na linahusu kipengele cha msingi cha maisha ya Kikristo: uhai wa uhusiano wetu na Kristo na, ndani yake, hisia ya umoja ambayo huundwa ndani yetu na pamoja na wengine. Mwalimu mkuu wa vijana, katika suala hili, alisema kwamba, "mzizi wa umoja wa maisha uko moyoni, [...] ni ukweli wa moyo, ni zawadi kutoka kwa Mungu, inayotakiwa kuombwa kwa unyenyekevu" (C.M. MARTINI, Kutoka Bethlehemu hadi Moyo wa Mwanadamu, Toleo la Nchi Takatifu, 2013).

Papa amekutana na vijana wa Monaco
Papa amekutana na vijana wa Monaco   (@Vatican Media)

Enzi za Kisasa na utajiri wake:Utamaduni,dawa na afya,Teknolojia na Mawasiliano

Baba Mtakatifu Leo XIV aliendelea kusisitiza, "Enzi za kisasa na za baada ya usasa zimetutajirisha kwa mambo mengi mazuri, zikitoa vichocheo na uwezekano ambao haukuwahi kujulikana hapo awali katika ngazi nyingi: kuanzia utamaduni hadi dawa na afya, kuanzia teknolojia hadi mawasiliano. Hata hivyo,  Papa Leo XIV  alisisitiza, pia zinatuletea changamoto kubwa, ambazo hatuwezi kuzipuuza na ambazo lazima tuzikabili kwa uwazi na ufahamu."  Kama Benjamin alivyosema, Lala aliongeza "tunaishi katika ulimwengu ambao unaonekana kuwa na haraka kila wakati, wenye hamu ya mambo mapya, mcha Mungu wa utelezi usio na mipaka, unaooneshwa na hitaji la karibu,  la lazima la mabadiliko ya mara kwa mara: katika mitindo, mwonekano, katika mahusiano, katika mawazo, na hata katika vipengele vya mtu ambavyo ni muhimu kwa utambulisho wake. Lakini kinachoipatia nguvu maisha ni upendo: uzoefu wa msingi wa upendo wa Mungu, kwanza kabisa, na kisha, kwa upanuzi, uzoefu wa kuelimisha na utakatifu wa upendo wa pande zote."

Mmoja wa kijana aliyeuliza swali
Mmoja wa kijana aliyeuliza swali   (@Vatican Media)

Kupendana kunahitaji uwazi wa ukuaji wa mabadiliko na uaminifu

Na kupendana, huku Baba Mtakatifu alisisitiza, kwa upande mmoja kukiwa kunahitaji uwazi wa ukuaji na kwa hivyo mabadiliko, kwa upande mwingine kunahitaji uaminifu, uvumilivu, na nia ya kujitolea katika maisha ya kila siku. Ni kwa njia hiyo tu ambapo kutotulia kunaweza kupata amani na utupu wa ndani ambao Andrea alizungumzia kujazwa, si kwa vitu vya kimwili na vya muda mfupi, hata kwa idhini ya mtandaoni ya maelfu ya watu wanaopendwa, au kwa ushirikiano wa hali ya juu, ubandia, na wakati mwingine hata wa vurugu. Lazima tuondoe mambo haya katika mioyo yetu, ili hewa yenye afya na oksijeni ya neema iweze kuburudisha na kuhuisha vyumba vyake, na ili upepo mkali wa Roho Mtakatifu uweze kujaza tena tanga za uhai wetu, ukisukuma kuelekea furaha ya kweli. Haya yote, wapendwa, yanahitaji sala, nafasi za ukimya, na kusikiliza, ili kunyamazisha msisimko wa kutenda na kusema, wa jumbe, mizunguko, na mazungumzo, na kuimarisha na kuonja uzuri wa kuwa pamoja kiukweli na kwa uhalisia.

Vijana na wakatekumeni wa Monaco
Vijana na wakatekumeni wa Monaco   (@Vatican Media)

Mtakatifu Carlo Acutis alizungumzia Ekaristi kama Njia ya kwenda Mbinguni

Katika suala hilo, Mtakatifu Carlo Acutis alizungumzia Ekaristi kama "njia kuu ya kwenda Mbinguni" na Ibada ya Ekaristi kama jua, lenye uwezo wa kuifufua roho. Pia kunaweza kuwa na jibu hapa kwa swali la Ethan kuhusu kujiandaa kwa Ubatizo usiku wa Pasaka: kuishi Juma Takatifu katika kutafakari mafumbo ya Mateso, katika mazingira ya kusikiliza sauti ya Roho na kinachotokea moyoni mwa mtu, na kuifanya fursa ya mapitio ya utulivu na ya kina ya maisha ya mtu, yaliyopita na ya sasa. Na ikiwa hii ni muhimu kwa maisha ya kiroho na sala, ni kweli pia kwa utendaji wa upendo.

Ethan aliuliza:Tunawezaje kutoa ushuhuda wa zawadi ya uzima tulipokea katika Kristo?

