Papa,Ponte Mammolo,Jumuiya iliyo karibu na Ndugu wafungwa wa Rebibbia
Vatican News
Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu huko Ponte Mammolo (kupitia Casal de Pazzi, 88) itatembelewa na Papa Leo XIV Dominika ijayo tarehe 15 Machi 2026. Hii itakuwa ziara ya tano ya Papa kwenye Parokia, na itifaki hiyo itafuata kimsingi ile ya mikutano iliyopita: Papa atawasili yapata saa 10:00 jioni na atakaribishwa na watoto, vijana, na familia zao katika uwanja wa Parokia hiyo atatoa hotuba. Kisha ataingia kwenye kumbi za parokia na kuwasalimia wagonjwa, uwakilishi wa maskini na wasio na makazi wanaotumia vifaa vya kuogea katika eneo la Parokia. Watu wa kujitolea wa Caritas na Jumuiya ya Mtakatifu Egidio wanaowatunza pia watakuwepo.
Misa na Mikutano
Tena, saa 11:00 jioni, Papa Leo XIV ataongoza Ibada ya Misa, akiwa pamoja na Kardinali Vicar Baldo Reina, Askofu Mteule Marco Valenti, Paroko Padre Francis Refalo, na Mapadre wengine wa Parokia Pia atakuwepo Padre Giuseppe Argento, Paroko wa zamani wa parokia wa jumuiya hiyo ambaye asili yake ni Agrigento; na Padre Yesu, kijana Mhispania ambaye aligundua wito wake wa kipadre alipokuwa akihudhuria jumuiya ya Ponte Mammolo alipokuwa Italia kwenye programu ya Erasmus. Mwishoni mwa maadhimisho Papa Leo XIV atakutana na Baraza la wachungaji la Parokia na hatimaye na mapadre wanaofanya kazi na kuishi katika Parokia. Hatimaye, atawasalimu waamini walio nje ya Kanisa na kisha atarudi Vatican.
Ukaribu na Wafungwa wa Rebibbia
"Habari ya kwamba Papa angetutembelea ilikuwa ya kugusa moyo sana," alikumbuka Paroko wa Parokia Padre Francis Refalo, mwenye asili ya Malta, ambaye kila mtu anamwita kwa upendo "Don Franz." "Watu wengi, hata wale ambao kwa kawaida hawahudhurii parokia, walijitokeza na kutaka kusaidia. Mwali wa moto uliwaka ndani yao." Gereza la Rebibbia pia liko ndani ya eneo la parokia. "Ukaribu huu ni wito maalum wa parokia yetu," kasisi anasisitiza. Sio kwa bahati kwamba tuko hapa; ni ukweli ambao lazima tuitikie. Kuna hamu ya kujenga vyumba vya masomo kwa wale walio kwenye msamaha."
Jumuiya ya makabila mengi
Uangalifu mkubwa utakuwa kwa "ndugu zetu walio magereza," lakini pia kwa wazee, wagonjwa, na vijana, ambao kituo cha majira ya joto kimefunguliwa tena. Wageni wengi pia wanaishi katika eneo hilo, kutoka nchi za Asia kama vile Ufilipino, Bangladesh, na Pakistan, lakini hasa kutoka Amerika Kusini, nchini Peru. "Familia ya Peru inayokuja mara kwa mara Parokiani kwetu kila siku itashiriki katika ofa," alisisitiza Padre Franz. "Wana binti wa miaka 12, ambaye atapokea sakramenti za ukatekumeni wakati wa Mkesha wa Pasaka." Parokia inawafikia wahamiaji katika eneo hilo kwa njia nyingi tofauti: pamoja na Kituo cha Kusikiliza, na pamoja na shule ya lugha ya Kiitaliano kwa wageni, inayofanya kazi kwa miaka ishirini, "ambayo sio tu husaidia katika ujumuishaji lakini pia inakuwa aina ya usindikizaji," alisisitiza Padre wa Parokia.
Asante kwa kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku bonyeza hapa: Just click here
