Tafuta

2026.03.09 Nembo na Kauli mbiu ya Ziara ya Kitume ya Papa Leo XIB katika Ufalme wa Monaco 2026.03.09 Nembo na Kauli mbiu ya Ziara ya Kitume ya Papa Leo XIB katika Ufalme wa Monaco  

Ziara ya Kitume ya Papa huko Monaco:Ratiba Rasmi imechapishwa!

Ziara ya Kitume ya Papa XIV katika jiji-Serikali ya Ulaya mnamo Machi 28 itadumu kwa takriban saa tisa.Papa atakutana na Mfalme Albert,Jumuiya ya Wakatoliki,vijana,na wakatekumeni na ataongoza Misa katika Uwanja wa Louis II.Nembo na kauli mbiu,iliyochukuliwa kutoka Injili ya Yohane,pia imetolewa:“Je suis le Path,la Verité et la Vie,” "Mimi ndimi njia na ukweli na uzima."

Vatican News

Ofisi ya Habari ya Vatican imewakilisha na kuchapisha Jumatatu tarehe 9 Machi 2026, Ratiba, Nembo na Kauli mbiu ya Ziaya ya Hija ya Kitume ya Baba Mtakatifu Leo XIV katika Ufalme wa Maonaco, inayotarajiwa kufanyika Jumamosi tarehe 28 Machi 2026, siku moja, lamba ya kuingia Juma Kuu Takatifu.  Hii itakuwa safari ya takribani saa tisa, iliyojaa mikutano minne, ikianza na mmoja na Mfalme Albert, kisha na jumuiya ya Wakatoliki na vijana na wakatekumeni, na Misa ya mwisho katika Uwanja wa Louis II.

Ziara ya Kwanza Barani Ulaya

Na ni ziara yake ya kwanza kwa Papa Leo Barani Ulaya na ya kwanza kati ya safari zake za kigeni katika nusu ya kwanza ya 2026 (ikifuatiwa na safari ndefu kwenda Afrika mwezi Aprili na safari kwenda Hispania mwezi Juni). Kauli mbiu: Je suis le Chemin, la Verité et la Vie – “Mimi ni njia, ukweli na maisha (Yh 16,6). Yaani, kifungu kilichochukuliwa kutoka Injili ya Yohane kinasisitiza ukweli kwamba Papa anakuwa mbebaji wa Kristo mwenyewe na ujumbe wake. Ziara ya Papa itaanza kwa kutembelea familia ya kifalme. Kuondoka Vatican kwa helikopta kumepangwa saa 7:00 asubuhi; kuwasili Monaco  saa 3:00 asubuhi, kufuatiwa na mapokezi rasmi na sherehe katika Jumba la Kifalme. Katika makazi ya kale, yenye usanifu wake wa Baroque na Renaissance, ziara ya heshima kwa mkuu itafanyika, ikifuatiwa na salamu kutoka kwa Papa, hotuba ya kwanza kati ya nne za ziara  hiyo.

Papa ataongoza hata misa katika Uwanja wa Mchezo Louis II

Ya pili ni mahubiri, ambayo Papa Leo  XIV atayatoa mbele ya jumuiya ya Wakatoliki, ambao atakutana nao saa 5:00 asubuhi katika Kanisa Kuu la Bikira Maria Asiye na Dhambi. Mkutano huu utafuatiwa, dakika 45 baadaye, na mkutano na vijana na makatekumeni katika eneo lililo mbele ya Kanisa la Mtakatifu Devote, mahali pa ibada ya Wakatoliki wa karne ya 19 katika Mtaa wa Condamine, makao ya  Parokia yenye jina moja katika Jimbo Kuu la Monaco. Papa Leo XIV pia  atatoa hotuba katika tukio hilo. Baada ya mapumziko ya chakula cha mchana na mapumziko mafupi, Papa atahamia Uwanja wa Louis II, ambacho ni kiwanja cha michezo kilichopewa jina la Mfalme Louis II, aliyetawala kuanzia 1922 hadi 1949, ambapo Monaco inacheza michezo yake ya nyumbani na ambayo inaandaa michuano ya Ligue 1 ya Ufaransa. Hapo Baba Mtakatifu ataongoza Misa na kutoa mahubiri. Baada ya maadhimisho Papa ataondoka katika Ufalme wa  Monaco baada ya sherehe rasmi ya kuaga katika Heliport. Kuondoka kumepangwa kufanyika saa 11:45 za jioni , saa mbili baadaye atafika Roma.

Bango linalomkaribisha Papa Leo XIV katika Ufalme wa Monaco
Bango linalomkaribisha Papa Leo XIV katika Ufalme wa Monaco

Ufafanuzi wa Nembo

Nembo hiyo, juu kushoto, ina picha nyeusi na nyeupe ya Baba Mtakatifu, akitabasamu na kubariki, amevaa mavazi ya kiliturujia, kofia,(Mitria) na Fimbo ya Kichungaji, likionesha mwelekeo wa kiroho na kichungaji wa ziara hiyo. Kulia, sanamu iliyochorwa ya mnara wa Jumba la Kifalme la Monaco, ikikumbusha utambulisho na uhuru wa Ufalme huo. Mnara huo ni wa manjano hafifu kabisa, hivyo sehemu nzima ya juu, inayoonekana kwa ujumla, inakumbuka bendera ya Vatican. Sehemu ya chini imekaliwa kabisa na maandishi yanayotangaza ziara hiyo, yaliyotawaliwa na jina "Léon XIV," lililowekwa kwa herufi kubwa katikati, na neno "Monaco," ambayo inajitokeza kwa rangi nyekundu angavu ya bendera ya taifa na nembo ya kifalme. Chini kuna kauli mbiu: "Je suis le Chemin, la Verité et la Vie" yaani Mimi ni Njia, Ukweli na Njia (Yh 14:6), ambayo inaonesha kwamba Papa ndiye mbebaji wa Kristo mwenyewe na ujumbe wake. Kwa ujumla, nembo hiyo inaakisi umbo la Papa na utume wake wa kitume, sambamba na hali ya ukarimu wa Ufalme, ambayo dini yake ya serikali ni Ukatoliki.

Asante kusoma makala yetu. Unaweza kuendelea kupata habari mpya kwa kujisajili kwa jarida letu la kila siku. Just click here.

09 Machi 2026, 16:00