Ethan aliuliza jinsi tunavyoweza kutoa ushuhuda wa zawadi ya uzima tunayopokea katika Kristo; na Sophie aliuliza jinsi tunavyoweza kuwa mashuhuda wa matumaini kwa wale ambao, wakiwa wameguswa na mateso, wanahatarisha kupoteza nuru na faraja ya imani. Alipokabiliwa na changamoto, Yesu alipendekeza: “Msijali jinsi mtakavyosema  […], si ninyi mnaosema, bali ni Roho wa Baba yenu asemaye kupitia kwenu”(Mt 10:19-20). Alikuwa akimaanisha mateso yaliyoteswa kwa ajili ya Injili, lakini tunaweza kutumia maneno yake katika hali yoyote ambayo upendo unatutaka tukabiliane na mtihani mkubwa kwetu na kwa wengine. Maneno na ishara za ushuhuda na matumaini hazijapangwa, na hatujipatii wenyewe: vinatokana na uhusiano wa kina na Mungu, ambapo kwanza tunapata majibu ya msingi ya maisha. Ikiwa njia ya kitendo chake ndani yetu iko wazi, na ikiwa kubadilishana kwa pande zote kumefunguliwa, ambapo tunafanya uhusiano huu wa upendo kuwa zawadi ya kawaida na ya pamoja, tunaweza kuwa na uhakika kwamba maneno sahihi na nguvu zinazohitajika kutenda zitakuja, kwa wakati unaofaa.

Vijana wa Monaco
Vijana wa Monaco   (@Vatican Media)

Monaco ni nchi nzuri, lakini uzuri wa kweli unatoka kwenu mnapowatazama wanaoteseka

Kwa maana hiyo Papa Leo XIV alisema kwamba "tunaweza pia kusoma kifungu kizuri, lakini wakati mwingine kisichoeleweka, cha Mtakatifu Agostino: "Penda na ufanye utakavyo" (Katika Barua kwa Ioannis wa Parthos, 7, 8). Upendo, yaani, kuwa zawadi ya bure kwa Mungu na wengine; kuwa karibu, usiondoke, hata wakati huwezi kutatua matatizo yote na kurekebisha matatizo yote katika upendo na imani. Monaco ni nchi nzuri, lakini uzuri wa kweli unatoka kwenu, mnapowatazama wale wanaoteseka au wale wanaohisi kutoonekana katikati ya taa za jiji, Papa alisema. "Hivi ndivyo Mtakatifu Devota alivyopata nguvu ya kutoa maisha yake kikamilifu, na hivi ndivyo Mtakatifu Carlo Acutis alivyoishi njia yake ya utakatifu, akiacha njia ya mwanga hata katika ulimwengu wa mtandao," Papa alibainisha. "Wapendwa vijana, msiogope kutoa kila kitu, wakati wenu, nguvu zenu, kwa Mungu na kaka na dada zenu, ili kujitoa kikamilifu kwa ajili ya Bwana na kwa ajili ya wengine." Ni kwa njia hiyo  tu mtapata raha mpya na maana zaidi katika maisha. Ulimwengu unahitaji ushuhuda wenu ili kushinda hali zisizotabirika za wakati wetu na kukabiliana na changamoto zake, na zaidi ya yote kugundua upya wema wa upendo kwa Mungu na jirani

Ulimwengu unahitaji ushuhuda wenu ili kushinda hali zisizotabirika za wakati wetu

Papa Leo XIV akiwageukia wengine alisema: “Kwenu vijana Wakatekumeni, mnaojiandaa kwa ajili ya Ubatizo, na kwenu ambao tayari mmepokea zawadi hii ya neema, ninawatakieni matashi yangu mema ya dhati: muishi maisha kamili na ya kweli katika Kristo; na muwe, kwa ajili ya mema ya wote, katika imani, tumaini, haki,na upendo, wajenzi wa amani. Ninyi  ndiyo uso wa ujana wa Kanisa hili na Serikali."  Papa aliongeza: "Monaco ni nchi ndogo, lakini inaweza kuwa maabara kubwa ya mshikamano, na dirisha la matumaini." Papa Leo XIV aliwaomba wapeleke Injili katika chaguo zao  za kitaaluma, katika kujitolea kwao kijamii na kisiasa, ili kutoa sauti kwa wale ambao hawana, wakieneza utamaduni wa utunzaji. "Fanyeni kila kitu kuwa zawadi ya Mungu na muishi kila kitu kama utume, mnaowaita kuwa marafiki katika Kristo na wenzi waaminifu kwa kila mmoja katika safari. Kwa kuhitimisha Papa Leo XIV, aliwakabidhi kwa maombezi ya Maria Mama yetu,  Mtakatifu Devota, na Mtakatifu Carlo Acutis. Na kuwapatia Baraka zake za dhati.

Vijana wakicheza ngoma ya kiutamaduni
Vijana wakicheza ngoma ya kiutamaduni   (@Vatican Media)

Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata taarifa mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku:Just click here.

28 Machi 2026, 16:08